Dar: Kinondoni kutengeneza Mtaa maalum wa Baa tu

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
“Kinondoni nina mpango wa kutengeneza mtaa mmoja maalum wenye bar tu ili watu wakitaka kwenda kunywa pombe waende mtaa huo bila kubugudhi. Nasubiri muda tu ufike kwa sababu haiwezekani kila eneo liwe na bar mpaka nyuma ya misikiti na nyuma ya makanisa,” ameeleza Makonda.

Unakubaliana nayo hii au unaipinga?

Hivi, Hiyo ni kazi ya baraza la madiwani au mkuu wa wilaya?
 
Makonda aliitisha wenyeviti wa mitaa manispaa ya kinondoni pale leaders club ..akaahidi kuwa anataka garage zote ziwe mtaa mmoja,bar ,machine za mbao,yard za magari , yaani takataka zozote za biashara ziwe na mitaa husiku ..sio unaenda kinondoni unakutana na yard za magari, mbele kuna bar nyuma kuna karakana za vyuma ujakaa vibaya kuna soko yaani vurugu tu.. Ila sasa je hili swala linahitaji budjet ya kutosha kutafuta hayo maeneo ambayo asilimia 100 mengi ni ya wazi ambayo yameuzwa na hao hao wenyeviti wa mitaa wakishirikiana na watu wa idara ya ardhi hapo manispaa ya kinondoni.
 
“Kinondoni nina mpango wa kutengeneza mtaa mmoja maalum wenye bar tu ili watu wakitaka kwenda kunywa pombe waende mtaa huo bila kubugudhi. Nasubiri muda tu ufike kwa sababu haiwezekani kila eneo liwe na bar mpaka nyuma ya misikiti na nyuma ya makanisa,” ameeleza Makonda. Unakubaliana nayo hii au unaipinga??
Hivi,Hiyo ni kazi ya baraza la madiwani au mkuu wa wilaya?
Mkuu ni kweli Dar imejengwa kifujo fujo sana. Lakini njia ya kurekebisha ni kuwa na master plan (kama hakuna) na ifuatwe. Tukiacha wakuu wa wilaya kila mmoja aibuke na Masterplan yake itakuwa ni fujo mara tano. Na ndio maana tunarudi pale pale: Bila serikali kufanya kazi kwa pamoja na kuongozwa na sheria na kanuni nzuri tulizojiwekea hatutaweza kutatua matatizo mengi! Tujijifanya tunaendekeza hii one man show hatutafika popote.
 
Mambo ya red lighst districts
dunia nzima haya mambo yapo...

unapaswa kuwa na eneo maalum ambako watu wanaweza kukesha na kupiga kelele usiku kucha
mchana kutwa....

sheria tulizo nazo zinasema pombe kuuzwa ni kuanzia saa kumi
na mwisho saa tano usiku....

sio kila kitu kupinga sababu ni Makonda kasema
hii idea ni nzuri
 
Mambo ya red lighst districts
dunia nzima haya mambo yapo...

unapaswa kuwa na eneo maalum ambako watu wanaweza kukesha na kupiga kelele usiku kucha
mchana kutwa....

sheria tulizo nazo zinasema pombe kuuzwa ni kuanzia saa kumi
na mwisho saa tano usiku....

sio kila kitu kupinga sababu ni Makonda kasema
hii idea ni nzuri
watu wanapinga hadi fursa.... hapa lazima malaya wajazane huo mtaa kwa sababu itakuwa ni shida tupu...mpaka kuchere hapo..huku ngwasuma kula mzee yusuph pale pembeni baba na wanaye duh!! Makonda huyu dogo akipewa mkoa wa dsm ataupeleka mchaka mchaka hadi basi ..sidhani kama inatakiwa kumpinga kila kitu kisa yeye ni ccm..mambo mengine yanamake sense
 
utaratibu ni mzuri
haukulazimishi kwenda huko kama hutaki
bar zitakuwepo sehemu zingine
isipokuwa hapo zinakuwa masaa 24
nchi zingine hapo sio bar tu hadi madanguro yanakuwa na eneo maalum...
so unakuta mtaa mmoja mreefu una bar ,casino,madanguro na kadhalika

inasaidia malezi mazuri kwa watoto badala ya kuruhusu kila mta uwe na madanguro na ma bar
'massage parlous ' na kadhalika
 
Kuna watu wataona kama makonda amekuwa kichaa, Lakini ukweli kuwa watakuwa hawajaishi nje ya tz,
Haya anayoyasema makonda Ndio utaratibu wa dunia nzima, Kila kitu Kila huduma zinasehemu zake maalum sio Kila sehem unaweza kufanya chochote bila kujali eneo
 
Back
Top Bottom