Jamani nisaidieni, nina ugomvi mkubwa na Tanesco. Kwanza tulikuwa tunalipa ankara za umeme kwao kila mwezi iweje leo wawe wanadaiwa na Dowans, ina maana pesa yote walikuwa wanachikichia? pili hii biashara ya umeme kwanini isiwe ya ushindani kama ilivyo kwenye secta ya mawasiliano ya simu za mkononi? Ona siku hizi tunapeta katika simu ingawa Tanesco hao hao wanajaribu kuwaangusha kwa kukosa umeme.