Dar leo wapasua jipu lingine la ufisadi

mmzalendo

Senior Member
Nov 1, 2010
165
1
UJERUMANI YASITISHA KUTOA FEDHA ZA KUPAMBANA NA UKIMWI -TZ
WIZARA ya Maendeleo ya Ujerumani imetangaza kwamba itasitisha kutoa fedha kiasi cha euro milioni 200 ambazo hutolewa kila mwaka kwa mfuko unaopambana na maradhi ya UKIMWI,kifua kikuu na
Malaria duniani kutokana na kuwepo kwa tuhuma za ufisadi.
Waziri wa Maendeleo wa Ujerumani, Dirk Niebel amesema katika taarifa yake kwamba,hatua hiyo inachukuliwa ili maswali kadhaa muhimu yaliyojitokeza kuhusiana na kazi za shirika hilo ili yaweze kufanyiwa uchunguzi wa kina.
Hivi karibuni, vyombo vya habari viliarifu kuwa mamilioni ya dola katika shirika hilo yametumika vibaya na kwamba udhibiti wa kufuatilia michango inayotolewa ni mdogo au haupo kabisa.
Ujerumani ni nchi ya tatu inayotoa kiasi kikubwa cha fedha katika shirika hilo la kupambana na maradhi ya Malaria, UKIMWI pamoja na TB.

PAMBANA NA UFISADI

kuna habari njema blogs ya www.lifeofmshaba.com ina rusha article zote kwa hiyo kama unaona article yako inafaha kuwafikia wasio wana forum itume kwenda info@lifeofmshaba.com
 
Aaah wasitishe tu, kwani tunajiweza bwana. kwa nini tusaidiwe kwa ajili ya mijifisadi kadhaa tu. Heri pesa zao wakanunue mvinyo wanywe na wake na waume zao. Kuna maana gani kulagahai wtz kwa ujinga huku wakitafuna fedha za watu kwa jina la wa TZ.
 
wewe serikali gani kwenye bajeti ya 12 trilioni kwenye maendeleo kuna rtilioni 3 tu. nani atakubali kutoa pesa yake ten wajameni?
 
Kuna kipindi walikuwa pia wanatoa scholarships kwenye chuo cha elimu ya watu wazima wakasimamisha kwa sabu ya ufisadi. Peas ilikuwa haiwafikii walengwa.
 
Back
Top Bottom