Dar: Kivuko cha MV Magogoni chagonga boti ya uvuvi

kiboksi manyoya

JF-Expert Member
Nov 16, 2016
377
311
Leo muda wa 05:25 alfajiri eneo la bahari upande wa Kigamboni, Kivuko cha MV Magogoni kilichokuwa kinatoka Kigamboni kwenda upande wa Magogoni kimegonga boti ya uvuvi iliyokuwa inatoka ferry soko la samaki kwenda Kigamboni eneo la encorage,

Watu waliokuwa kwenye boti walijitosa baharini huku boti hiyo ikiburuzwa na MV Magogoni kwa umbali kadhaa na baadae MV Magogoni ilisimama na kuiacha boti ikielea bila uelekeo maalum, wajuzi wa sheria za bahari watueleze nani mwenye makosa kati ya MV Magogoni na boti ambayo ilitaka kupita mbele ya kivuko ambacho kiko kwenye mwendo, ilikuwa ni usiku sikuweza kupiga picha.
 
Kwa haraka haraka naona kama wavuvi walipaswa kusimama ili kupisha pantoni ipite. Maana kwa hali ya kawaida pantoni si rahisi ikasimama ghafla ghafla tena katikati ya maji.
 
Lile pantoni linavyoenda polepole pengine wenye boti walihisi wangeliwahi.

MV Magogoni likiharibika utasikia kuliweka sawa miezi nane... Hiki kipindi chote mtasukumana kama mbuzi zizini.
 
Binaadamu watu wa ajabu sana,Daraja lipo unahatarisha maisha kwa kupanda kivuko,na oili hizi za kichina? Sitapanda kivuko ng'o
 
Back
Top Bottom