Dar Kuna mgao wa umeme wa kimya kimya?

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
2,173
2,000
Wakuu ni siku ya tatu sasa mtaa ninaokaa huku Kimara umeme unakatwa masaa 8 Hadi zaidi kwa siku

Nauliza ni mtaa wa kwetu tu ama Ni sehemu nyingine? Isije ikawa Ni mgao wa umeme umeanza kimyakimya
 

Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Sep 29, 2016
6,018
2,000
Kuna maboresho ya miundombinu yanafanyika, muwe wavumilivu
Maboresho huwa yanatolewa taarifa na matangazo na watu wanakaa wanaelewa.

Sasa kukata kimya kimya na kwa muda mrefu kwa lengo lolote ni dharau, hivi kwanini waTanesco hawajifunzi?

Mpaka leo watendaji hamjajirekebisha tu!

Mmeanza tena kuchezea sharubu za Kalemani?
Anafukuzaga kama mbwa bila kujali, msije kusema hamumjui!
 

funzadume

JF-Expert Member
Jan 28, 2010
11,007
2,000
Ni kweli Kimara umeme unakatwa kila siku. Nina biashara mitaa ya kule yaani mpaka nataka niifunge. Inategemea umeme 100%. TANESCO ni jipu baya sana nchini na ni kama limeshindikana. Nadhani wabadilishe Mkurugenzi Mtendaji aje mtu makini
 

nyakisese

Member
May 3, 2020
87
125
Kuna transifoma ina leta shida na si mara moja yaani kero mna weza kaa hata siku 2 bila umeme na Tanesco Wana kuja na gari yao! Sasa sijui shida nini
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
17,598
2,000
Ninaposhinda na ninapolala ni sehemu mbili tofauti na kote hakujawahi kua na shida unayoisema.

Ni kwenu tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom