Dar es Salaam: Serikali taabani kifedha 2013/2014

Dar es Salaam: Serikali taabani kifedha 2013/2014

Kwa jinsi hali ilivyo huku mtaani naiamini hii habari bila shaka. Ni muda muafaka kwa serikali kukiri imefilisika ili tujue tunasavaivu vipi...!
Unajua maana ya kufilisika za kuambiwa changanya na za kwako.
 
Serikali ina Fedha nyingi tuu. Kwa sababu wanauwezo wa Kubandua Barabara za Dar es salaam na Kuzijenga upya tena kwa kiwango cha kimataifa. Angalia Morogoro Rd, Mwai Kibaki Rd Old and New(aka Bagamoyo Road). Mikoani ndio usipime nasikia kila kijiji kinaunganishwa kwa Lami au Reli na Viwanja vya Ndege kila Mji. Miradi yote hii si Pesa ya Serikali?

Acha ujuha, hiyo ni mikopo ambayo bado vitukuu wetu watalirithi hilo deni
 
Porojo zingine hazina hata mshiko.

Serikali yenu hii ya kifisadi iko hoi kwakuwa imekuwa legelege katika kukusanya kodi, ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za umma.
Hali ni mbaya sana na muda si mrefu nchi itaporomoka hii kwa sababu ya mandondocha ya ccm na serikali yake.
 
Serikali yenu hii ya kifisadi iko hoi kwakuwa imekuwa legelege katika kukusanya kodi, ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za umma.
Hali ni mbaya sana na muda si mrefu nchi itaporomoka hii kwa sababu ya mandondocha ya ccm na serikali yake.

Wewe yako ipi?
 
Kama Halmashauri ya Urambo wasilete tu hela, Afisa Utumishi fisadi Mr Maganga anakula sana hela na genge lake kama vile hazima mwenyewe. Madiwani wenyewe vilaza wote.
 
Km serikali haina hela, jamaa hakawii kutoka nje ya nchi kuzisaka. Nilikuwa nikijiuliz a siku zote ivi rais wetu anasiku nyingi zaidi alizo kaa nje kuliko zile anazo kaa ndani. safari zisizo na malengo maalum. kila janga likitokea mchini kwake ye hayupo inchini ivi anaishi wapi? mlipuko mbagala hakuwepo,gongo la mboto hakuwepo,viongozi wa dini kuuawa hakuwepo inchini, mabomu yote ya arusha hakuwepo inchini. hadi hapo tusifilisike kwel? mbunge au waziri akikohoa tu kutibiwa nje. mbona Mandela anatibiwa nyumbani! watu gani hatujifunzi,hatuelewi chochote, maneno mengi practical F, madini kibao, mali asili had mlangoni. Bandari tungeweza kuwa nazo zaidi tano zenye uwezo km ya dar, ila sasa du! sijui tupewe nn tukacho weza! wameingia kuinusuru inchi kwa kuongeza kodi kwny simu, hawana hata haya! ukifkiria sana unaweza ingia porini ...
 
Ni wiki chache zilizopita kikao cha Bunge cha bajeti ya 2013/2014 kuanzia July 2013 mpaka June 2014 ndio kimemalizika. Sasa hata mwezi wa kwanza wa mwaka wa fedha wa Serikali haujaisha tayari Serikali imekwishafilisika!!!!

Nchi ina utajiri mkubwa lakini bajeti ya Serikali ya mwaka mzima haimalizi hata mwezi kabla haijafilisika!!! Kweli hii Serikali ni Serikali ya kisanii.


fedha za nje kutoka kwa wafadhili hazijafika.
 
Back
Top Bottom