Dalili za mapenzi kunyauka 1,2,3...15

eRRy

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2009
Messages
1,084
Likes
17
Points
135

eRRy

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2009
1,084 17 135
Tuendelee​
1261636322_dos1v.jpg

7 : Mkibeba fikra binafsi kwa kila mtu kutaka mafanikio yake.​
Maisha ya wapenzi wengi yamekuwa yakipoteza maana kiasi cha kufikia kuchuja kutokana na wapenzi wenyewe kuwa na mawazo ya ubinafsi. Utakuta watu wameoana lakini kila mmoja anakabili changamoto za maisha peke yake, hali ambayo humfanya atumie nguvu kubwa kutafuta ushindi wa matatizo yake.

Mantiki ya maisha ya ndoa ni kusaidiana. ‘Mungu alimwambia Adamu kuwa atampatia msaidia wa kufanana naye ambaye ni mwanamke aliyeitwa Hawa.’ Upo pia msemo usemao ‘Kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi’ Ni wajibu wa wanandoa kuhakikisha kuwa maisha yao yanakuwa ya nyuzi mbili ili yasikatike upesi. Lakini ikiwa kila mtu anajenga nyumba yake, anafanya biashara zake, ana mipango yake binafsi ujue mwisho mbaya wa mapenzi umesogea.
8 : Mkiwa watu wa kutoa siri zenu nje.​

Upo udanyanyifu mwingi wa kimawazo miongoni mwa wapenzi wengi kiasi cha kudhani kuwa kumwambia rafiki au ‘shoga’ masuala ya ndani ya ndoa ni kutafuta suluhu ya matatizo. Hii si sahihi kwa vile upo ushahidi mkubwa juu ya wapenzi wengi ambao walijikuta katika wakati mgumu baada ya kutoa siri zao nje. Ifahamike kuwa ndoa imara ni ile inayoheshimika katika jamii, na heshima hiyo haiwezi kuwepo kama wanandoa hawatakuwa makini katika kutunza siri za mapenzi yao.

Haipendezi kwa mwanamke/ mwanaume kwenda kijiweni na kuanza kuanika mambo ya ndani kwa mfano. ‘Yaani leo mume wangu hakuacha kitu chochote ndani sijui itakuwaje. ‘Sema wanawake wote lakini si mke wangu, ana kasoro nyingi sana.’
Kauli kama hizi na nyingine ambazo zinatoa nje udhaifu wa maisha yenu hazifai, kwani katika kila ndoa kuna udhaifu mwingi ukiwepo ukimya ina maana wahusika wanaweka udhaifu wao kifuani kwa maslahi ya maisha yao. Na wewe uwe hivyo kwa kutunza siri za mumeo,mkeo.

9 : Msipokuwa wawazi katika kuzungumzia upungufu wa kibinadamu mlionao na kusaidiana
Wapenzi wasomaji wangu, hakuna mwanadamu aliyekamili kwa asilimia mia moja. Ukimuona hodari wa hili ni dhaifu wa lile, kinachotakiwa ni kusaidiana katika kufikia ukamilifu. Faraja inayopatikana katika upungufu wa mwanadamu hasa usiokuwa wa kimaumbile ni kuwepo kwa utatuzi wake. Kuna wapenzi wengi wamefikia kuachana kwa kasoro ndogo ndogo kama za kutojua mapenzi, au hata uchafu wa mwili ambao kama wangekaa na kujadiliana pamoja wangepata ufumbuzi wa tatizo.

Inashauriwa kuwa kunapokuwepo upungufu wowote wa kati ya mwanaume na mwanamke ni wajibu wa wapenzi wenyewe kukaa chini na kuelezana wazi na kushirikiana katika kupata ufumbuzi. Unashindwa nini kumwambia mpenzi wako kuwa hakutoshelezi katika tendo la ndoa, ana harufu mbaya mwilini, mchafu, hajui mapenzi na mambo kama hayo! Kikubwa katika hili ni kujua namna ya kuwasilisha ujumbe, maana kuna wengine hawana lugha nzuri za mawasiliano “Yaani mke wangu unanuka sana mimi nakerwa sana” Ukisema hivi utamfanya mwenzako aone kama unamnyanyapaa. Tumia lugha nyepesi itakayosaidia kumaliza tatizo msikae kimya bila kuzungumzia upungufu wenu mtajikuta mnaachana.

10 : Mkiendekeza nguvu katika kutwaa madaraka ndani ya familia​
Kuna baadhi ya familia kila mmoja ni mtemi hakuna diplomasia katika kutatua migogoro. Utakuta mwanamke ni Mbogo na mwanaume naye ni Simba, basi shughuli inakuwa nzito. Ndoa inakuwa uwanja wa ndodi kila siku kutoana manundu. Hakuna mapenzi ya namna hiyo! Kanuni za mapenzi bora zinakataza wapenzi kutumia nguvu kutwaa madaraka au haki ndani ya familia. Inawezekana kabisa wewe kama mke/ mume ukawa na haki katika jambo fulani lakini haki hiyo haikupi fursa ya kutumia nguvu kuipata.

