Dar es Salaam: Serikali taabani kifedha 2013/2014

Dar es Salaam: Serikali taabani kifedha 2013/2014

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,685
“Mashirika ya Umma yaagizwa kuchangia asilimia 10 ya mapato yake ili kunusuru hali hiyo” Dar es Salaam. Miradi mbalimbali ya Mashirika ya Umma nchini, iliyopangwa kutekelezwa Mwaka 2013/2014 huenda ikakwama kutokana na uamuzi wa serikali kuagiza mashirika yote hayo yatoe asilimia 10% ya mapato yake kwa kuichangia Serikali…. Taarifa za ndani kutoka Wizara ya Fedha zinasema kwamba Serikal haina fedha kwa sasa ambapo sasa inalazimika kukusanya fedha kutoka katika mashirika yake ili kuendesha shughuli zake. Pia ibainika kuwa Serikali haijapeleke fedha za ruzuku katika halmashauri mbalimbali nchini, pamoja na kushindwa kuwalipa posho wafanyakazi wake maeneo mbalmbali “Miongoni mwa mashirika ya umma yanayoguswa na uamuzi huo wa serikali ni MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII, ikiwamo; NSSF, PSPF, Mamlaka Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Shirika la Ugavi wa umeme (Tanesco), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na mengine kadhaa…” Chanzo: Mwananchi, Jumamosi, Julai 20, 2013 (kwa habari zaidi)
===
Updates: HABARI KAMILI
===
Serikali taabani kifedha

naibu.jpg

Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum

Kwa ufupi
Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi Jumamosi umebaini kuwa tayari Serikali, imetuma waraka kwa mashirika hayo, ambayo hata hivyo baadhi yapo katika hali mbaya kwa sasa kutokana na kushindwa kuendeleza miradi kadhaa ya maendeleo

