Dar es Salaam: Serikali taabani kifedha 2013/2014

Dar es Salaam: Serikali taabani kifedha 2013/2014

Bunge Kubwa, serikali watumishi kibao wasio na tija. Ukienda wilayani na wizarani unakuta watu wanapigana vikumbo hata wanachofanya hakijulikani. Punguza wafanyakazi wachovu weka vijana wpya hawa wa vyuoni wapige training wafanye kazi.
 
Hoja zingine kama za wauza ----- vile hana mbele wala nyuma kazi tunayo na watanzania wa namna hii.
 
Kweli serikali hii dhaifu,si juzi tu wamesoma bajeti yao kwa mikogo leo hali mbaya du you can only find this in tz
 
Kama unaona elimu gharama jaribu ujinga make comment yako inaonesha wazi kuwa elimu ya kuchambua mambo hunayo.
Aliyekuambia Elimu Ina Maana Tz nani? Angalia mafisadi wote ni wasomi Ww mwenyewe ni mjinga ebu jiulize akiba ya fedha Hazina imekwenda wapi?na Kama unajidai una Elimu hiyo Elimu yako imeleta manufaa gani kwa janga hili? Usijidai Msomi kiswanglish wewe tafakari kwanza ! au wewe ni wale walionufaika na Pesa ya Obama nini?mbona imekuuma?
 
gambazzzzz na lumumba oyeeeee kina shonza,mtela na mwigulu wamekomba pesa yote kwaajili ya Arusha duuuh so sad aisee.
 
Kama unaona elimu gharama jaribu ujinga make comment yako inaonesha wazi kuwa elimu ya kuchambua mambo hunayo.

Eti na Ww unajiita Msomi !nina mashaka na Ufahamu wako kwani inaelekea ni aina ya wale Wasomi feki waliofaulu kwa kuiba mitihani na kukariri kila kitu ili wapate Vyeti tu! wakati kichwani Hakuna Taaluma yeyote huku wakijitahidi kuzungumza kiswanglish wakidhani English ni Taaluma kumbe ni Lugha ya kawaida tu !kumbuka Taaluma hupatikana ktk lugha mbali mbali Ndio Maana Rais wa Rusia,china,Italy,German nk hawazungumzi English kokote waendako duniani Jitambue usijifanye msomi Tz hapa Hakuna cha usomi tunahitaji Hekima Busara ungwana jumlisha na usomi wa Ukweli si usomi wa kukariri maisha kama wako
 
Mitanzania bwana... Sasa habari ambayo ni positive wao wameiweka negative... Huwezi wekeza kwenye biashara ya duka alafu ukasema hutatoa hata thumni huko...is that true that vile vibanga vya kina mangi hawachukui hela huko... Reality wanachukua na biashara zinaendelea. Serikali imefanya vizuri mashirika yake yawe na taratibu nzuri za kubana matumizi wakijua mwenye kampuni (serikali) anahitaji 10% yake regardless... In long run this is very positive...ingekuwa imefanywa hivi tangu zamani tungekuwa mbali sana.

Haya mabadiliko ni mazuri sana... It will make mashirika ya kufa yanakufa na ya kuendelea yanaendelea as opposite na kutoa ruzuku kila cku... Mashirika yanatakiwa kuhudumia serikali... Sio serikali kuhudumia mashirika.
 
Ina maana bakuli la JK huko nje ya nchi kila siku halijajaa au anaendaga kutalii tu.
Au hizi project za Lameck huwa hazina return ya Cash??
 
Hoja zingine kama za wauza ----- vile hana mbele wala nyuma kazi tunayo na watanzania wa namna hii.

inaelekea wewe unaishi kwa kukariri maisha umekariri unavyoona Ww kumbuka wenzako hawaishi kwa Mazoea wanaenda na wakati Maisha ya kukariri Ndio yanakufanya usiwe na Upeo wa kutambua wenzako wanazungumzia nini?na kipi kifanyike ili kumaliza tatizo?wewe umekariri ujinga tu!
 
