daladala za dsm na mziki wa taarab/mipasho.

daladala za dsm na mziki wa taarab/mipasho.

kadoda11

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2011
Posts
21,453
Reaction score
20,755
wadau baada ya kuwadondoshea thread iliyohusu kuhitaji ajira usalama wa taifa,hapa tena nashusha nyingine.
kwa wale wenzangu na mimi wanaoutumia usafiri wa daladala sio wageni wa hili jambo.mimi sio shabiki wa mziki wa taarab.iwe asilia,modern
na hata hii ya sasa ya wacheza KIDUKU(sijui wenyewe wanaiitaje).karibu daladala zote haijalishi ni za root ya wapi-kutwa ni kupigiwa
taarab tuu mpaka kero.tangu ningali mtoto mpaka sasa nimekuwa nikichukulia mziki huu kuwa ni wa kinamama-kutambiana,kuonyeshana umwamba,jeuri,mikogo nk.madereva wa daladala/makondakta nao tuwaingize kwenye kundi lipi?nawasilisha.Big tym,week end njema.
 
Wameathirika na mijimama ya kipwani,kana kwamba Tanzania hatuna miziki mingine mizuri kazi ni uswahili tu mwisho wa siku watu wote wanakuwa wanamipasho
 
kinachonishangaza makonda wengi na madereva wapo kisela saana

halafu unakuta wameweka cd ya taarab
yaani vitu viwili tofauti.....lol
 
Ukiona hivyo ujue unauza zaidi huku uswahilini. Sio vizuri private interest kuifanya iwe public interest hivyo wapo wanaopenda na wasiopenda kama wewe labda ungetoa takwimu uonavyo wewe na athari zake.
Sorry mkuu, hivi unapo tu remaind threds zako huwa unamaana gani?
 
napeda sana.. taarabu... na wala sijaathirika na mijimamama... sana sana taarabu asilia...

ni muziki tuliokuwa nao sisi waatu wa pwani... sasa nashangaa sijui kwa nini watu wa bara iwaume hivoo
 
Labda hawa husikiliza Taarabu ili waweze kupata vijineno vya kuwaambia abiria, manake hawa jamaa kwa maneno ya kiswahili hawajambo....
 
Sasa miziki ya mbele lugha nayo utata kwa hawa watu
 
We mshabk wa masharobaro nn? Kwa m2 mwenye kuutambua mzk nadhan taarabu anaipa heshma yake...achlia mbal hz za mnaowaita wacheza kduku zenye burudan ya pekee kunazleee aslia zlzokuwa na mafundsho ya mana ktk jamii.
 
Vile vile kuna mabasi mengine huwa yanaweka miziki ya kwaya lakini tunapanda na kustahmili tu, ndiyo dunia hiyo kuvumiliana. Kama hupendi kitu mwenzako anakipenda basi wewe vumilia tu.
 
Ukiona hivyo ujue unauza zaidi huku uswahilini. Sio vizuri private interest kuifanya iwe public interest hivyo wapo wanaopenda na wasiopenda kama wewe labda ungetoa takwimu uonavyo wewe na athari zake.
Sorry mkuu, hivi unapo tu remaind *threds* zako huwa unamaana gani?
nitakujib subir kidooogo.nina kikao na wakuu wangu.hapo kwenye alama za nyota sio threds ni threads.lol
 
Hivi kwenye usafiri wa umma (public transport) kama dala dala, muziki unaowekwa unatakiwa uwe ule wanaopenda abiria au dereva na kondakta wake? Manake mie nishapanda basi nikakuta mwingine kaweka nyimbo za kwaya za Kikristo, mwingine kaweka akina Rose Mhando, mwingine kaweka taarabu, mwingine kaweka kaswida, nk. Abiria ni mpitaji katika basi hilo, ukifika kituo chako unashuka. Kama huupendi huo muziki inabidi kuvumilia au kuteremka; na utakuta kuna wenzio wanasuuzika nyoyo zako. Maisha ndivyo yalivyo!
 
we we si upo dar unashangaa nn na huo ndo muziki wa pwani kama vp rudi kwenu ukasikilize muziki wa kwenu, endeleeni madereva wa daladala
 
tuko pwani hapa tupeni muziki wenye ladha ya pwani
Wameathirika na mijimama ya kipwani,kana kwamba Tanzania hatuna miziki mingine mizuri kazi ni uswahili tu mwisho wa siku watu wote wanakuwa wanamipasho
 
bora ya ww bintimkongwe umenena, kinachotakiwa ni kuvumiliana tu na mara nyingi muziki wanaweka dereva na konda wapate kuburudika wao ndio wanashinda kwenye gari kutwa nzima sie tunapita kwa muda ukifika kituo chako unashuka so vumulia muziki hata kama huupendi toa simu yako ya mchina kula muziki uupendao
Vile vile kuna mabasi mengine huwa yanaweka miziki ya kwaya lakini tunapanda na kustahmili tu, ndiyo dunia hiyo kuvumiliana. Kama hupendi kitu mwenzako anakipenda basi wewe vumilia tu.
 
Wakati mwingine mziki ukiusikia kwa mda mrefu inatokea kuupenda nadhani hata wao wana-adopt kutoka kwa wake zao
 
Back
Top Bottom