Dar es Salaam. Miradi mbalimbali ya mashirika ya umma, nchini iliyopangwa kutekelezwa mwakawa fedha 2013/14 huenda ikakwama kutokana na uamuzi wa Serikali kuagiza mashirika yote hayo yatoe asilimia 10 ya mapato yake kwa kuichangia Serikali.
Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi Jumamosi umebaini kuwa tayari Serikali, imetuma waraka kwa mashirika hayo, ambayo hata hivyo baadhi yapo katika hali mbaya kwa sasa kutokana na kushindwa kuendeleza miradi kadhaa ya maendeleo.
Mbali na mashirika ya umma kutakiwa kuchangia fedha kwenye mfuko wa Serikali, Serikali pia haijapeleka fedha za ruzuku katika halmashauri mbalimbali nchini pamoja na kushindwa kuwalipa posho wafanyakazi wake maeneo mbalimbali.
Hali hiyo imesababisha baadhi ya halmashauri kushindwa kuendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyomo kwenye bajeti.
Mtendaji wa moja ya halmashauri mkoani Pwani aliliambia gazeti hili; Kwa sasa kweli hali ni mbaya, hakuna fedha iliyofika kutoka serikalini, hakuna shughuli inayohitaji fedha ambayo inafanyika.
Taarifa za ndani kutoka Wizara yaFedha zinasema kwamba Serikali haina fedha kwa sasa ambapo sasa inalazimika kukusanya fedha kutoka katika mashirika yake ili kuendesha shughuli zake.
Miongoni mwa mashirika ya umma yanayoguswa na uamuzi huo wa Serikali ni mifuko ya hifadhi ya jamii ikiwamo NSSF, PSPF, Mamlaka Udhibiti wa Nishati na Maji(Ewura)Shirika la Ugavi wa Umeme (Tanesco), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa(Tanapa), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro(NCAA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS)na mengine kadhaa.
Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti, baadhi ya wafanyakazi wa Idara za Fedha za mashirika hayo, walieleza kuwa kutokana uamuzi huo wa Serikali sasa wanalazimika kukaa ili kuandaa upya bajeti za mashirika hayo.
Ukweli haya maagizo yana athirikubwa kwetu kwani tayari tulikuwa tumepanga bajeti kutokana na mapato na kwa uamuzi huu ambao kimsingi hakuna mamlaka ya kuyapinga, itabidi tutoe, ila adhari zitakuwepo,alisema ofisa mmoja wa juu wa moja ya mashirika ya umma.
Hata hivyo, alisema kuwa iwapo wangeshauriwa mapema basi walau wangetakiwa kuchangia asilimia tano kwa mwaka huu wa fedha na mwaka ujao ndipo ingeongezeka kufikia asilimia 10.
Ofisa mwingine wa shirika la umma aliyeomba kutotajwa jina alieleza kuwa uchangiaji huo, ulipaswa kutazama mashirika, kwani yapo yanayojiendesha kwahasara, mengine yanapokea ruzuku na mengine yanajiendesha kwa fedha zake.
Uchunguzi wa Mwananchi Jumamosi umebaini kwa Tanapa pekee inatakiwa kulipa Sh24 bilioni, zinazotakiwa kukatwa kutoka kwenye bajeti yao ya kutekeleza miradi ya maendeleo ya shirika na jamii inayowazunguka.
Tumelazimika kupunguza bajeti zetu kwa kiwango kikubwa, maana awali ilikuwa Sh16.2 bilioni walizoelekeza, sasa wameagiza asilimia tatu ya mapato ghafi kwa ajili ya kuchangia shughuli za uendeshaji Serikali.
Shirika linatakiwa kurejea bajeti yake na kupunguza matumizi ya miradi ya maendeleo kwa kiasi cha Sh21 bilioni na zingine zinaongezeka hadi Sh24 bilioni,alisema mmoja wa maofisa hao. Ofisa huyo alisema kuwa licha ya Serikali kutambua ukubwa wa tatizo la ujangili ambalo walielekeza nguvu kwa kupanga kuajiri askari, ununuzi wa magari na vifaa vingine, sasa wataajiri askari wachache na mambo mengine yataachwa.
Hata hivyo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma,Deo Filikunjombe, alipotakiwa kuelezea malalamiko ya mashirika hayo, alisema kamati yao bado haijayapokea.
Alisema wanatarajia kukutana namashirika yote ya umma mwezi ujao na kwamba wana imani kama kuna malalamiko jambo hilo litatokea .
Hata hivyo, alisema kwa muda mrefu baadhi ya mashirika yamekuwa hayaichangii chochote Serikali, badala yake hata kama yakipata faida wanachofanya ni kuongeza mishahara na malupulupu ya wafanyakazi na bodi.
Naibu Waziri
Akizungumza na Mwananchi Jumamosi, Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, alisema kuwa waraka huo unatokana na maazimio yaliyopitishwa na Bunge kuwa mapato yote ghafi ya mashirika ya umma yachangie Serikali.
Tumerekebisha sheria bungeni na mashirika yote yanatakiwa kufanya hivyo kwani hakuna kipya, alisema Saada.
Kuhusu kuchelewa kupelekwa kwa fedha katika halmashauri mbalimbali na malimbikizo ya posho kwa watumishi wa Serikali alisema kuwa Serikali ipo katika mchakato na utakapokamilika fedha zitatumwa.
Tumetoka bungeni kama wiki tatu hivi, hivyo tuko katika maandalizi ya kukusanya fedha za mapato, kisha tutapeleka, alisema Saada.

Chanzo: MCL
 
Ni wiki chache zilizopita kikao cha Bunge cha bajeti ya 2013/2014 kuanzia July 2013 mpaka June 2014 ndio kimemalizika. Sasa hata mwezi wa kwanza wa mwaka wa fedha wa Serikali haujaisha tayari Serikali imekwishafilisika!!!!

Nchi ina utajiri mkubwa lakini bajeti ya Serikali ya mwaka mzima haimalizi hata mwezi kabla haijafilisika!!! Kweli hii Serikali ni Serikali ya kisanii.
 
