Dalili ya kuyumba kwa mifuko ya hifadhi ya jamii, FAO la kujitoa lafutwa Rasmi

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
mhagama.jpg

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Vijana), Jenista Mhagama.

Dodoma. Serikali imesema fao la kujitoa halipo, badala yake imekuja na fao la bima ya afya.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Vijana), Jenista Mhagama alisema hayo bungeni jana kuwa suala la fao la kujitoa haliwezekani kwa sasa na badala yake imeanzisha mchakato wa fao la bima ya afya ambalo itakuwa ni mbadala wa fao la kujitoa.

“Katiba ya Tanzania katika kifungu cha 11 kinaeleza namna ambavyo mifuko hiyo (akimaanisha ya hifadhi ya jamii) inapaswa kuwa, lakini hata juzi Mheshimiwa Rais aliagiza utengenezwe utaratibu katika bima ya mfuko na itakuwa ni mbadala wa watu wasiokuwa na ajira,” alisema Mhagama.

Mapema bungeni jana, swali kuhusu malipo ya mafao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii liliwaibua wabunge wengi waliotaka kuuliza maswali ya nyongeza licha ya mawaziri kutoa majibu.

Akijibu swali la wafanyakazi waliopatikana na vyeti feki kama wanaweza kulipwa mafao yao, Waziri wa Utumishi Angella Kairuki ali hatuwezi kutoa taarifa kwa sasa kwani bado wanashughulikia jambo hilo ili kuona namna bora ya kufanya na wakifikia hatua nzuri watatoa majibu ya kuaminika na kuomba wapewe muda kwa sasa

Mapema mbunge wa Viti Maalumu, Amina Mollel alitaka kujua kwa nini wafanyakazi waliopatikana na vyeti feki wasilipwe mafao yao.

Naibu wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Anthony Mavunde alisema kuanzishwa kwa mifuko ya jamii kumefikia hatua mbalimbali ikiwamo kukamilika kwa tathimini ya mifuko ya hifadhi ya jamii (actuarial evaluation) ambayo imetoa mapendekezo kuhusu namna bora na mambo ya kuzingatia katika kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii.

“Mpaka sasa Serikali haijafanya uamuzi rasmi wa idadi ya mifuko itakayobaki baada ya kulinganisha mifuko iliyopo hivi sasa,” alisema Mavunde.
 
Nani aliwadanganya kuwa ccm ina nia njema na nchi hii?! Chini ya ccm ni uendawazimu tu kuamini mabadiliko chanya kutokea katika nchi hii

Magufuli pumzi imekata baada ya majipu kumuishia hana jipya tena zaidi ya kutukana Watanzania
 
Kaka sehemu pekee kudhulumu watanzania wanyonge ni kilimo wanawazingua sanaa huko na wafanyakazi wangewapa pesa zao wajiajiri wenyewe kilimo na biashara zao! Wao haiwahusu wamekaa wanalipwapesa za walipa kodi baada miaka 5 wanalipwa mafao yao! Vyama wafanyakazi wamepewa juice, ikulu wametoka kimya ! Pesa Zetu wanaziweka bima afya kwa mkataba gani? Sisi tuliingia mifuko jamaa sio bima afya kwa nini wantulazimisa? Afya gani bila kuwa na pesa???
Inakuwaje mtu ambaye ameacha/kuachishwa kazi, na akakosa ajira mahali pengine na kuamua kuwa mkulima asilipwe mafao yake ili yawe mtaji?
 
Mifuko haina hela,yote imewekeza kwenye long term investments na nyingine serikali imekopa.

Kwa kifupi hali ya hiyo mifuko ni mbaya,serikali inadaiwa matrillioni.
 
Mimi ninavyo fahamu mbadala wa FAO la kujitoa ni unemployment benefit, sasa hii bima ya afya inakujaje tena? Naomba ufafanuzi no kama sielewi hivi!
 
mhagama.jpg

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Vijana), Jenista Mhagama.

Dodoma. Serikali imesema fao la kujitoa halipo, badala yake imekuja na fao la bima ya afya.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Vijana), Jenista Mhagama alisema hayo bungeni jana kuwa suala la fao la kujitoa haliwezekani kwa sasa na badala yake imeanzisha mchakato wa fao la bima ya afya ambalo itakuwa ni mbadala wa fao la kujitoa.

“Katiba ya Tanzania katika kifungu cha 11 kinaeleza namna ambavyo mifuko hiyo (akimaanisha ya hifadhi ya jamii) inapaswa kuwa, lakini hata juzi Mheshimiwa Rais aliagiza utengenezwe utaratibu katika bima ya mfuko na itakuwa ni mbadala wa watu wasiokuwa na ajira,” alisema Mhagama.

