DAR: Kituo cha mabasi Mwenge chahamishiwa Makumbusho

DAR: Kituo cha mabasi Mwenge chahamishiwa Makumbusho

mkuzi

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2013
Posts
1,627
Reaction score
1,462
Dar es Salaam. Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imetangaza kuhamisha kituo maarufu cha daladala cha Mwenge kwenda eneo la Makumbusho.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, ofisa mfawidhi wa Sumatra wa Kanda ya Mashariki, Conrad Shio alisema Kituo cha Mwenge kitafungwa rasmi Jumapili na eneo hilo litabaki wazi kupisha upanuzi wa Barabara ya Ali Hassan Mwinyi. Shio alieleza sababu ya kuhamisha kituo hicho kuwa ni ufinyu wa eneo lenyewe jambo linalosababisha magari kushindwa kuingia kituoni hapo kwa wakati, hasa nyakati za asubuhi na jioni. Hali hiyo husababisha foleni kubwa isiyo ya lazima.

Alisisitiza madereva wote kutii agizo hilo kuanzia Jumatatu na kwamba atakayekiuka agizo hilo atachukuliwa hatua kali za kisheria. Pia, aliwataka abiria kutolazimisha kushushwa katika eneo hilo wakati hakuna kituo. Shio aliongeza kuwa barabara za kuingia na kutoka Kituo cha Makumbusho bado zinakarabatiwa na Manispaa ya Kinondoni ili kurahisisha uingiaji na utokaji wa magari katika kituo hicho.

Hivi karibuni, madereva wa daladala zinazofanya safari kati ya Mwenge, Tegeta na Ubungo waligoma kutoa huduma kushinikiza Serikali kueleza kituo mbadala baada ya kufungwa kwa kituo cha Ubungo kutokana na ujenzi unaoendelea wa barabara.
 
serikali chenga tu sasa watu wanaofanya kazi maeneo ya mwenge washukie wapi
 
si wangesubiri kwanza hizo barabara zinazokarebatiwa zikamalizika ,kuna haja gani ya kuhakisha?
 
Mafisadi wakiwa ndio viongozi kila kitu hovyo,wao hawapandi daladala ndio maana wanafanya watakavyo.Kama wangejua matatizo ya kuhamisha kituo,wangekuwa tayari kuwalipa fidia wenye nyumba za karibu kuongeza eneo la stendi
 
tunatoa zogo sehemu moja na kulihamishia kwingine
 
Back
Top Bottom