Dalili za ugonjwa wa H-PYLORI

Dalili za ugonjwa wa H-PYLORI

Naxria abdalla

Senior Member
Joined
Feb 28, 2025
Posts
158
Reaction score
281
Hamjambo natumai mupo wazima naomba kueleweshwa ni zipi dalili za ugonjwa au h-pylori, maana natamani kwenda kupima huu ugonjwa kutokana na homa za mara kwa mara zinazonikabili ila niliwahi kuskia watu wanaongea kwamba huu ugonjwa unatokana na matumbo

Namaanisha tumbo likiwa linauma ndio unapaswa kwenda kupima

Naomba munieleweshe kwa anaejua
 
Hamjambo natumai mupo wazima naomba kueleweshwa ni zipi dalili za ugonjwa au h-pylori,mana natamani kwenda kupima huu ugonjwa kutokana na homa za mara kwa mara zinazonikabili ila niliwahi kuskia watu wanaongea kwamba huu ugonjwa unatokana na matumbo namaanisha tumbo likiwa linauma ndio unapaswa kwenda kupima naomba munieleweshe kwa anaejua
Hakuna Ugonjwa wa H-PYLORI
 
H pylori ni mdudu bakteria anayeweza kuchangia ugonjwa wa madonda ya tumbo
Ingawa asilimia kubwa ya wagonjwa tunawakuta wakiwa hawana h pylori
 
Mgonjwa ukienda kuonwa na mtaalamu,eleza dalili za kinachokusibu inatosha,siyo ume-google vitu huko unatajataja terminologies hautasaidika.

Kujieleza ndiyo hatua muhimu kuelekea kupata tiba sahihi.
 
Mgonjwa ukienda kuonwa na mtaalamu,eleza dalili za kinachokusibu inatosha,siyo ume-google vitu huko unatajataja terminologies hautasaidika.

Kujieleza ndiyo hatua muhimu kuelekea kupata tiba sahihi.
ivi apo ndio umejiona umejibu kitu cha maana sana
 
ila watu bana, mtu kauliza swali na ww unamuuliza swali tena, maana yake hajui yeye anachotaka mtajie dalili Siyo kumuuliza tena
 
ila watu bana, mtu kauliza swali na ww unamuuliza swali tena, maana yake hajui yeye anachotaka mtajie dalili Siyo kumuuliza tena
Yeah naitaji dalili wamenieleze tu ila wao wananiambia mambo mengine
 
Bil
Yeah naitaji dalili wamenieleze tu ila wao wananiambia mambo mengine
Yeah naitaji dalili wamenieleze tu ila wao wananiambia mambo mengine

H. pylori (Helicobacter pylori) ni bakteria wanaoishi tumboni na husababisha maambukizi kwenye kuta za tumbo au utumbo mdogo. Watu wengi huweza kuwa nao bila dalili, lakini kwa wengine husababisha matatizo.

Dalili za maambukizi ya H. pylori:
1. Maumivu ya tumbo (hasa sehemu ya juu)
2. Kuhisi tumbo kujaa au kuvimbiwa mara kwa mara
3. Kuchoka kwa haraka baada ya kula chakula kidogo
4. Kichefuchefu au kutapika
5. Kupungua uzito bila sababu ya moja kwa moja
6. Kiungulia au gesi nyingi
7. Kinyesi chenye damu au cheusi sana (ikiashiria vidonda tumbo)
8. Hamaki au maumivu yanayopungua baada ya kula.

Matokeo ya muda mrefu:
  • Vidonda vya tumbo (peptic ulcers)
  • Saratani ya tumbo (kwa baadhi ya watu wachache)

Kama unahitaji kujua zaidi juu ya matibabu yake,hususani kwa njia ya tiba mbadala na mimea usisite kuuliza zaidi.
 
Hamjambo natumai mupo wazima naomba kueleweshwa ni zipi dalili za ugonjwa au h-pylori, maana natamani kwenda kupima huu ugonjwa kutokana na homa za mara kwa mara zinazonikabili ila niliwahi kuskia watu wanaongea kwamba huu ugonjwa unatokana na matumbo namaanisha tumbo likiwa linauma ndio unapaswa kwenda kupima naomba munieleweshe kwa anaejua
Acha kutumia sukari na vitu vyenye sukari, kula Milo michache kwasiku izo Hpylori zitapotea zote
 
Natumai mumeamka salama na mizunguko ya kutafuta riski inaendelea ila naomba kuja kwenu kupata majibu ya hili hivi bacteria wa h-pylori anapokupata kwenye mwili wako dalili zake ni wewe kuumwa tumbo au unaweza kumpata na tumbo lisiume?je ni dalili gani nyengine ambazo zinakuonesha umempata huyu bacteria?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom