kama bado kuna utata wa kuhesabu sasa wafanyaje au kama watu wanagomea na kulilia recount? Huu mfumo wengine tuliipigia kelele muda mrefu lakini kama watu hawajifunzi kabisa... This will change.
Tatizo unafikiri una akili sana kuliko Watanzania wengine. Kila kitu ni wewe tu ulishawahi na kukipigia kelele. Ungetoa solutions basi!!
Zungu (CCM) kidedea jimbo la Ilala kwa zaidi ya kura 35,000.
Tume wanafanya yao. Ninaomba sana UKAWA, jumulisheni matokeo kwa kutumia nakala za mawakala katika ngazi zote. Tume hii inachakachua mpaka basi na haitakiwi kuiamini bila kuthibitisha. Kama kuna sehemu mawakala hawajawapa nakala za nakala zao tafadhali fanyeni vile haraka iwezekanavyo or else tume hii siyo.
Ninasema haya kwa uchungu baada ya kusikiliza ITV alivyofanyiwa Wenje wa Nyamagana. Kwamba hadi wanafunga mahesabu, kwenye form za tume ambazo mawakala wote walikuwa nazo, Wenje alikuwa akiongoza kwa kura zisizopungua 4,000 Elfu nne mbele ya yule wa Ccm. Wakati wanasubiri atangazwe, kule kwa mkurugenzi kwa ubabe wakamtangaza wa Ccm eti kashinda.
Ninasikitika sana ninapoandika haya. Wenje akagoma kusaini na kutoa rai ya kuhesabu kura moja baada ya nyingine. La kuhuzunisha zaidi eti tangu asubuhi wanarudia kuhesabu kura hadi sasa hawajamaliza na hakuna kinachoeleweka.
Kweli hii ni tume ya kuamini wanahcokisema? Si kura za Madiwani, Si kura za Wabunge na zaidi sana Si kura za Raisi zinazotangazwa na tume zinatakiwa kuaminiwa hta kidogo bila kuthibitishwa.
UKIZINGATIA NA KITENDO CHA JANA CHA KUVAMIA TALLYING CENTER YENU ILI MSIJUE UHALISIA WA KILE KINATNGAZWA. NAOMBA SANA HILI MLICHUKULIE HATUA ZA HARAKA KABLA HAMJACHELEWA.
Hadi muda huu,hakuna hata jimbo moja jijini Dar es Salaam lililotangaza matokeo ya Ubunge. Yote bado kuna ukimya.
Si Ukonga,Segerea,Kinondoni,Ilala,Temeke,Mbagala,Kigamboni,Kawe,Ubungo wala Kibamba kulikotangazwa. KWANINI hayatangazwi?
Mnayakumbuka wakati Mrema anagombea Urais kupitia NCCR?
Ni aibu kubwa mno kwa vyombo vya dola na tume kukaa kimya bila kuchukua hatua ya aina yoyote wakati kuna wana CCM wanakamatwa na raia wakiwa na maboxi ya kura feki kila mahala.
Ukiona matokeo ya jimbo lolote linachukua muda zaidi kutanganzwa ujue Tume inakokotoa nambari ili chama cha mwenyekiti kisipate pigo la nguvu.Hadi muda huu,hakuna hata jimbo moja jijini Dar es Salaam lililotangaza matokeo ya Ubunge. Yote bado kuna ukimya.
Si Ukonga,Segerea,Kinondoni,Ilala,Temeke,Mbagala,Kigamboni,Kawe,Ubungo wala Kibamba kulikotangazwa. KWANINI hayatangazwi?