Kinachotakiwa katika mapenzi ni kuheshimiana, kwani katika hali ya kawaida utumiaji wa nguvu katika kudai haki ndani ya familia ni moja kati ya mambo yaliyoshindwa katika historia kuleta maelewano. Kama unadhani naongopa keti chini ujitathmini tangu umeanza kumchunga mumeo/mkeo na kumbana umepata mafanikio gani, ameacha tabia yake au ndiyo anazidi? Umwamba haufai kutumika katika maisha ya ndoa kwa mtu yeyote awe mwanaume au mwanamke.
11 : Mkiwa watu msioheshimiana mbele za watu na kupenda zaidi kusema kuliko kusikiliza.​
Nimeshuhudia wapenzi wengi ambao hawajui umuhimu wa kuheshimiana mbele za watu. Utakuta mwanamke/mwanaume akimwaibisha mwenzake mbele za watu kwa kumfokea, kumwita jina baya, kumtusi, kumtoa kasoro na hata kumdhalilisha. Kitendo hiki ni kibaya na maumivu yake hudumu kwa muda mrefu akilini mwa mtendewa.

Inashauriwa kwamba wapenzi wanapokuwa mbele za watu wachunge ndimi zao na wawe watu wanaopenda zaidi kusikiliza kuliko kunena. Inaelezwa, penye wingi wa maneno hapakosi kuwa na uovu. Kuna wanawake wakianza kuwatusi waume zao mpaka nyumba ya 50 wanasikia au wakati mwingine hutoka nje na kumwaga mitusi kana kwamba wameambiwa watapewa tuzo. Hiyo si heshima na hajawahi mtu kuheshimika kwenye jamii kwa uhodari wa kutukana watu.


12 : Msipokuwa tayari kukubali kosa na kujirekebisha​

Dalili nyingine ya mapenzi kunyauka ni kwa wapenzi wenyewe kuwa na tabia ya kutokukubali makosa na kujirekebisha. Utakuta mwanaume/,mwanamke ameshaambiwa mara nyingi na mwenza wake juu ya tabia zake na pengine hata marafiki zake wamemtahadharisha lakini habadiliki, kila siku anarudia makosa yale yale ambayo yanamuumiza mpenzi wake. Huu ni mwenendo mbaya, ubinadamu unamtaka kila mtu kuwa tayari kukiri kosa na kujirekebisa

13 : Msipokuwa watu wa kuitafuta furaha pale inapokosekana​
Wakati mwingine harakati za maisha huleta huzuni, kwa mfano, kama wanandoa watafiwa, kuuguza, kufukuzwa kazi, kupoteza mali kwa kuibiwa na matukio kama hayo huondoa furaha. Hapa inashauriwa kwamba endapo furaha itaondoka kwasababu yoyote wanandoa wanajukumu la kuitafuta. Hapa namaanisha kutiana moyo na kuwezeshana kusonga mbele wakiamini kuwa hakuna marefu yasiyokuwa na ncha. Kuacha huzuni itawale nyumba yenu kwa muda mrefu hupunguza mapenzi.

14 : Msipozingatia kuombana msamaha bila kujali nani mwenye kosa​
Kuombana msamaha ni jambo la lazima kabisa katika ndoa, na busara inamtaka mwenza kuwa tayari kuomba masamaha hata kama anaona kabisa hakuna kosa la msingi alilolifanya mbele ya mwenzake. Kung’ang’ania kutaka haki kipindi cha kuzozana ni njia ya kuelekea kukosana zaidi na hatimaye kuachana. “Nakuomba unisamehe mke/mume wangu, najua nimekuudhi.” Baada ya kutoa kauli hiyo na mzozo kupoa mhusika anaweza kufafanua kilichotokea na hapo anaweza kueleweka zaidi kuliko kipindi ambacho mpenzi wake anakuwa na hasira.

15: Msipokuwa tayari kukumbushana wajibu na mwenendo wenu​
“Atajijua mwenyewe siku yakimkuta ya kumkuta huko ndo atafahamu” “Mimi nimechoka nimebaki namwangalia tu.” Kubaki unamwangalia mpenzi wako anaharibikiwa si uamuzi wa busara kwani mwishoni aibu itakufikia na wewe pia. Ukimuona mwenzako anakwenda nje ya mstari wa jamii mrejeshe na kuzidi kumkumbusha kila siku wajibu wake kama baba au mama wa familia, hii inasaidia kumuweka sawa mahali anapokosea.

have_a_nice_day_3.gif

Mwisho
 

Forum statistics

Threads 1,190,580
Members 451,229
Posts 27,675,890