Dalili 6 Zinazopelekea Mwanamke Kufikiria Kuchit!

Dalili 6 Zinazopelekea Mwanamke Kufikiria Kuchit!

Wateule

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2010
Posts
390
Reaction score
368
Kwa mujibu wa Jarida maarufu la MensHealth, kuwa makini na sababu vyanzo vifuatavyo, ambavyo vinaweza kupelekea mke au mpenzio kutoka nje, yaani “Kuchit”.

1. Anatimiza miaka 20, 25, 30, 35…….miaka hii yenye kupishana Tano Tano ni hatari sana kwa Mwanamke, kwani ni nyakati ambazo anaanza kufikiria amefanya nini miaka mitano iliyopita? Atafikiria kwa kina kuhusu maisha yake katika suala zima la mapenzi, na kama hayaendi kama atakavyo, anaweza akatumia fursa ya Kuchit na jamaa mwingine kama njia ya kurekebisha mambo au kujifurahisha nafsi tu! Anasema Don-David Lusterman, PHD. Matukio ya wanawake wasio kwenye mahusiano ya furaha Kuchit yanaongezeka zaidi ya maradufu inapofika siku za sherehe zao za kuzaliwa.
Mwanaume anatakiwa afanye nini basi, ili kuepusha hili janga?: unatakiwa usicheze mbali na sherehe za kuzaliwa za mpenzi wako na sherehe za mwaka mpya, kwani hizi ndio siku ambazo Mwanamke anataka kuwa na mpenzi wake kitandani kuliko siku nyingine zozote.

2. Amepandishwa cheo kazini. Wanawake hupenda kujiwekea mipango na malengo, na wanapofikia malengo hayo- huenda wakajiuliza sasa nini kinafuata? Kama wapo kwenye uhusiano wenye misukosuko, basi ile konfidensi ya mafanikio waliyoyapata kazini inaweza ikapelekea wao kutafuta mahusiano bora zaidi, na hapo ndipo suala la Kuchit huanzia. Pia wanawake wenye mishahara minono wana asilimia kubwa sana ya Kuchit. Uchunguzi uliofanywa na Chuo Kikuu cha Washington uligundua kwamba wanawake wanaotengeneza $75,000 au zaidi kwa mwaka wana nafasi ya Kuchit mara 1.5 zaidi ya wale wanaotengeneza $30,000 kwa mwaka.
Mwanaume anatakiwa afanye nini, ili kuepusha hili janga?: sheherekea na jisikie ufahari kwa mafanikio ya mpenzio, kwani akiona hivyo atajisikia unamjali kama wanavyomjali kazini, hivyo basi hatokuwa na haja ya Kwenda kwa jamaa mwingine kutimiziwa matakwa ya nafsi (emotional support for her accomplishment).

3. Anahamia kuishi nyumba moja na wewe (maalum kwa wale ambao hawajaoana na wanaishi nyumba tofauti). Huenda ilikuwa ni wazo lake ku “move in” na wote mmefurahi, lakini tatizo sasa ni kwamba kutokana na kuwepo kwenu pamoja 24-7, na kushirikiana katika Kila maishani, kunakuwa hamna haja ya kuwa na mazungumzo marefu Kila mara. Hali hii inaweza ikatafsiriwa na Mwanamke kwamba sasa unamuona anaboa, yaani kwa ung’eng’e “boring”. Hivyo basi, inaweza ikapelekea yeye Kwenda nje na kutafuta mtu ambaye “bado anamuona yeye ana mvuto na aboi”, anasema Prof. Stuart Fischoff, wa Chuo Kikuu cha California, Los Angeles. Kwa uchunguzi uliofanywa na Jarida la MensHealth, umegundua kwamba asilimia 41 ya wanawake wanaochit hufanya hivyo na wafanyakazi wenzao.
Hapa pia tatizo huchangiwa na ile hulka ya “mipango na malengo”, ambayo wanawake wanayo kama tulivyogusia hapo mwanzo. Ni kwamba sasa Mwanamke ameshahamia kwako na mnaishi pamoja, kwa mawazo yake kinachofuatia ni ndoa na watoto……sasa kama mwanaume haweki hilo wazi, basi atarajie janga! Mtaalam mwingine wa mapenzi, Susan Heitler, aliyeandika kitabu kiitwacho “Power of Two”, anaongezea kwa kusema “lazima tukubali kwamba wanawake wengi wanataka kuolewa na kuwa na watoto, kwahiyo kama unawabania mojawapo au yote, basi jua kwamba una karibisha hatari ya Mwanamke Kwenda kwa jamaa mwingine, ambaye anaweza akampa hivyo vitu”
Mwanaume anatakiwa afanye nini, ili kuepusha hili janga?: weka wazi kwamba unafikiria kutumia fursa hii ya kuishi pamoja kama mwanzo wa mipango mikubwa ya baadae, yaani ndoa na watoto.

