Dar: Kivuko Kipya cha MV KAZI chazinduliwa, Kimeundwa Tanzania!!

SALOK

JF-Expert Member
Sep 20, 2011
3,134
2,000
Kama ndoto vile ila ndo hivyo yametimia!! Kivuko cha kisasa chazinduliwa kilichojengwa hapa hapa Tanzania, na watanzania wenyewe!!
Labda ndio matokeo ya kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda!!

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amepokea Kivuko cha MV Kazi kutoka kwa Kampuni ya kizalendo ya M/S Songoro Marine Transport Boatyard ya Mwanza iliyokuwa inafanya kazi ya ujenzi wa Kivuko hicho mara baada ya ujenzi wake kukamilika.

Akizungumza na wananchi, Prof Mbarawa alisema lengo la Serikali kuongeza Kivuko hicho ni kuboresha huduma za kusafirisha abiria na magari kati ya Magogoni na Kigamboni.

“Uwepo wa vivuko vitatu kutasaidia utoaji wa huduma kwa wakati na kwa urahisi na ikitokea Kivuko kimoja kimepelekwa kufanyiwa ukarabati huduma zitaendelea kama kawaida bila kuathiri utaratibu wa kawaida”.Alisema Prof Mbarawa.

Ameongeza kuwa ili kuendana na kasi ya Mhe. Rais John Magufuli Wizara yake itaendelea kuboresha huduma za Vivuko katika Mikoa mingine ikiwemo Mkoa wa Lindi , Kivuko cha Pangani, na Kivuko cha Kigongo Busisi Mkoani Mwanza.

Nae Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Dkt. Mussa Mgwatu alisema Kivuko cha MV Kazi kimejengwa kulingana na viwango vinavyotakiwa Kimataifa na ukaguzi wake umefanywa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) na kuthibitishwa kuwa ni salama kwa ubebaji wa abiria na magari.

Ujenzi wa MV KAZI umegharimu Shilingi Bilioni 7.3 za Kitanzania na kina uwezo wa kubeba abiria 800 magari 22 sawa na jumla ya tani 170.

Kivuko hicho kimekabidhiwa leo kwa ajili ya kuanza kutoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni Jijini Dar es salaam na kuongeza idadi ya vivuko katika eneo hilo kufikia vitatu.

Na. Eliphace Marwa
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,550
2,000
kimetengenezwa na watanzania au kimeunganishwa na watanzania...???..

kutengeneza = design+manufacturing+assembling+testing+commissioning.
kuunganisha = assembling+testing +commissioning.

kuunganisha kwa engineer yeyote mwenye uzoefu kwenye kazi husika sio tatizo na ukizingatia michoro ipo ni kama kuunganisha makabati ya kichina tu...
 
ginnery

JF-Expert Member
Nov 9, 2016
200
250

Naamini kimetengenezwa hapa mkuu kuna jamaa anaitwa songolo marine huyu bwana afai ametengeneza vivuko vingi tu hapa nchini na vinapiga kazi vizuri tu pongezi kwake
 
Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
6,964
2,000
Taasisi /kampuni au kiwanda gani iliyotengeneza kivuko? Nina imani kwa serikali, bilioni 7 si nyingi, na kama inachukua mwaka kukiunda/kukitengeneza, basi suluhisho kwa sehemu mbalimbali Tz zinazohitaji vivuko ni kama limekwisha.
 
Nyangomboli

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
3,158
2,000
kimetengenezwa na watanzania au kimeunganishwa na watanzania...???..

kutengeneza = design+manufacturing+assembling+testing+commissioning.
kuunganisha = assembling+testing +commissioning.

kuunganisha kwa engineer yeyote mwenye uzoefu kwenye kazi husika sio tatizo na ukizingatia michoro ipo ni kama kuunganisha makabati ya kichina tu...
Kimetengenezwa na Songoro kijana wa Sengerema.
 
N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
4,923
2,000
Acheni dharau hao wazungu wenyewe gari likikamilika linakuwa na brand name ya nchi husika wakati parts zinaundwa nchi tofautitofauti...Mchina juzi kazindua ndege kubwa ya abiria injini kaagiza Ulaya....Rolls Royce body parts zinaundwa sehemu tofauti na injini yet ni brand ya Uingereza...Hapa kwetu mzawa Gallery - SONGORO MARINE TRANSPORT LTD. BOATYARD anaunda meli,boti,vivuko vya kila sample hata meli kule nyasa imeundwa hapahapa home...tatizo hatuna appreciation kwa sababu tuzijuazo hebu tuthamini kilichoundwa nyumbani,hatushindwi na tusijidharau...Hicho kinakuwa branded made in Tanzania,proudly Tanzanian.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom