DAR: Askari Polisi wanne wauawa na raia 2 wajeruhiwa, silaha zaporwa!

Yaani ......hebu niishie hapa nisijeonekana sina ubinadamu bure.

Shame to you; yaani unafurahia watanzania kuuawa? hapo tu bila kuchangia zaidi imeonekana msimamo wako wa jambo hili. siasa zititufikishe huku jamani, tusishangilie majambazi kuua majambazi, vyama vya siasa muwe makini, majambazi wanaweza kuaharibu jambo zuri la kutafuta haki. hivyi muwe makini na kauli zenu ktk matokeo km haya.
 
Huu ni mtizamo potofu sana. Una chembe nyingi sana za hisia negative za kisiasa.
Unajenga dhana kuwa polisi wameuawa kwa sababu wanachukiwa na jamii kitu ambacho sio sahihu kwa jamii yetu. Huwezi jenga hoja hii pasipo kuwepo ushahidi wa kisasi binafsi dhidi ya askari waliouawa.
Umenielewa vibaya si kosa lako.
 
This is too much...!!! Hivi ni nani amewafundisha chuki kiasi hiki..?
Huyo aliyesewa 'wapige tu', huyo analiyesema 'wamejilipua ktk mkutano- Arusha', huyo aliyesema "tutashinda hata kwa gori la mkono', huyo analiyezuia mchakato katiba mpya-,,,huyo anayefikili amani inalindwa na mtutu kwa kukandamiza haki, huyo aliyemua Mwangosi akapandiswa cheo.....wewe usiyependa demo ichukue mkondo wake.

Jibu hili halina usiano na tukio la vifo vya askari wetu waliokuwa ktk majukumu yao ya kulinda raia na mali zao (benk.) ila litakuwa zuri na kubwa zaidi kwao hao watakaothubutu kuzuia na kuua badala ya kulinda waandamanaji na mikutano halali iliyo na vibali
 
Suala la kuuawa binadamu si la kufurahia hata kidogo. Sio kuuawa kwa Polisi wenye silaha tu, bali hata Polisi haipaswi kuuwa raia wasio na silaha wala hatia. Utawala uliopo sasa umezidisha vitisho kwa raia kwa kutumia Polisi, hata pale ambapo hoja nzuri zingetosha kutuliza watu. Vitisho hivi vilivyopitiliza ndio vimejenga chuki hii uionayo. Nchi zilizochafuka hali ilianza hivihivi, ubabe wa dola dhidi ya raia wake, hapo hata wahalifu wa kawaida huona ni fursa na kuitumia. Shambulio hili la kusikitisha, kila nikilitafakari napata taabu kulielewa, hao majambazi walikuwa wakitaka nini hasa kwa hao vijana wetu waliowaua? Kama ni bank, ilikuwa imefungwa, kama ni bunduki moja walioichukua, haiingii akilini kuwa wauwe askari wetu wanne kisha wachukue bunduki moja tu. Nionavyo haya ni mauaji ya chuki tu (hate murder) dhidi ya jeshi letu la Polisi, na kwa wanaofurahia mauaji haya, wajue kuwa waliofanya hivyo sio raia wa kawaida bali ni majambazi hatari ambao iko siku watakuja kuwashambulia na kuwaua hao wanaofurahia na kisha watalilia msaada wa Polisi, kisha ni Polisi ndio wataweka rehani roho zao kuwalinda raia dhidi ya majambazi hao. Chuki zangu haziko kwa Polisi wetu, wao hupokea amri tu kutoka kwa wakubwa zao, bali chuki zangu ziko kwa viongozi wa kisiasa wanaolitumia vibaya jeshi hili dhidi ya raia kwa malengo ya kisiasa.
 
Inteligensia ya kawaida tu inaniambia kama waliovamia hawakuchukua hela kuna kazi kubwa na ya akili sana polisi wanatakiwa kufanya.
 
Nadhani jeshi la polisi linahitaji mazoezi pia ya kutumia vifaa vyao.

Hii ni Sawa kweli? Uzio wa polisi nadhani unatakiwa kuwa umezuia eno tosha na sio kama picha hizi zinavyoosha.
 