TANESCO kifedha iko hoi bin taabani. Inaendeshwa kwa hasara kubwa kwa miaka mingi sana. Bado wanatakiwa kuwalipa mafisadi wa Richmond/Dowans bilioni 111 na bado wanabebeshwa mzigo mwingine wa kutoa 10% ya mapato yao kwa Serikali ya kifisadi!!!!
 
Huwezi kuunda vyeo vya Naibu mawaziri, wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wasaidizi wa Idara, Naibu makatibu wakuu lukuki kwa muda mfupi wa chini ya miaka mitatu halafu Serikali yako ikawa salama kifedha. Kuna watu walipiga kelele sana juu ya teuzi lukuki za wakurugenzi wasaidizi, na wakuu wa wilaya bila kuangalia mfumo wa mapato lakini wakaziba masikio.
 
Serikali ina Fedha nyingi tuu. Kwa sababu wanauwezo wa Kubandua Barabara za Dar es salaam na Kuzijenga upya tena kwa kiwango cha kimataifa. Angalia Morogoro Rd, Mwai Kibaki Rd Old and New(aka Bagamoyo Road). Mikoani ndio usipime nasikia kila kijiji kinaunganishwa kwa Lami au Reli na Viwanja vya Ndege kila Mji. Miradi yote hii si Pesa ya Serikali?
 
Pia kuongeza gharama za Serikali kwa kuongeza idadi ya mikoa kila kukicha. Katiba mpya nayo inaweza kuongeza gharama hizo kwa kiwango cha juu. Kwa kuwa imependekezwa kufutwa kwa viti maalum vya kuteuliwa na Rais bungeni, tume ya katiba inapendekeza kila jimbo liwe na Wabunge wawili wa kike na wa kiume. Hii itaongeza kwa kiasi kikubwa gharama za uchaguzi, mishahara na marupurupu watakayolipwa Wabunge.

Huwezi kuunda vyeo vya Naibu mawaziri, wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wasaidizi wa Idara, Naibu makatibu wakuu lukuki kwa muda mfupi wa chini ya miaka mitatu halafu Serikali yako ikawa salama kifedha. Kuna watu walipiga kelele sana juu ya teuzi lukuki za wakurugenzi wasaidizi, na wakuu wa wilaya bila kuangalia mfumo wa mapato lakini wakaziba masikio.
 
Pia kuongeza gharama za Serikali kwa kuongeza idadi ya mikoa kila kukicha. Katiba mpya nayo inaweza kuongeza gharama hizo kwa kiwango cha juu. Kwa kuwa imependekezwa kufutwa kwa viti maalum vya kuteuliwa na Rais bungeni, tume ya katiba inapendekeza kila jimbo liwe na Wabunge wawili wa kike na wa kiume. Hii itaongeza kwa kiasi kikubwa gharama za uchaguzi, mishahara na marupurupu watakayolipwa Wabunge.
(Bila kuathiri maudhui ya mada) Kwani ni kila jimbo (kama yalivyo sasa) au kila mkoa?
 
Mkuu unaulizia kuhusu capital letter ya Jimbo? Kama swali lako linalenga huko basi jibu ni Jimbo na si jimbo.

(Bila kuathiri maudhui ya mada) Kwani ni kila jimbo au kila Jimbo?
 
Na hii ndio shida ya mbunge wako pia. Tunaongelea baba mwenye nyumba kusema kafulia lakini anamiliki ng'ombe wa familia na kuku na ndo anapeleka sokoni mazao. Tunahitaji pocket money, madawa, maji, barabara na hata elimu. Wewe unaangalia spelling mistakes na typo errors ukimaliza unasinzia!
(Bila kuathiri maudhui ya mada) Kwani ni kila jimbo au kila Jimbo?
 
