Dangote yaanza kusambaza cement Tanzania

Dangote yaanza kusambaza cement Tanzania

Aliyesema cement itauzwa 5000tzs anapaswa kushtakiwa kwa uwongo huo, sema bongo hatujali sana haki zetu au tunaogopa kuzidai. Haiwezekani uambiwe mfuko mmoja wa saruji utauzwa kwa 5,000 tzs halafu uuziwe 13,500 tzs, ni udanganyifu mkubwa na kuwadharau watanzania ambao ndio wateja wa bidhaa hiyo. Ni afadhari kama kuna jambo ilibidi aliyetoa tamko hilo aombe radhi wananchi kwa kuwaambia bei ya awali haiwezekani na kwamba mahesabu yalipigwa vibaya..
 
Tulitegemea hiki kiwanda cha Dangote cement iwe nafuu kuliko cement nyingine ila sioni tofauti yotote hiyo bei ya 13500 ndio bei tunayonunulia cement nyingine kwa sasa hapa dar.
Kulikuwa na tetesi mwanzo kuwa alitaka auze rahisi ila akaambiwa ataua viwanda vingine vya cement mwenye taarifa sahihi atujulishe vizuri.
 
HIVI Kumbe Ndio KIWANDA Kimeanza KUZALISHA Cement JANA!!!!?? SI Tulikuwa Tunaambiwa Products Zao Ziko Sokoni Tayari Na Bei Ya Mfuko 1@ sh. 6.000/: Kwa Mikoa Ya Kusini!!!!!?? YAKISEMWA Na MAGUFULI Wkt Ule Wa KAMPENI, Hasa Kule KANDA Ya ZIWA, Ambako Alikuwa Akiwaeleza Wananchi Wajiandae Kujenga Majumba Ya Kisasa Ya Tofali, Maana Cement Itakuwa Zikiuzwa Kwa Bei Nafuu Mno, Kutokana Na UZALISHAJI Wa KIWANDA Hicho Cha DANGOTE!!! SASA Taarifa Yako Inapingana Na Mh. MAGUFULI Kabisa, JE, Ni Nani Ambaye Amesema UONGO Ktk Hilo!!!??
 
5000 limekuwa tikiti maji hilo....
Sasa si bora tikiti maji, hata likiuzwa elfu kumi sawa tu kwa sababu linakaa shamba kwa muda mrefu na kuhitaji huduma nyingine nyingi ikiwemo muda wa kukuwa hadi kufikia hatua ya kuingizwa sokoni ila sio saruji ambayo process yake ni ya faster tu, au unataka kusema aliyesema saruji itauzwa elfu tano alidanganya huku akijua haiwezekani?
 
Enewei.. Tuliomba ajira january kwa Dangote,sijui mchakato uliishaje mwenye taarifa ya usaili ningependa kufahamu kama mchujo tayari ama unasikiliziwa bado
 
Ndugu yangu isue ni ivi kiwanda kinauza cement kwa sh 8000 + 3500 ya VAT =11,500
Kwa hiyo mpaka ikufikie wewe ni 13,500
Kwa hiyo tatizo ni hapa kazi tu
Hiyo VAT ni % ngapi?,au kuna other hiden charges!
 
Naamin itapungua, maana miongon mwa ahadi za rais ni kuishusha, ila pia si rahis kwa sasa, naamin baada ya july vitu vingi vitashuka sana,

Ikumbukwe hawezi kuanza chin ya hapo kutokana na soko huria, mnakumbuka kile king,amzi cha azam kinaanza tukaambiwa itakuwa rahis mwisho soko likawalazim kuwa sawa na wengine,

Kwa hyo itawezekana mabadiliko si ya haraka kama kuzungusha mikono, ni process, hatua kwa hatua ngazi kwa ngazi, tutafika tu..
 
1. Dangote tuli imbishwa nyimbo kwamba bei yake itakuwa mkombozi kwa Watanzania, ukombozi ni wa kutuuzia mfuko moja kwa Tsh 13,500??? Kuna tofauti yoyote na wazalishaji wengine? Kama kweli hiyo ndiyo bei ya cement yenu iwe ni reja reja mtaani, au jumla kiwandani, vyovyote iwavyo mtakuwa mmenza biashara kama HALOTEL!
2. Mleta mada na wenzake baada kadai saruji ya Dangote mfuko mmoja ni tsh 13,500. Baada ya kuwa challenged na wafukunuzi amesema bei ni 8,000 +3,500 VAT kwa hiyo total inakuwa 11,500. Tofauti ya 2,000 sijui ina kazi gani, transport?? Kiwandani?? Hata hivyo 3,500/8,00 = 43.75% VAT = 18% why 43%+???
3. Wanasiasa, TPDC, Wizara ya Nishati na madini, etc mtueleze unafuu na umuhimu wa kiwanda dangote mliyo tuambia uko wapi???? Ardhi alinunua kwa watu binafsi au serikali ilimuuzia au kumgawia?
4. Mali gafi anatoa nje au anachota katika shamba la babu maana la shamba la bibi limeoza???

