Dar es Salaam waigeni Mombasa

falcon mombasa

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
9,186
9,288
Tofauti kati ya kivuko cha kigamboni na kile cha likoni mombasa ni kuwa kubwa kabisa watembea kwa miguu wanavuka bure masaa 24, bali wenye magari huchangia cent kidogo kwa ajili ya kuchangia gharama za uendeshaji.

Pia katika kivuko cha Likoni Mombasa idadi ya ferry ni nyingi zinazokaribia nane ukilinganisha na kivuko cha Kigamboni ambacho kina ferry mbili,tena kubwa moja na ndogo moja.

Kuhusu usalama kila abiria anayetaka kupanda ferry lazima apitishiwe mashine maalum ya kudetect kama anasilaha au lah,pia licha ya wingi wa ferry katika kivuko cha Likon pia life jacket hubadilishwa mara kwa mara pindi zinapoisha muda wake.

Ambapo ferry ya Kigamboni utakutana na life jacket kukuu,hivi leo niwaulize,zile pesa mnazolipa zinafanya nini?ukizingatia serikali ya kenya haiwatozi gharama yoyote wanaotaka kuvuka Likoni.

Msisahau ujenzi wa daraja pia unaendelea hata jijini mombasa.naamini mamayor wapya wa ukawa mtasimamia hili kuondoa gharama za vivuko ni kumyanyasa mtanzania wa hali ya chini kumlipisha ferry.

Chonde chonde UKAWA ndio tumaini pekee lilobaki kwa wakazi wa Kigamboni.
 
Duh!Leo umeamua kuwachokoza wenzako?Unajua vyema hawapendi kuskia chochote kizuri kuhusu Kenya.Waache na ferry zao mbili labda zinawafaa hivo zilivo tu,pesa wanazo za kulipia,shida iko wapi?Ngoja utawaona hapa,wengi wao wataenda nje ya mada watasahau kabisa mambo ya ferry waanze Mombasa oooh,Kenya oooh,sijui aaah!
 
Na mimi nawasubiri niwakate vidomo vyao
 
Ukisema Likoni nakumbuka kile kisa cha pantoni kubinuka........@Mshana jr......hivi ulisikia kile kisa.....?.....eti sababu ilikuwa ni mtu kajitumbukiza baharini watu wakaelemea upande mmoja kumtizama......(ndivyo nilivyosikia).......hii ilileta maruweruwe sana......
 
msisahau ujenzi wa daraja pia unaendelea hata jijini mombasa.
Sawa Mzee, tunaomba updates za daraja la Mombasa:
Kigamboni.jpg

Kigamboni2.jpg
Kigamboni2.jpg
Kigamboni2.jpg
3.jpg
2.jpg

Nadhani ushauri wako uwe daladala za Kigamboni zianze kununua life jackets za kutosha kwa ajili ya abiria!!!
 
Ukisema Likoni nakumbuka kile kisa cha pantoni kubinuka........@Mshana jr......hivi ulisikia kile kisa.....?.....eti sababu ilikuwa ni mtu kajitumbukiza baharini watu wakaelemea upande mmoja kumtizama......(ndivyo nilivyosikia).......hii ilileta maruweruwe sana......
Aaaahaaa
 
Na wewe visa hivyo vya ferry kuzama vipo almost dunia nzima,ni kwa kenya nadhani ndio kilikuwa kisa pekee unlike tanzania,mara mv spaget mara mv spices islander zingine utalist down by your own
 
Na wewe visa hivyo vya ferry kuzama vipo almost dunia nzima,ni kwa kenya nadhani ndio kilikuwa kisa pekee unlike tanzania,mara mv spaget mara mv spices islander zingine utalist down by your own
Najua visa ni vingi......lakini cha Likoni ni cha aina yake......watu kulemea upande mmoja na kuzamisha ferry sio kitendo cha kila siku........
 
Nilishtuka kidogo na heading, nikadhani ni ule utaratibu wao wa kwenda na sime au kisu sokoni
 
Back
Top Bottom