Dar inawapotezea watu muda

Dar inawapotezea watu muda

nandembako

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2013
Posts
655
Reaction score
528
Nimeishi Dar kwa takribani miaka 13,hakuna cha maana nilichokifanya,ila niliporudi mkoani ndani ya mwaka mmoja maisha yalikuwa tofauti kabisa. Niliacha kufikiria mawazo ya muda mfupi mfano nitakula nini kesho,kodi itakuaje na mengineyo ya kipuuzi..

Sasa hivi nawaza itakuaje baada ya mwaka au miaka kumi nitakuwa wapi. Hilo Dar linaishia kwenye maneno tu,maisha ya Dar yanamfanya mtu awe mtumwa,wana wengi wanaogopa kurudi mahome kwao kwa kuhisi watadharaulika.

Acha fikra potovu rudi ubadili namna ya kufikiri,huku mambo yanaenda ukitia nia.
 
Wengi watakuja kukubeza mtoa mada,ila ukweli wengi walio Dar ni wachumia tumbo,kipato chao chote kinaishia kwenye usafiri,na muda wao mwingi wanaupotezea mabarabarani,hawalali vizuri,wala hakuna sehemu ya kutulia na kuwaza au kupumzika bila bugudha,wengi wanalijua hilo,lkn wakiwaza time waliyoipoteza,wanaona noma kurudisha mpira kwa kipa,bora umewasanua,mimi naamini bado hawajachelewa...hasa kwa wale wenye nia ya kubadilisha maisha yao,maana wengi wao washakata tamaa.
 
Ninyi nyote kwa kifupi mawazo yenu ni finyu na uwezo wa kutoka ndani ya kundi la wajanja hamuwez, kwa kifupi mnarudi kwenye ule msemo wa kizamani kwamba jogoo wa shamba.....niwaulize mnawaza habari ya eti kodi ya nyumba, chakula maji, kwa hio huko mikoani kuna nyumba za bure? Kama kamji kadogo namna hii mnaona ni kupoteza muda inakuwaje ungetupwa jiji kama NY, Milan ama London ukaambiwa utafute connection mtoboe? Wasema Dar ni kupoteza muda lakini tambua nyumba nzuri kushinda zoote Tanzania iko Dar, viwanja vikal viko Dar, Tajiri namba 1 Tanzania yuko Dar, hata gari ya kifahari nchi nzima inaendeshwa Dar..nyie endeleeni kukusanya matembele huko na kujigamba mnamilik nyumba huko ambayo ukiileta dar itathaminishwa na ilioko tandale
 
Baba yangu Mkubwa Anaish Dar mwaka wa 28 huu ndo msomi zaid na mwenye kipato kikubwa zaid ndan ya familia ila ndo maskn zaid kwenye familia yao.

Sitak kuweka maelezo meng Jitahd hvyo hvyo tu unielewe
 
Hana akili, kuna kitu kinaitwa rasilimaliwatu, hii ukiitumia vizuri inakutoa, ukifikiri vizuri, changamoto inaweza kuwa fursa.
 
Ninyi nyote kwa kifupi mawazo yenu ni finyu na uwezo wa kutoka ndani ya kundi la wajanja hamuwez, kwa kifupi mnarudi kwenye ule msemo wa kizamani kwamba jogoo wa shamba.....niwaulize mnawaza habari ya eti kodi ya nyumba, chakula maji, kwa hio huko mikoani kuna nyumba za bure? Kama kamji kadogo namna hii mnaona ni kupoteza muda inakuwaje ungetupwa jiji kama NY, Milan ama London ukaambiwa utafute connection mtoboe? Wasema Dar ni kupoteza muda lakini tambua nyumba nzuri kushinda zoote Tanzania iko Dar, viwanja vikal viko Dar, Tajiri namba 1 Tanzania yuko Dar, hata gari ya kifahari nchi nzima inaendeshwa Dar..nyie endeleeni kukusanya matembele huko na kujigamba mnamilik nyumba huko ambayo ukiileta dar itathaminishwa na ilioko tandale
Gari zuri lipo arusha wewe,,,dar hakuna magari
 
Kwakweli jamaa amenishangaza anavyo generalize..
Amefeli yeye.
Wapo ambao hawawezi kuishi nje ya dar.
 
