Dalili 5 za Mtu asiyejiamini

Dalili 5 za Mtu asiyejiamini

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,113
Reaction score
34,953
[h=3][/h]

KUJIAMINI ni hali ya kuwa na uhakika juu ya kile unachokifanya, tenda, nena na hata muonekano kwa ujumla.

Kujiamini kunasaidia sana katika kutafuta njia ya mafanikio maishani. Ni suala la muhimu sana kujiamini.

Mwandishi mmoja wa vitabu vya saikolojia, Ben Carson aliwahi kuandika;
‘Confidence can pull you to success’ (Kujiamini kunaweza kukusogeza palipo na mafanikio).
Kwa nini watu hawajiamini? Kutojiamini kunatokana na nini? Haya ni baadhin ya maswali ambayo ni lazima tujiulize.
Utamjuaje mtu asiyejiamini? Hapa chini nitaainisha dalili tano za mtu asiyejiamini kabisa. Lakini pia kabla sijaendelea mbele zaidi, naomba niweke kumbukumbu sawa kuwa, mtu asiyejiamini ni nadra sana kufanikiwa maishani.

KULALAMIKA

Dalili ya awali kabisa ya mtu asiyejiamini ni pamoja na kulalamika kila mara. Yaani jambo dogo tu lakini malalamiko yanakuwa mengi kupita jambo lenyewe.

Mwanasaikolojia mmoja nchini Marekani, Willie Jollie katika kitabu chake cha It Only Takes A minute to Change your Life, aliandika kuwa;
‘Too much complaining proves how weak and unconfident you are’ (Kulalamika kupita maelezo kunathibitisha ni kwa namna gani ulivyo dhaifu na hujiamini).

Mtu wa kulalamika, anakuwa hawezi kujisimamia juu ya jambo f’lani pasipo uwepo wa wengine na pia kulalamika sana kuonesha ni jinsi gani hujiamini katika kufanikisha mambo maishani.
Lakini pia, kulalamika kunaambatana na woga katika maisha kwani mara nyingi mtu muoga haishi kulalamika hasa anapoachiwa jambo f’lani alitende peke yake. Hivyo dalili ya awali kabisa ya mtu asiyejiamini ni pamoja na kuendekeza tabia ya kulalamika kila wakati.

Mtu anayejiamani hapendi kulalamika, badala yake hutenda mambo kwa vitendo na si malalamiko.
Lakini pia, tafiti za kisaikolojia zinaonesha kuwa, watu wanaopenda kulalamika ni wale wenye maneno mengi ambao kazi yao kubwa ni kuongea na si kutenda. Hili ni jambo baya sana maishani. Achana na maneno mengi, jiepushe na tabia za kalalamika ovyo, fanya kazi kwa vitendo huku ukitumia muda mwingi kuwa kimya.

KUTEGEMEA SANA WENGINE

Kuna baadhi ya watu hawawezi kufanya jambo lolote maishani pasipo kutegemea mawazo ya wengine. Hata kama jambo hilo liko ndani ya uwezo wake lakini hawezi kulitenda hadi atakapoambiwa na watu, sasa tenda.
Watu hawa huwa na uwezo mkubwa sana ndani yao lakini hushindwa kujisimamia wenyewe. Hata kama ana fedha kiasi gani, lakini hawezi kutenda jambo bila kusukumwa.

Mfano utakuta mtu anataka kuchukua hatua fulani nzuri sana lakini anashindwa hadi baadhi ya watu wamuamulie ndipo atende.
Mfano mtu amegombana na mkewe anakuwa hawezi kuamua nini cha kufanya juu ya suala hilo na hapo ndipo atakimbilia kwa rafiki zake kuwaomba wamsaidie nini cha kufanya jambo ambalo huashiria ni kiasi gani hajiamini.

Usiishi kwa mawazo ya wengine. Hata wewe una akili kama wao na pengine kuwashinda lakini unakuwa huna uhakika na unachokiwaza na kuona kama bila wao huwezi kujisimamia maishani. Hii ni hatari sana. Jitegemee, jiamini, tenda mambo kwa kutegemea muongozo wa upeo, busara, maarifa, akili na mawazo yako mwenyewe. Ni suala la utulivu tu.
 
Naendelea kuchambua mada yetu tuliyoianza wiki iliyopita na sasa nahitimisha na dalili nyingine zilizosalia. Twende pamoja...

KUSITA KATIKA MAAMUZI

Kipengele hiki hakiko mbali sana na kilichotangulia lakini kuna baadhi ya vitu katika kuelekezana. Kwamba unakuta mtu ana vitu vingi sana kichwani mwake lakini hawezi kuchukua hatua kuvikamilisha na kuviweka katika hali ya utendaji.
Hapa nazungumzia suala la kusita katika kuchukua hatua juu ya unachokiwaza na kukifikiria maishani. Mfano labda mtu yuko kijijini, ana kipaji cha kuandika habari au ana ndoto za kuwa mfanyabiashara, ameamua kwenda mjini kutafuta hizo njia za kumuwezesha kutimiza ndoto yake. Tatizo linakuja katika kuchukua hatua za utekelezaji juu ya jambo hilo. Anakuwa hajiamini kama anaweza kukaa mbali na nyumbani kwao. Anakuwa mtu wa kusita katika kufanya maamuzi sahihi.
Wakati mwingine una rafiki ambaye hakika hana faida yoyote kwako, yeye ni mtu wa kukunyonya tu lakini hana mchango wowote kwako. Sasa unashindwa kufanya maamuzi sahihi ya kuachana naye kwa kuhofia kuwa bila yeye utapwaya. Eti umemzoea sana. Huku ni kusita katika maamuzi ambapo nasema ni dalili ya kutojiamini. Usisite, chukua uamuzi muafaka tena kwa wakati. Jiamini katika kuamua mambo.

KUJIKOSOA

Hii ni dalili kubwa sana ya kutojiamini maishani. Unakuwa ni mtu wa kujifananisha na wengine kisha kujishusha katika thamani. Hapa nazungumzia watu walio na mawazo mazuri sana lakini kabla hujayawasilisha kwa watu, unaanza kujikosoa. Hivi kweli hili ni jambo jema kulisema? Au nitaelewekaje? Watakubali kweli mawazo yangu? Yaani ni mtu wa kujikosoa kila wakati, kuona kama huna kitu cha kusema au kuwasilisha kwa wengine.
Achana na tabia ya kujilinganisha na wengine. Iwe kwa mavazi, fedha, uzuri wa sura nk. Jione kuwa wewe ni bora kuliko wengine kama yeye ni mzuri wa sura, basi ni yeye. Kama ana nguo nyingi kuliko wewe sawa. Lakini jambo la msingi hapa ni kujiamini na kuondoa zana ya kujikosoa. Mchango wako ni mkubwa sana katika jamii . Ni suala la wewe kujiamini. Jiamini kuanzia leo.

WIVU

Hapa nazungumzia wivu ambao hauna maana hata kidogo. Utakuta mtu anampinga mtu pasipokuwa na sababu maalum. Unakuwa mtu wa kuwapinga wengine kila wakitaka kufanya jambo muhimu la kimaendeleo kwa kuhofia tu kuwa watakuzidi kwa sababu hujiamini katika utendaji wako wa mambo.
Unakuwa unawaza, f'lani akifanya hivi atanizidi katika suala hili, au akifanya hiki mimi nitaonekana sifai mbele za watu na jamii kwa ujumla. Ni mtu wa kuwaza uwezo wa watu pasipo kujifikiria mwenyewe. Achana na wivu wa kutojiamini. Jiamini sasa. Kwa kufanya hivyo kila kitu kitanyooka na maisha utayaona yapo tofauti.

MUHIMU

Maisha yanaendelea kama kawaida, jitahidi kuondoa zana zote potofu katika maisha, ondoa fikra za kushindwa hata kidogo kani wewe hukuumbwa kuja kuteseka hapa chini ya jua.
 
Mfano mdogo wa kuona watu wasiojiamini ni hapa JF.
"
Unakuta mtu amenuniwa na mkewe anakuja hapa kuomba ushauri
"
Sisemi kuwa ni vibaya kuomba ushauri,hapana,ila ni vyema ukaangalia na tatizo lenyewe.
"
Sio unapigiwa simu unaambiwa jana mkeo alikua na mtu,unahamanika na kukimbilia JF.
"
Tulia kisha uamue kama kuna haja ya kuthibitisha kauli hiyo ama la!
 
Mfano mdogo wa kuona watu wasiojiamini ni hapa JF.
"
Unakuta mtu amenuniwa na mkewe anakuja hapa kuomba ushauri
"
Sisemi kuwa ni vibaya kuomba ushauri,hapana,ila ni vyema ukaangalia na tatizo lenyewe.
"
Sio unapigiwa simu unaambiwa jana mkeo alikua na mtu,unahamanika na kukimbilia JF.
"
Tulia kisha uamue kama kuna haja ya kuthibitisha kauli hiyo ama la!

Duh!ngoja waje wasiojiamini!!
 
ENDELEA KUTOA DONDOO ZA WATU WASIOJIAMINI ILI TUWATAMBUE!

Je! tabia ya kutamba mbele za watu kwa vitu visivyo na maana je?

Unamkuta mwanaume anatamba kwamba eti yeye nyumbani kwake huwa anafagia uwanja na kuosha vyombo..... likoje!

Mwanamke anatamba eti yeye hata akirudi nyumbani amechelewa hakuna m2 wa kumgombeza.... hiyo je!

Mtu anatamba kuwa mwenza wake hana ubavu wa kumuacha labda aamue mwenyewe kuacha ... na hiyo!
 
Back
Top Bottom