A-town
JF-Expert Member
- Oct 25, 2011
- 494
- 169
Leo nimesikitishwa sana na kitendo cha wahudumu wa basi la Dar Express kumnyanyasa mgeni wangu. Safari ilianzia eneo la Mto wa Mbu, mgeni wangu kakata tiketi na kupanda akiwa na mzigo mdogo kama zawadi kwa wenyeji wake. Tangu safari inaanza hakuambiwa kwamba atapaswa kulipia kamzigo kake mwisho wa safari. Safari imeenda mpaka mgeni wangu alipokaribia kushuka kimara mwisho akatoa taarifa kwa mhudumu wa basi. Katika harakati za kushuka akashangaa anaambiwa alipie Tsh 5000/= ya mzigo ambayo haikuwa imesemwa kabla. Mgeni huyo akamwambia mhudumu wa basi kuwa hana hicho kiasi anachokitaka na hata hivyo haikuwa makubaliano. Wakazozana hapo na yule mhudumu na dereva wakaamua kumpitisha kituo yani badala ya kumshusha kimara mwisho wakaenda kumuacha kimara bucha na mzigo wake.
Hapo nimejihoji maswali kadhaa:
1. Hivi gharama za mzigo abiria anashitukizwa wakati wa kushuka?
2. Kama hayo malipo yalikuwa halali kwanini wamshushe bila kulipwa?
3. Kumpitisha abiria kituo chake huku ni mgeni mhudumu husika anayajua madhara yake?
Baada ya kupewa taarifa hizo na mgeni wangu kuwa amepitishwa kituo nilipiga simu ofisini na kueleza Shida yangu,niliambiwa nisubiri wahusika wafike ofisini ili ijulikane nini kilitokea. Mpaka naandika hapa sijapokea taarifa yoyote inayohusu kadhia hiyo. Hali hii inanipa shaka juu ya utendaji wa kampuni hii na thamani ya abiria wake.