Hiyo sheria ipo toka zamani ingawa ilikuwa haitekelezwi. Tofauti ni kwamba hapo awali kila shirika lilipaswa kuchangia 10% ya FAIDA yake kwa mwaka, ikaonekana mashirika mengi yana declare faida kidogo kwa kutumia mbinu za kihasibu (creative accounting or earnings management), ndo maana sasa wameamua kuicharge kwenye MAPATO GHAFI. Angalia repoti za CAG miaka iliyopita. Mashirika kamaTANAPA, EWURA, TCRA n.k yanapata hela nyingi sana, matokeo yake wanaishia kujipangia posho kubwa za vikao vya board na perdiems na safari za nje kibao. Wakati rate za posho za kujikimu za juu serikalini ni 80,000, yapo mashirika wajumbe wake wa board wanalipwa hadi 450,000 per day na bado analipiwa tiketi ya ndege, malazi, chakula na vinywaji. Posho za vikao zinafikia hadi 1,000,000 per sitting. Naunga mkono uamuzi wa serikali
 
Na hii ndio shida ya mbunge wako pia. Tunaongelea baba mwenye nyumba kusema kafulia lakini anamiliki ng'ombe wa familia na kuku na ndo anapeleka sokoni mazao. Tunahitaji pocket money, madawa, maji, barabara na hata elimu. Wewe unaangalia spelling mistakes na typo errors ukimaliza unasinzia!
Hapana King'asti sikuwa na lengo la kuangalia mistakes ila nilikusudia kuandika kila Jimbo (kama yalivyo sasa) au kila Mkoa juu ya wabunge wawili? wacha ni-edit kwenye post yangu
 
Mkuu unaulizia kuhusu capital letter ya Jimbo? Kama swali lako linalenga huko basi jibu ni Jimbo na si jimbo.

Na hii ndio shida ya mbunge wako pia. Tunaongelea baba mwenye nyumba kusema kafulia lakini anamiliki ng'ombe wa familia na kuku na ndo anapeleka sokoni mazao. Tunahitaji pocket money, madawa, maji, barabara na hata elimu. Wewe unaangalia spelling mistakes na typo errors ukimaliza unasinzia!

My god, lo nilikuwa namaanisha kila Jimbo au kila Mkoa uwe na wabunge wa2, si suala la Capaital letter hata kidgo, ni typing error-sorry

Hapana King'asti sikuwa na lengo la kuangalia mistakes ila nilikusudia kuandika kila Jimbo (kama yalivyo sasa) au kila Mkoa juu ya wabunge wawili? wacha ni-edit kwenye post yangu

kaka asubui hii kuna shughuli nyingi tu za kufanya,sio lazima uchangie
Sikuwa namaanisha mistakes za capital letter au typing, bali mapendekezo mapya ya Katiba ni wawili kwa kila Jimbo la Uchaguzi litakalokuwa na ukubwa wa mkoa hivyo kufanya zaidi ya 50 kwa Tanganyika na 10 kwa Zanzibar. Mantiki ya kuuliza hivi ni kwamba, idadi ya wabunge wa Bungge la Muungano itapungua na gharama kupungua pia (ila kigezo cha Gender ndio bado mtihani). Nikasema bila kuathiri maudhui ya mada hii nikimaanisha kwamba mada haihusiani na rasimu ya Katiba hivyo swali langu huenda lilikuwa linatoka nje ya mada. Kwa niliowakwaza, nawaomba msamaha.
 
Kwa mapendekezo ya Tume ya katiba mpya wao wanaona kwamba kufuta viti maalum kutasababisha bunge kuwa na Wabunge wanawake wachache sana, hivyo ili kuhakikisha hali hiyo haitokei ndio wamekuja na hilo pendekezo kila jimbo liwe na Wabunge wawili mmoja mwanaume na mwingine mwanamke kwa maana hiyo kuongeza idadi ya Wabunge karibu maradufu ya hawa waliokuwepo katika bunge la sasa, sidhani kama kila mkoa uwe na Wabunge wawili. Ila kama nimekosea ni kila mkoa uwe na Wabunge wawili badala ya kila jimbo basi nitasahihishwa.

My god, lo nilikuwa namaanisha kila Jimbo au kila Mkoa uwe na wabunge wa2, si suala la Capaital letter hata kidgo, ni typing error-sorry
 
Back
Top Bottom