Ninyi nyote kwa kifupi mawazo yenu ni finyu na uwezo wa kutoka ndani ya kundi la wajanja hamuwez, kwa kifupi mnarudi kwenye ule msemo wa kizamani kwamba jogoo wa shamba.....niwaulize mnawaza habari ya eti kodi ya nyumba, chakula maji, kwa hio huko mikoani kuna nyumba za bure? Kama kamji kadogo namna hii mnaona ni kupoteza muda inakuwaje ungetupwa jiji kama NY, Milan ama London ukaambiwa utafute connection mtoboe? Wasema Dar ni kupoteza muda lakini tambua nyumba nzuri kushinda zoote Tanzania iko Dar, viwanja vikal viko Dar, Tajiri namba 1 Tanzania yuko Dar, hata gari ya kifahari nchi nzima inaendeshwa Dar..nyie endeleeni kukusanya matembele huko na kujigamba mnamilik nyumba huko ambayo ukiileta dar itathaminishwa na ilioko tandale

Majitu ya Dar bhana!
Yaani tajiri namba moja inakuhusu nini wewe unayeishi Gongo la Mboto?
Viwanja vikali wakati unalala sebuleni kwa shemeji yako inakusaidia nin?
Mikoa hatuwasalimii shemeji zetu.....wanaume wa Dar wanagongea sigara kwa shemeji zao!
 
Nimeishi dar kwa takribani miaka 13,hakuna cha maana nilichokifanya,ila niliporudi mkoani ndani ya mwaka mmoja maisha yalikuwa tofauti kabisa...niliacha kufikiria mawazo ya muda mfupi mfano nitakula nini kesho,kodi itakuaje na mengineyo ya kipuuzi....saiv nawaza itakuaje baada ya mwaka au miaka kumi nitakuwa wapi...hilo dar linaishia kwenye maneno tu,maisha ya dar yanamfanya mtu awe mtumwa,wana wengi wanaogopa kurudi mahome kwao kwa kuhisi watadharaulika,acha fikra potovu rudi ubadiri namna ya kufikiri,huku mambo yanaenda ukitia nia.
Ww maisha yalikushinda...
 
Umeelewa ulichoandika?
kama ungejua kua nakipato kikubwa na kua na hela n vitu viwili tofaut usingeuliza hl swali, na kama ungejua unachoingza hakitosh kukufanya kua hela/tajir bali n muunganiko wa unachoingza na matumiz ndo vitaamua hali yako ya maisha basi tungezungumza lugha moja,

jitahd na hapo unielewe kama ukitaka.
 
nyinyi ni waoga wa maisha, maisha popote, kama umeamua kurudisha mpira kwa kipa ni mpango wako kivyako vyako, wengine tumetusua na tunaendelea kutusua hapa hapa bongo daslamu
Huko ni kukalili misemo eti maisha ni popote. Labda kama unataka kuishi tu hapo sawa hata juu ya mti unaweza kuishi lakini kama lengo ni kufanikiwa katika maisha unahitaji kuelewa maeneo ya kukusapoti kufanya hivyo yaani uwe selective tena sana. Maisha ya kiumbe chochote kile na existence yake ni dependable sana katika selection za vitu vingi sana ambavyo ndo vitakavyokuongoza, ukishindwa hili inamaana unazidiwa hata na konokono anayejua wapi ni salama kwake kuishi, lini na kwanini.

Mwanadamu chagua eneo sahihi la kuishi na kufanikiwa na si kuishi tu
 
Back
Top Bottom