Yaani kila jimbo liwe na wabunge wawili??Hainingii akilini kabsa, Kwani wabunge c wanatetea watu wote bila ubaguzi wa jinsia???Kwa hili hawakustahili hata kulipwa sitting allowance kwa kweli. Huu ni uvujaji wa madaraka, na nchi ilivyokubwa c wabunge watafika zaidi ya 1000???
Kwa mapendekezo ya Tume ya katiba mpya wao wanaona kwamba kufuta viti maalum kutasababisha bunge kuwa na Wabunge wanawake wachache sana, hivyo ili kuhakikisha hali hiyo haitokei ndio wamekuja na hilo pendekezo kila jimbo liwe na Wabunge wawili mmoja mwanaume na mwingine mwanamke kwa maana hiyo kuongeza idadi ya Wabunge karibu maradufu ya hawa waliokuwepo katika bunge la sasa, sidhani kama kila mkoa uwe na Wabunge wawili. Ila kama nimekosea ni kila mkoa uwe na Wabunge wawili badala ya kila jimbo basi nitasahihishwa.
 
Hiyo sheria ipo toka zamani ingawa ilikuwa haitekelezwi. Tofauti ni kwamba hapo awali kila shirika lilipaswa kuchangia 10% ya FAIDA yake kwa mwaka, ikaonekana mashirika mengi yana declare faida kidogo kwa kutumia mbinu za kihasibu (creative accounting or earnings management), ndo maana sasa wameamua kuicharge kwenye MAPATO GHAFI. Angalia repoti za CAG miaka iliyopita. Mashirika kamaTANAPA, EWURA, TCRA n.k yanapata hela nyingi sana, matokeo yake wanaishia kujipangia posho kubwa za vikao vya board na perdiems na safari za nje kibao. Wakati rate za posho za kujikimu za juu serikalini ni 80,000, yapo mashirika wajumbe wake wa board wanalipwa hadi 450,000 per day na bado analipiwa tiketi ya ndege, malazi, chakula na vinywaji. Posho za vikao zinafikia hadi 1,000,000 per sitting. Naunga mkono uamuzi wa serikali

Hoja yako ni ya msingi sana Polisi. Ila nadhani serikali kuyadai mashirika haya michango haitoshi. Wakati umefika sasa kwa serikali kutoa mwongozo juu ya uendeshaji wa mashirkia, taasisi, tume na mamlaka za uma.

Ni kweli taasisi hizi zimepewa autonomy/uhuru unaoziwezesha kujiendesha bila kuingiliwa na serikali kuu. Hii ni pamoja na kuwa na mifumo yake ya mishahara, masurufu n.k. Lakini naona uhuru huu sasa umeanza kutumiwa vibaya. Kama mamlaka imeundwa kisheria kukusanya mapato kama ada n.k bado ada hizo ni mali ya watanzania. Wao ni custodian wa tozo hizo na si wamiliki na hawana sababu ya kujivunia.

Hatuna sababu ya kuwa na watumishi wa uma wenye housing allowance, transport allowance, entertainment allowance, communication allowance, tea allowance na zingine ambazo ni aibu kuzitaja wakati wengine hawana eti kwa sababu wao wanazalisha.Si lazima wote walingane lakini uwiano uwe reasonable. Kama watu wana viwango sawa vya elimu na majukumu yanayolingana wasipishane kimaslahi kwa zaidi ya 30%.Hatuwezi kuwa na double standards kwenye masurufu na mishahara ya watumishi kwa kiwango cha kufuru. Yaani kuna wakurugenzi wana mishahara maradufu ya makatibu wakuu!. This is Bullshit!

Lazima msajili wa hazina aweke mipaka ya viwango vya mishahara ambavyo ni reasonable. Haiwezekani Bsc. Telecom wa TCRA alipwe mara tatu ya yule wa TTCL wakati wote ni watumishi wa uma chini ya wizara moja na actually wote wanaiingizia nchi pesa.

La pili ni kuangalia utendaji wa mashirika hayo. Kuna agency zina wakurugenzi wanasafiri nje kwa wiki tatu katika mwezi. This is too much. Something serious needs to be done here!

La mwisho napendekeza tuirejeshee TRA mamlaka ya kukusanya ada na tozo zote za nchi hii zikiwemo za hayo mashirika kama EWURA na baada ya hapo migawanyo na matumizi vifanyike kama ilivyo kwa serikali kuu. Otherwise tunakosa uhakika wa mapato yetu.

Poleni wote mlioguswa kimaslahi. Mi naipenda nchi yangu. Nothing personal to anyone.
 
For similar title, nadhani hii ni single ya 3 au ya 4, sijui bado ngapi ili kutengeneza album!!
 