4. Anahisi mwanaume wake amechit. Matembezi ya visasi (revenge affairs) ni ya kawaida katika ulimwengu wetu wa leo. Mwanamke pia huamua kufanya matembezi au tembezi la kisasi katika jitihada za kurudisha hali ya kujisikia kwamba bado na yeye anahitajika, baada ya kuhisi au kugundua kwamba mwanaume wake anachit. Mtaalam Heitler anasema hapa kwamba hii ni hulka ya binaadam kwamba tunapenda kulipiza, kwahiyo Mwanamke akihisi ametendewa, basi nae huenda asiende nje kutafuta, lakini kama jamaa anajitokeza na kuchombeza, anakuwa mrahisi kukubali kutokana na kuwa na hasira za malipizi!
Kwa wale wanaume ambao hamchit, na bado Mwanamke wako haishi kukuhisi, basi huenda una Mwanamke mwenye kutojiamini (low confidence). Hivyo basi, mnashauriwa kutoa compliment za mara kwa mara kutoka moyoni, ili kutuliza nyoyo zao. Na kama mwanaume umechit, basi omba msamaha haraka iwezekanavyo na muonyeshe kwamba hautorudia tena, kama unataka usiwe mhanga wa hasira malipizi!

5. Hapati haki ya unyumba ipasavyo: oxytocin ni homoni(hormone) ambayo inauwezo mkubwa katika kukamilisha matakwa yetu ya kuwa karibu (bonding), yaani kuleta mahaba na ukaribu katika mapenzi. Hii homoni (oxytocin) huongezeka kiwango zaidi ya mara tatu au tano muda machache tu kabla ya kufika kileleni (orgasm). Kwa mijubu wa wataalam, hii homoni ina nguvu zaidi kwa wanawake kuliko wanaume. Kwahiyo basi, wanawake wanatengeneza ukaribu (bonding) zaidi kupitia kujamiiana (sex).
Kama haki ya unyumba haipatikani kama ilivyokuwa siku za mwanzo, basi anaweza akatafsri kama hapendwi tena, na hivyo Kwenda nje kutafuta ampendaye.

6. Amechoka na mahusiano, na yupo tayari kusonga mbele. Hii ni dalili au sababu ya mwisho, ambayo hutumiwa sana, sio tu na Wanawake, bali wanaume pia. David Buss, PHD., Profesa wa Saikolojia kutoka Chuo cha Texas, pale Austin na muandishi wa kitabu kiitwacho “The Evolution of Desire” aliwauliza wanaume 100 na wanawake, ni mbinu gani wanaweza wakatumia kumaliza mahusiano mabovu ya kimapenzi? Moja Kati ya majibu mengi aliyo pasta ni : kuanza mahusiano ya nje, yaani chit!!
Je Mwanaume au Mwanamke unaweza ukafanyaje kuepukana na janga hili?: hamna la kufanya zaidi ya kumuacha aende tu, kwani mpenzi anayetumia njia ya kuchit kama mbinu ya kumaliza mahusiano, hafai.
Mwisho……

Chanzo: Mean’s Health

Tafsiri: Blog ya habari Tanzania | Online Newspaper | Thehabari.com
Short URL: Dalili 6 Zinazopelekea Mwanamke Kufikiria Kuchit! | Blog ya habari Tanzania | Online Newspaper | Thehabari.com

29/09/2013
 
Kwa hiyo mkuu mambo yote hayo ndio hupelekea mwanamke "kuchit"
 
Mengine yanayopelekea tu cheat hata haujayasema af ndo yenyewe kabisa,au itaendelea?
 
fedha mbona hujataja,mwanaume akiporomoka kiuchumi expeect majanga
 
Mengine yanayopelekea tu cheat hata haujayasema af ndo yenyewe kabisa,au itaendelea?

Najua sababu zipo nyingi, ila kutokana na nafasi finyu, itakuwa ngumu kuzitaja zote. Ukiwa kama Mwanamke unaweza ukatupa muendelezo hapa JF......Asante.
 
Kwa hiyo mkuu mambo yote hayo ndio hupelekea mwanamke "kuchit"

Mkuu, unauliza jibu? Sababu zipo nyingi tu, ila makala hiyo imeziangalia hizo tu. Asante.
 
huku bongo hela baba kama wewe una njaazako mwanamke kucheat kawaida sana.. Hizo tuwaachie wazungu huku uswazi sex ni miatano miatano
 
Nadhani anazungumzia wanawake wasomi tena wazungu.

Mkulu

Hilo linatuhusu sana kaka

Hayo yapo...wakati mwingine unajiuliza why didi i got married?...lkn katika vituko vyote...bado NDOA INA RAHA ZAKE...

Ukiweza kutunza ndoa yenye makorokoro yote hayo...tunaweza kukuamini uwe kiongozi wa Jamii kwa capacity mbalimbali...failure tuliyonayo sisi kama taifa IMEANZIA HUKU...MAHUSIANO....
 
^^
Umesahau PESA
Wasione pesa,,utasoma plate number !!
^^
 
mmesahau "utongozaji." kuna watu wanalia atii ili wapewe tu. Kahuruma kadogo tu tayar. Ila hyo namba 3 hapo nahurumia wale wanaotaka uchumba wa miaka 4.
 
naomba unieleweshe mahali hapa sijaelewa:

Mwanaume anatakiwa afanye nini basi, ili kuepusha hili janga?: unatakiwa usicheze mbali na sherehe za kuzaliwa za mpenzi wako na sherehe za mwaka mpya, kwani hizi ndio siku ambazo Mwanamke anataka kuwa na mpenzi wake kitandani kuliko siku nyingine zozote.

2. Amepandishwa cheo kazini. Wanawake hupenda kujiwekea mipango na malengo, na wanapofikia malengo hayo- huenda wakajiuliza sasa nini kinafuata? Kama wapo kwenye uhusiano wenye misukosuko, basi ile konfidensi ya mafanikio waliyoyapata kazini inaweza ikapelekea wao kutafuta mahusiano bora zaidi, na hapo ndipo suala la Kuchit huanzia. Pia wanawake wenye mishahara minono wana asilimia kubwa sana ya Kuchit. Uchunguzi uliofanywa na Chuo Kikuu cha Washington uligundua kwamba wanawake wanaotengeneza $75,000 au zaidi kwa mwaka wana nafasi ya Kuchit mara 1.5 zaidi ya wale wanaotengeneza $30,000 kwa mwaka.
Mwanaume anatakiwa afanye nini, ili kuepusha hili janga?: sheherekea na jisikie ufahari kwa mafanikio ya mpenzio, kwani akiona hivyo atajisikia unamjali kama wanavyomjali kazini, hivyo basi hatokuwa na haja ya Kwenda kwa jamaa mwingine kutimiziwa matakwa ya nafsi (emotional support for her accomplishment).
 
wana jf i blive in trust bhna kama kweli mnapendana haijalish alafu na nyie wakaka mnachangia xana mana wengi hamjui kujali wapenzi wenu alafu hata malengo au future hamna xo unapokuwa na mpenzi mjali mtunze na umweshim xana hapo mtadum na kama hujampenda mwanamke alivyo bora ucwe naye kabisa wanawake cku hz wamebadilika shida ipo kwenu wakaka macho yenu yanataman xana hyo.ni mbaya mana kuna mda utahc mpenzi wako anakuchit kumbe wala pia haipendezi mwanaume uwe hauna kazi unamtegemea gel hvyo lazma uwaze anakuchit kumbe la. we have 2 think big mana mahuciano yanahitj moyo na uvumilivu
 
mkuu kaongea ukweli na huu angalau ndo mfano wa mwanzo kuwa great thinker, kuna watu wanadai kaacha vitu kibao kama pesa n.k. lakin niwambie kitu, jamaa kaongelea mapenzi ya kweli the way ambavyo mwenza mmojawapo anaweza mchit mwenzie, tukisema pesa hata hivyo ameisema japo sio direct, pale aliposema kuwa na mshahara mkubwa, ukisema pesa moja kwa moja hapo unaongelea biashara ya ngono na sio mapenzi aliyosema jamaa kwenye uzi wake
 
naomba unieleweshe mahali hapa sijaelewa:

Mwanaume anatakiwa afanye nini basi, ili kuepusha hili janga?: unatakiwa usicheze mbali na sherehe za kuzaliwa za mpenzi wako na sherehe za mwaka mpya, kwani hizi ndio siku ambazo Mwanamke anataka kuwa na mpenzi wake kitandani kuliko siku nyingine zozote.

2. Amepandishwa cheo kazini. Wanawake hupenda kujiwekea mipango na malengo, na wanapofikia malengo hayo- huenda wakajiuliza sasa nini kinafuata? Kama wapo kwenye uhusiano wenye misukosuko, basi ile konfidensi ya mafanikio waliyoyapata kazini inaweza ikapelekea wao kutafuta mahusiano bora zaidi, na hapo ndipo suala la Kuchit huanzia. Pia wanawake wenye mishahara minono wana asilimia kubwa sana ya Kuchit. Uchunguzi uliofanywa na Chuo Kikuu cha Washington uligundua kwamba wanawake wanaotengeneza $75,000 au zaidi kwa mwaka wana nafasi ya Kuchit mara 1.5 zaidi ya wale wanaotengeneza $30,000 kwa mwaka.
Mwanaume anatakiwa afanye nini, ili kuepusha hili janga?: sheherekea na jisikie ufahari kwa mafanikio ya mpenzio, kwani akiona hivyo atajisikia unamjali kama wanavyomjali kazini, hivyo basi hatokuwa na haja ya Kwenda kwa jamaa mwingine kutimiziwa matakwa ya nafsi (emotional support for her accomplishment).

Naomba uwe specific, ni wapi haujaelewa?
 
Kila siku tunalia na aina hii ya uandishi !!
Twisheni leo hujaenda ??
 
Msuguo ndiyo mpango mzima, ukipanda kama kuku dakika 3 umemaliza nani akusubiri! hela haina mpango hata siku moja kila matu ana uwezo wa kumake maoney ila ile issue siwezi fanya mwenyewe lazima dume la mbegu lije, likija lege lege linabwagwa vile vile
 
Back
Top Bottom