Dar Es Salaam: Mhitimu wa kidato cha nne aliyefichwa vifo vya wazazi na ndugu zake apewa taarifa baada ya siku 22

Daah imenisikitisha sana nahis kwanza mpk sasa akir sio yake kbs anahitaj msaada wa kiiman zaid na hapaswi kukaa peke ake muda mrefu anawaza sana na hapat majibu ila mungu ni mkubwa atampa moyo wa uvumilivu
 
Chochote kinachotokea kwetu tunaamin ni mipango ya Mungu maana yy ndio anajua hatima yetu

Pia kuhusu hilo tunaamin kila mtu ameletwa duniani kwa kusudi flani na anapoondoka bas tunasema siku zake zimetimia means amekamilisha kusudi aliloitiwa hapa duniani...

Na Mungu tunamuomba sababu tunaamini katika yeye na ndio muweza wa yote so lazima tumuombe kwenye kila jambo haijalishi ni nn....

Nadhan nmekujibu swali lako mkuu

Kwahiyo kibaka anayechomwa moto ni Mungu alipanga azaliwe aje kuwa kibaka afe kwa kuchomwa moto?
 
Ina maana alikosekana mmbeya mmoja wa kumwambia shule? jamani jamani kabisaa au mnatudanganya humu?
Kipindi tupo kwenye mitihani ya mwisho Necta. Tulikua tunasoma na mtoto wa kigogo wa mkoa fulani sasa kuna siku tunasikiliza radio tukasikia wanatangaza amekufa na tuli confirm kwa sababu huwa anamzungumzia mara chache baba yake lakini tulikausha mchizi akafanya mpaka alipoenda kuambiwa nyumbani kwao.

Mungu amfanyie wepesi binti hili jambo lipite salama.
 
Umri wake mdogo mali za wazazi wake mafisi watajinyakulia yote....


Mi namlaumu Baba yake kulazimisha kuvuka mto wakati daraja maji yanapita juuu..


Sipati picha watoto wakilia Baba/ Mama tunakufa. Baba naye hawezi wasaidia. Mikanda imewabana.... kifo cha maji kibaya.

Mimi nikiona maji sivuki maana niliwahi bebwa na maji nisingeruka sijui kingetokea nini
 
Mwenyezi Mungu ampe nguvu katika kipindi iki kigumu ambacho anapitia, mana ni kpnd ambch hkn binadamu ambaye angependa kukipitia.

Lkn ndo ivyo ,kila nafsi itaonja umauti...mbele yao nyuma yetu.

Raha ya milele uwape e Bwana, na mwanga wa milele uwaangazie..marehemu wote wapumzike kwa amani.
 
Hatimaye Anna Zambi (16), binti aliyefiwa na wazazi wake wawili na ndugu zake watatu waliopata ajali wakati wakienda kwenye mahafali yake mkoani Kilimanjaro Oktoba 26, 2019 leo Jumamosi Novemba 16, 2019 amefahamishwa kuhusu vifo hivyo.

Amewasili nyumbani kwao Goba Dar es Salaam saa 10.30 alfajiri akitokea shule ya Sekondari ya Mather Theresia of Calcuta baada ya kumaliza mtihani wa Taifa wa kidato cha nne ulioanza Novemba 4, 2019.

Wazazi wake, Lingston Zambi na Winifrida Lyimo na wadogo zake watatu, Lulu, Andrew na Grace walikufa katika ajali hiyo baada ya gari walilokuwa wakisafiria kusombwa na maji kutokana na mvua kubwa iliyonyesha wilayani Handeni mkoani Tanga.

Baada ya vifo hivyo, Anna ambaye hakuelezwa chochote na hata alipomaliza mitihani yake pia hakuambiwa mpaka leo alipofika nyumbani na kupewa habari hizo.

Ndugu zake walipata wakati mgumu kuhusu jinsi ya kuanza kumpa taarifa hiyo ya huzuni.

"Alipofika watu wanne walikwenda kumweleza. Kwa kweli alilia sana. Alipoingia ndani alijilaza miguuni mwa bibi yake na kuendelea kulia.”

"Aliongea mengi huku akilia akasema alihisi jambo hilo na kuna wakati alikuwa anaamka usiku na alisema mitihani yake amefanya kwa taabu sana," amesema Ibrahim Zambi ambaye ni baba yake mdogo.

Ibrahim amesema Anna alikuwa akilia na kuzungumza maneno ya simanzi, “mwenyewe alisema ‘kwanini mliniacha, hamkuja kunichukua tuondoke wote’.”
Ameongeza, “tunashukuru Mungu tulihofia sana angepata shida kubwa ila amepokea vizuri anaomboleza tu.”

Dk Doya Frederick aliyepo nyumbani kwa kina Anna, ameshauri mtoto huyo apumzike na baadaye asaidiwe kiimani na kisaikolojia.

"Mtu anapopata taarifa za jambo gumu anapitia hatua kadhaa ili akae sawa ndipo asaidiwe kisaikolojia lakini pia ajengwe kiimani. Hatua hizo ni kukataa, hasira, kubishia kwamba haiwezekani lakini baadaye kukubali uhalisia," amesema Dk Doya.

Tangu alipofika nyumbani kwao hadi saa 4 asubuhi leo alikuwa amepumzika kabla ya kushiriki ibada maalumu.

Baada ya ibada atapelekwa katika makaburi walikozikwa wazazi na ndugu zake kwa ajili ya kuweka mataji ya maua.

View attachment 1264370

Chanzo: Mwananchi
Nimejikuta nikilia
 
Back
Top Bottom