Dalili tisa (9) za mtumwa wa ngono

waneemayote

Member
Oct 20, 2019
56
153
DALILI 9 ZA MTUMWA WA NGONO

1. Akili yako imejaa picha za ngono, na ubongo wako umejaa mawazo ya ngono.

2. Uwezo wako wa kufikiri umeshuka hadi chini ya asilimia 5, na uwezo wako wa hisia umepanda hadi zaidi ya asilimia 95, na akili yako haitofautiani sana na akili ya mbuzi.

3. Huwezi kufanya chochote cha maana maishani kwa kuwa unapoteza asilimia zaidi ya 90 ya muda wako kuwaza na kufanya ngono.

4. Akili yako na hisia zako zimepinda kiasi kwamba usipopata fursa ya kuona picha za ngono au kufanya ngono halisi unakuwa teja, zoba, tayari hata kujiuza.

5. Kutokana na kutumia vibaya akili yako na muda wako, uko katika matatizo makubwa ya kifedha, unalelewa, au unakaribia kufilisika na utaishia kuwa masikini wa kutupwa anayelelewa.

6. Huna raha maishani maana una tamaa kuliko fisi maji, na ukishafanya ngono hutosheki, unataka tena na tena, hivyo umeanza kuwa chizi fresh kwa tamaa.

7. Hupendi mtu, unajipenda mwenyewe, unapenda mwili wako zaidi, huwezi kuoa wala kuolewa, na hujisikii vibaya wala huoni haya kuingilia ndoa za watu wengine.

8. Una roho mbaya sana kwa siri, uko tayari kuumiza mtu kwa ajili ya ngono, uko tayari hata kubaka na kulala na wanyama. Una nuksi na mikosi. Huna mbele wala nyuma.

9. Unataka kuachana na utumwa wa ngono lakini huwezi. Unajuta kila mara na kukusudia kujirekebisha, lakini unaanguka tena. Unasikia kujilaumu na kukata tamaa.

USHAURI
Utumwa wa ngono ni kifungo kibaya sana, lakini huwezi kuchomoka kwa nguvu zako mwenyewe. Unahitaji msaada. Keti chini, jitafakari; magonjwa, umasikini, ufukara, upweke, jela na kifo viko mbele yako. Jehanamu inakungoja.

Unahitaji neema ya Mungu kukuokoa kutoka katika gereza la utumwa wa ngono ulipo sasa, ili uwe huru.

HATUA ZA KUJIKOMBOA
1. Tamka maneno haya ukimaanisha toka moyoni.

Bwana Yesu Kristo, naomba uniweke huru na unipe neema yako ya msaada, niweze kuishinda dhambi. Naomba unisamehe maana sijui nitendalo. Amina.

2. Jiepushe na marafiki ngono wote.

3. Usiangalie tena picha na video za ngono.

4. Nenda Kanisani ukaombewe zaidi. Usiende kwa waganga au kwa wenye imani za majini, watakutupia jini mahaba na mapepo mengine ya ngono, na hali yako itakuwa mbaya kuliko awali.


Mungu akubariki sana.

Credits:RUMONDO
 
"Usiende kwa walio na imani za majini, utatupiwa jini mahaba, una maanisha wenzetu wa upande wa pili ndio hurusha hayo majini..anyway, but tabia zote ulizo oanisha hapo ni zangu pure wala hakuna hata moja yenye sina
 
Kuacha ngono hauhitaji kutaja jina la yesu wala jina la Juma,

cha muhimu ni kujitambua tu .

Ebu jiulize tangu uanze kufanya ngono umepata faida gani ??

Kwanini ufanye zinaa?

Umeshindwa kabisa kuoa??
 
samahani padri mtoa mada ,hivi mfalme Sulemani aliwezaje kuwamudu wanawake wote wale? (nje ya mada)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom