Pamoja na Dar es Salaam kuwa na upepo mwanana na mandhari nzuri kutokana na uwepo wa Bahari, Fukwe za Jiji la Dar es Salaam limejaa uchafu wa plastic bags , bottles , na kila aina ya uchafu. Tunaomba mamlaka husika zijipange vizuri kufuatilia usafi wa fukwe mara kwa mara, labda kwa kushirikisha wamiliki wa hoteli zinazozunguka maeneo yenye fukwe, kampuni za usafi za binafsi na wananchi ili kurejesha mandhari nzuri yenye uhalisia wa fukwe zenye hali ya usafi zitakazovutia . Uchafu huu sio tu ni hatari kwa nchi inayotegemea sana mapato kwenye utalii , bali pia ni hatari kwa uhai na ustawi wa viumbe wa majini na madhara mengine ya kiafya kwa watumiaji na hasa watoto.
Hili linakera sana na wengi waliotembelea baadhi ya fukwe zetu mtakubaliana kuwa hali si nzuri hata kidogo (angalia picha).Jambo hili linahitaji ufuatilia wa karibu Wizara ya Muungano na Mazingira na Utawala wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Usafi wa fukwe na maeneo mengine unategemea sana upigaji marufuku chupa na mifuko ya plastiki. Hili jambo limeshaongelewa mara kadhaa , Zanzibar , Kenya na Rwanza wameweza bila plastiki , tuchukue hatua tuache kigugumizi.
Nawasilisha kero yangu kwa wahusika