Mapema bungeni jana, swali kuhusu malipo ya mafao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii liliwaibua wabunge wengi waliotaka kuuliza maswali ya nyongeza licha ya mawaziri kutoa majibu.

Akijibu swali la wafanyakazi waliopatikana na vyeti feki kama wanaweza kulipwa mafao yao, Waziri wa Utumishi Angella Kairuki ali hatuwezi kutoa taarifa kwa sasa kwani bado wanashughulikia jambo hilo ili kuona namna bora ya kufanya na wakifikia hatua nzuri watatoa majibu ya kuaminika na kuomba wapewe muda kwa sasa

Mapema mbunge wa Viti Maalumu, Amina Mollel alitaka kujua kwa nini wafanyakazi waliopatikana na vyeti feki wasilipwe mafao yao.

Naibu wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Anthony Mavunde alisema kuanzishwa kwa mifuko ya jamii kumefikia hatua mbalimbali ikiwamo kukamilika kwa tathimini ya mifuko ya hifadhi ya jamii (actuarial evaluation) ambayo imetoa mapendekezo kuhusu namna bora na mambo ya kuzingatia katika kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii.

“Mpaka sasa Serikali haijafanya uamuzi rasmi wa idadi ya mifuko itakayobaki baada ya kulinganisha mifuko iliyopo hivi sasa,” alisema Mavunde.
na redudance ndo zimepamba moto huku kwenye maofisi ya watu twafaaa
 
PSPF sasa inawekewa msalaba makaburini pamoja na mashada ya maua!

Serikali imekopa trilioni nane katika mifuko hii,pesa nyingi sana,bunge lisimamie hii mifuko ilipwe hela yake haraka sana,bajeti isipite hivi hivi

Pia bunge liikinge kisheria mifuko hii isikopwe na serikali,iwe marufuku

Bodi za wakurugenzi za mifuko hii zisijae watu wa serikali,ambao ndio wakopaji wakubwa na taarifa za mifuko hii kila mwaka zijadiliwe kwa siku mbili bungeni.
 
mhagama.jpg

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Vijana), Jenista Mhagama.

Dodoma. Serikali imesema fao la kujitoa halipo, badala yake imekuja na fao la bima ya afya.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Vijana), Jenista Mhagama alisema hayo bungeni jana kuwa suala la fao la kujitoa haliwezekani kwa sasa na badala yake imeanzisha mchakato wa fao la bima ya afya ambalo itakuwa ni mbadala wa fao la kujitoa.

“Katiba ya Tanzania katika kifungu cha 11 kinaeleza namna ambavyo mifuko hiyo (akimaanisha ya hifadhi ya jamii) inapaswa kuwa, lakini hata juzi Mheshimiwa Rais aliagiza utengenezwe utaratibu katika bima ya mfuko na itakuwa ni mbadala wa watu wasiokuwa na ajira,” alisema Mhagama.

Mapema bungeni jana, swali kuhusu malipo ya mafao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii liliwaibua wabunge wengi waliotaka kuuliza maswali ya nyongeza licha ya mawaziri kutoa majibu.

Akijibu swali la wafanyakazi waliopatikana na vyeti feki kama wanaweza kulipwa mafao yao, Waziri wa Utumishi Angella Kairuki ali hatuwezi kutoa taarifa kwa sasa kwani bado wanashughulikia jambo hilo ili kuona namna bora ya kufanya na wakifikia hatua nzuri watatoa majibu ya kuaminika na kuomba wapewe muda kwa sasa

Mapema mbunge wa Viti Maalumu, Amina Mollel alitaka kujua kwa nini wafanyakazi waliopatikana na vyeti feki wasilipwe mafao yao.

Naibu wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Anthony Mavunde alisema kuanzishwa kwa mifuko ya jamii kumefikia hatua mbalimbali ikiwamo kukamilika kwa tathimini ya mifuko ya hifadhi ya jamii (actuarial evaluation) ambayo imetoa mapendekezo kuhusu namna bora na mambo ya kuzingatia katika kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii.

“Mpaka sasa Serikali haijafanya uamuzi rasmi wa idadi ya mifuko itakayobaki baada ya kulinganisha mifuko iliyopo hivi sasa,” alisema Mavunde.
Tuliwaonya msiyaingize majini ikulu sasa mtakula jeuri yenu stupid!! Kila haki itaporwa mjue kuwa hao si watu wala binadamu!! watu wanaumizwa eti vyeti fyeki!! kumbe hayana mishahara wala mafao ya haki zao!! Natamka mene mene tekeli na peresi Magufoool
 
Back
Top Bottom