Dar es Salaam yaanza kupotea midomoni mwa watu

Podcast

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2018
Posts
842
Reaction score
1,032
DAR ES SALAAM IMEANZA KUPOTEA MIDOMONI MWA WATU..!

Kwanza nianze kwa kutoa salamu kwa jf member wote heri ya mwaka mpya,Pia tushukuru Mungu kutuweka hai mpaka muda huu...!

Kama kichwa cha habari kinavojieleza hapo juu,Kwa hizi sasa umaarufu ambao Dar ulikuwa nao miaka ya nyuma umepotea sana kwa miaka ya hivi karibuni. Kwa miaka za zamani Dar ilisifika kwa vitu vingi sana (NB. Sisemi zamani za kale maana sikuepo)Naongea kuhusu miaka ya kuanzia 2000 kwani ndio miaka ambayo nilianza kusikia kuhusu jiji hili.

Miaka hio ukisikia mtu katoka Dar lazima umtafute umuone anafanana vipi hasa kile kiswahili cha Dar Dar hahahaha! Hatari sana kipindi nakumbuka nilikuwa Mwanza maeneo flan hv panaitwa (iloganzala) basi kuna dogo alikuja kwa ndugu yake katokea Dar basi tulikuwa tunashinda hapo kwao muda wote ilimradi tu tuone watu wa Dar wanavyoishi.

Miaka hio ukiletewa nguo kutoka Dar lazima watu wajue na hata kama hawataki utasema tu "Hii nguo sio ya (sabasaba-Mwanza) imetoka Dar kwa wajanja.

Kipindi hicho mtu ukiwa na safari ya kwenda Dar uwezi lala usiku maana huamini kama kweli utaenda Dar maana unapasikia tu kwenye redio na siku ukifanikisha lazima wataelewa mtaani nikirudi.

Miaka hio watu walikimbilia sana Dar kwa ajili ya kutoka kimaisha wengi waliamini ukifika Dar lazima utusue japo wenyeji wa Dar wengine walikimbilia south..maana walipachoka Dar.nakumbuka kulikuwa na case nyingi sana watu kudandia treni au malori ya mizigo ili kufika Dar lakini sikuizi hakuna tena.

Ukiwa mikoani sasa hivi uwez simama na kusema eti mimi natoka Dar ni bora useme mikoa mingine maana Dar imekuwa na image yake tofauti sana watakuona huenda ukawa mwizi,taperi, muuni au mtu ambae haeleweki hasa pale watakapo kuita mwanaume wa Dar....hahahahah..! Hii ndo inakela sana.

Kwanini nasema Dar Imeanza kupotea midomoni mwa watu.
Hii yote ni kwa sababu watu wameanza kutoka Dar na kurudi mikoani ili kutafuta maisha upya maana Dar hakukaliki tena...shida zimekuwa nyingi sana ajira,kodi,wingi wa watu. nk.
Haya yote yalikuwepo miaka yote lakini kwa sasa yameongezeka mara dufu kuna baadhi ya watu humu wameandika kuhusu maisha yao baada ya kutoka Dar na kwenda mikoani sisemi ukiwa .mikoani lazima ufanikiwe ila namaanisha Dar haisemwi sana kama zamani.
 
Mimi mbona sioni shida kuitwa mwanaume wa Dar maana nyie wanaume wa mikoani ni dhaifu sana kwanza ni wadhaifu kwenye mapenzi, mkisalitiwa ni rahisi sana kujiua au kuwaua wapenzi wenu sababu huko mikoani kwenu mademu ni kitu cha ajabu sana...licha ya mapungufu mengi ya watu wa Dar, bado ipo vile vile ndo maana uliona aliesema anataka kuhama Dar kuhamia Dodoma mpaka leo bado yupo Dar...
 
Dar haiwezi kuisha midomoni kwa watu na hizo flyovers na mwendokasi basi wanatamani wavione vinafafanaje ndio maana bado ni mji wenye watu wengi sana.
 
Dah...Usilinganishe Dar na vitu vya ajabu... Bigi mwenyewe alisema atakayebaki Dar ndiyo mwanaume....na yeye mwenyewe Hadi leo Bado anaisikilizia safari ya Dom....Dar iiache tu Kama ilivyo...[emoji41]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zamani Dar ilikua inaonekana ya maana kwasababu watu wengi walikua hawana exposure ya kujua sehemu zingine zikoje (ujamaa). Sasa hivi watu wamefunguka wanasafiri nje ya nchi na kujionea majiji yalivyo ndio hapo wanagundua kumbe dar ni sehemu ya hovyo kuwahi kutokea duniani. Angalao sasa na vi flyover hivyo viwili vitatu labda itaanza kufanana na majiji ila otherwise kwa mtu ulietembea huwezi thubutu kusema unatokea Dar.
 
Kuishi Dsm ni chuo kikuu tosha

Siku zote binadamu hua anakimbia sehemu ambayo kuna ugumu wa maisha kwenda sehemu yenye urahisi wa maisha. Dar ndio sehemu rahisi kabisa kuishi hapa Tz nandio maana mjinga mjinga yoyote anaweza kukimbia mkoa na kuja hapo na kutoboa. On the contrary, ili utoboe mkoani lazma utumie akili sana na uwe very creative..
 
Si
Dah...Usilinganishe Dar na vitu vya ajabu... Bigi mwenyewe alisema atakayebaki Dar ndiyo mwanaume....na yeye mwenyewe Hadi leo Bado anaisikilizia safari ya Dom....Dar iiache tu Kama ilivyo...[emoji41]

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijaringanisha mkuu nimejaribu kueleza ukweli
 
Back
Top Bottom