Nilishawahi kupendekeza hapa kwamba tunahitaji kampuni ama organisation ya kuratibu matukio makubwa ya kitaifa na kuyafuatilia kwa ajili ya kuona utekelezaji wake au maboresho ya kuzuia yasitokee tena. Nilipendekeza wataalam wanao takiwa ni wanasheria, waandishi wa habari za kiuchunguzi ama mwanadishi yeyote menye taaluma hiyo, wachumi (fedha na biashara), taaluma ya utawala, mwenye taaluma na mjuzi wa mambo ya ulinzi / investigation! Ni bahati mbaya hakuna aliyo onyesha interest / kujali, tungekuwa tunarecord matukio yote na kwa mfano katika hili tunge wafuata walio toa ahadi au tambwe kipindi kile waje waseme kulikoni! Nirudie tena kusema hatujachelewa, jambo hili ni nyeti ukiachilia mbali kukomesha wanao penda kuhamisha mijadala ya kitaifa kwa kuanzisha mijadala mipya kwa malengo yao, watu wangetengeneza ajira na maendeleo ya kibiashara. Mwenye interest anipm.​
 
Sasa mpk ifike Mwanza itauzwa sh.ngapi?
Ndio Hapo Sasa Mkuu!! SIJUI MAGUFULI Wkt Ule AKIPIGA KAMPENI, Kuwa Bei Ya Cement Itakuwa Elfu 6 Tu Kwa Mfuko, Baada Ya KIWANDA Hicho Kuanza KUUZA Cement Yake Kwa Bei Hiyo Kule Mkoa Ya Kusini!!! KUMBE Sio KWELI, UZALISHAJI Wenyewe Ndio Umekamilika Hiyo Jana Na Bei Ndio Hiyo!!!! SASA Sijui MAGUFULI Alizipata Wapi Hizo Taarifa Alizokuwa ANAZOTOA MAJUKWAANI!!!!
 
HIVI Kumbe Ndio KIWANDA Kimeanza KUZALISHA Cement JANA!!!!?? SI Tulikuwa Tunaambiwa Products Zao Ziko Sokoni Tayari Na Bei Ya Mfuko 1@ sh. 6.000/: Kwa Mikoa Ya Kusini!!!!!?? YAKISEMWA Na MAGUFULI Wkt Ule Wa KAMPENI, Hasa Kule KANDA Ya ZIWA, Ambako Alikuwa Akiwaeleza Wananchi Wajiandae Kujenga Majumba Ya Kisasa Ya Tofali, Maana Cement Itakuwa Zikiuzwa Kwa Bei Nafuu Mno, Kutokana Na UZALISHAJI Wa KIWANDA Hicho Cha DANGOTE!!! SASA Taarifa Yako Inapingana Na Mh. MAGUFULI Kabisa, JE, Ni Nani Ambaye Amesema UONGO Ktk Hilo!!!??
Mkuu umenikumbusha mbali sana!!!
 
Ndugu yangu isue ni ivi kiwanda kinauza cement kwa sh 8000 + 3500 ya VAT =11,500
Kwa hiyo mpaka ikufikie wewe ni 13,500
Kwa hiyo tatizo ni hapa kazi tu
8000 plus 18% VAT ni 9440 tu.
 
Kile kiwanda kikubwa cha Africa mashariki na Africa kwa ujumla kwa mara ya kwanza kimeanza kuzalisha kusambaza cement jana tar 21/02/ 2016.

Kiwanda hicho ambacho ni tegemeo jipya kwa waakazi wa mikoa kusini Mtwara na Lindi kiliahidi ajira nyingi ya wakaanzi wa mikoa hiyo na watanzania kwa ujumla
Cement tayari iko maduka kwa bei nafuu ya sh 13,500 tofauti na cement ya viwanda vingine.

Tunawakaribisha wateja wa cement hiyo na wenye magari makubwa kufungua office mkoani Mtwara ili kuongeza ajira za madereva hapa mkoani.
Magufuli alituahidi cement ya dangote itauzwa 8000/= je alitudanya???
 
Mimi nilikuwa nasubiri nijengee cement hiyo ya elfu nane naona imekula kwangu.
 
Back
Top Bottom