Ninachoona ni mwandishi wa rusha roho ameingilia mambo asiyoyajua... Mbona huu utaratibu umepitishwa na bunge na uko kwenye bajeti ... Sasa kukusanya kodi ni ishara ya kutokuwa na hela?
 
Nadhani halmashauri kutopata fedha kwa wakati inaweza kuwa imechangiwa sana name tatizo la bajeti tegemezi. Binafsi naunga mkono hatua ya serikali kukusanya kiasi hicho kutoka mashirika ya umma ili wajue kuwa hawapo huko kukusanya pesa ili wajilipe posho kubwa bali kuchangia katika shughuli za serikali.
 
Hoja yako ni ya msingi sana Polisi. Ila nadhani serikali kuyadai mashirika haya michango haitoshi. Wakati umefika sasa kwa serikali kutoa mwongozo juu ya uendeshaji wa mashirkia, taasisi, tume na mamlaka za uma.

Ni kweli taasisi hizi zimepewa autonomy/uhuru unaoziwezesha kujiendesha bila kuingiliwa na serikali kuu. Hii ni pamoja na kuwa na mifumo yake ya mishahara, masurufu n.k. Lakini naona uhuru huu sasa umeanza kutumiwa vibaya. Kama mamlaka imeundwa kisheria kukusanya mapato kama ada n.k bado ada hizo ni mali ya watanzania. Wao ni custodian wa tozo hizo na si wamiliki na hawana sababu ya kujivunia.

Hatuna sababu ya kuwa na watumishi wa uma wenye housing allowance, transport allowance, entertainment allowance, communication allowance, tea allowance na zingine ambazo ni aibu kuzitaja wakati wengine hawana eti kwa sababu wao wanazalisha.Si lazima wote walingane lakini uwiano uwe reasonable. Kama watu wana viwango sawa vya elimu na majukumu yanayolingana wasipishane kimaslahi kwa zaidi ya 30%.Hatuwezi kuwa na double standards kwenye masurufu na mishahara ya watumishi kwa kiwango cha kufuru. Yaani kuna wakurugenzi wana mishahara maradufu ya makatibu wakuu!. This is Bullshit!

Lazima msajili wa hazina aweke mipaka ya viwango vya mishahara ambavyo ni reasonable. Haiwezekani Bsc. Telecom wa TCRA alipwe mara tatu ya yule wa TTCL wakati wote ni watumishi wa uma chini ya wizara moja na actually wote wanaiingizia nchi pesa.

La pili ni kuangalia utendaji wa mashirika hayo. Kuna agency zina wakurugenzi wanasafiri nje kwa wiki tatu katika mwezi. This is too much. Something serious needs to be done here!

La mwisho napendekeza tuirejeshee TRA mamlaka ya kukusanya ada na tozo zote za nchi hii zikiwemo za hayo mashirika kama EWURA na baada ya hapo migawanyo na matumizi vifanyike kama ilivyo kwa serikali kuu. Otherwise tunakosa uhakika wa mapato yetu.

Poleni wote mlioguswa kimaslahi. Mi naipenda nchi yangu. Nothing personal to anyone.
Mkuu nakubaliana na wewe kwa uchambuzi wako uliotulia ila hapo kwenye nyekundu nachelea kuungana na wewe. Mimi bado naona TRA wamerundikiwa mamlaka mengi mno ya kukusanya kodi ambazo zingeweza kukusanywa na taasisi nyingine kwa ufanisi. Nitoe mifano michache
1. Halmashauri zimenyang'anywa vyanzo vingi sana vya mapato. Nyingi zilizoendelea, Halmashauri ndiyo wakusanyaji wakubwa wa mapato na kuipatia serikali kuu, tofauti na kwetu ambapo serikali kuu inakusanya na kuzipatia halmashauri
2. Nchini Rwanda, leseni za magari issue zote zinaishia polisi, then polisi wanasubmit serikali kuu. Hii inaondoa mlolongo wa mlipa kodi kuzunguka na kutumia rasilimali nyingi ku comply kulipa kodi. Yaani nenda TRA, then nenda POLISI, then nenda BENKI halafu urudi TRA tena kwa ajili ya kusubmitt payslip achilia mbali danadana utakazopigwa kufuatilia hiyo leseni
 
Back
Top Bottom