Attachments

  • mbeleee.jpg
    mbeleee.jpg
    56.8 KB · Views: 32
  • DSCN2236_thumb%255B1%255D.jpg
    DSCN2236_thumb%255B1%255D.jpg
    43.1 KB · Views: 36
  • motorcycle3img_4166.jpg
    motorcycle3img_4166.jpg
    64 KB · Views: 30
Polisi hawashauriki, Hats ukiwapa ushauri hawakubali, Hata mafunzo yao wengine hawayatekelezi. MF, ukiwa na silaha muda wote iwe tayari kulenga, Usiruhusu MTU akusogelee, Leo ukienda benki MF NMB pale Posta unawakuta wamekaa kwenye viti na silaha wameishika wakiwa wameisimamisha chini!Sasa wanaokuja hapo sio wote ni Wateja, Kifupi wanatakiwa wasiamini MTU yeyote hata awe mlemavu, Tatizo lingine MASAA YA KUPOKEZANA LINDO LIANGALIWE, HUWEZI UKAWA UMESOMAMA MASAA MANANE NA BUNDUKI YAKO LAZIMA UTACHOKA, NI VIZURI WAKAWA WANAWATOA KILA BAADA YA MASAA MANNE, Halafu Serikali iajiri Askari wengi tena vigezo na mashariti vizingatiwe, Askari wasio waadilifu watolewe haraka wanawaumiza wenzao. Namba za makamanda waPolisi na za waziri mwenye dhamana ziwekwe hadharani ili Askari wasiofuata maadili yao RAIA watoe taarifa kupitia hizo namba za simu ili wakubwa wamfanyie uchunguzi Hugo askari na kumuwajibisha. Ajira za kujuana zikomeshwe. Kunawengine walipata ajira kwa SABABU Shemeji yake alikuwa na cheo Fulani akapigiwa pande aende Upolisi hapo yeye hakuwa tayari , Sasa MTU kama huyu kamwe usitegemee kuyaishi maadili ya Upolisi. Polisi ishirikiane na RAIA, RAIA ndiyo wanaoishi na hayo majambazi, Ulinzi shirikishi ulikuwa mzuri sana ila ulipaswa ufanyiwe marekebisho madogo tu. Polisi ni wachache sana, hivyo hawana budi kushirikiana na RAIA, Lingine Viongozi wa Serikali na wanasiasa wasilitumie jeshi LA Polisi kwa maslahi yao, Waliache litende haki kwa RAIA wote na kwa vyama vyote vya siasa. Kulitumia vibaya ni kuwagombanisha Polisi na RAIA kwahiyo KILA RAIA kuwa na chuki nalo, Poleni wafiwa wote, Mungu aziweke mahala panapostahili Roho za hawo marehemu wote, Kwa nitakayemkwaza naomba anisamehe, Mimi najaribu kutoa ushauri Wangu tu, Ila kama Kuna MTU mwingine anaushauri mzuri so vibaya akautoa. Lengo tukomeshe uhalifu huu.
 
Ni mbaya sana wanasiasa kuwachonganisha polisi na raia, hali hii inaweza kuwa mbaya sana baada ya septemba, mosi. Najua ninyi wanasiasa akiwemo Rais na watoto wenu mtakuwa mmetulia majumbani kwenu lakini polisi na familia zao wataishi kwa hati hati majumbani kwao.

Yetu macho lakini ipo siku Mungu atanena tu.
 
Kova angekwepo ungeskia leo wahalifu wote wamedakwa wakitubu dhambi zao kanisani tukawadaka wote!
 
Kuna Uzi humu ndani, ulitabiri haya ya askari kuvamiwa na kuporwa silaha na raia, yametimia sasa!
Jeshi la polisi linapoamua Kuwa adui ya wananchi madhara Yake ni makubwa Kwa jeshi Hilo zaidi kuliko Kwa hao ukuta. Tukumbuke tu Kwamba CCM ilishindwa Na rais Huyu Ndio rais wa CCM aliyepata Kura chache kuliko rais mwingine yoyote. Katika Hali ya kawaida tungetegemea Kiongozi wao atutie Muda wake mwingi katika kujenga mahusiano Na hasa Kati ya raia Na wananchi. Badala Yake yeye yuko busy kuwajengea ukuta. Bahati Mbaya hata hao viongozi wa polisi ni uchwala badala ya kumsaidia mkulu Kwa kumshauri opasavyo, wao wana piga vigelegele huku vijana wao wakiachiliwa ku swim in the high sees pasipo protection. Nasikia hata baada ya hayo. Mauaji very few people around the area wewe interested to know what has happened. Ule Upendo wa watanzania unaoonekana kwenye ajali Za kawaida, sasa haupo inapowahusu polisi. Hivi inakuaje tu nakubali kuzika polisi shirikishi, tuliyoijenga for years, for a single statement jamani
 
Du Wa4 wanauawa kwa mpigo!,kweli majambazi noma.Raia wema ambao wanamiliki sirah kwa mashart amani hatuna kabisa
 
Ila tuseme tu ukweli, hawa jamaa wakiwa wanawapiga Chadema au wanafunzi wa vyuo wanaoshea kinoma! Wengine wanaruka mpaka judo na samasolt kama Bruce Lee ila wakija wazee wa kazi hadi huruma.. Tatizo wamejivika kuwa tawi la CCM wakaisahau kazi yao.... RIP wahanga

Hakuna namna.....!
Ukatili wa polisi kwa wafuasi wa CHADEMA unatokana na kufukuzia kupandishwa vyeo, au kuteliwa kwenye vyeo vya kisiasa U-DC, na U-RC.
 
Poleni wafiwa,matukio ya mauwaji ya askari na kupora silaha yamerudi tena.Mungu atusaidie !!!!!
 
Siyo kweli wana siasa wanachonganishwa na raia...polisi wenyewe wanavyo wa treat raia ndiyo raia wanavyo lípizia polisi ndomana hakuna ukaribu,lazima polisi wabadilike
Ni mbaya sana wanasiasa kuwachonganisha polisi na raia, hali hii inaweza kuwa mbaya sana baada ya septemba, mosi. Najua ninyi wanasiasa akiwemo Rais na watoto wenu mtakuwa mmetulia majumbani kwenu lakini polisi na familia zao wataishi kwa hati hati majumbani kwao.

Yetu macho lakini ipo siku Mungu atanena tu.
 
Back
Top Bottom