Daladala za Arusha kwa mrombo zagoma, abiria watembea kwa miguu kuja mjini

Kuna mtu wangu wa karibu yuko Arusha Mr Andrew Ngobole, anasema "Hali ni tete hapa mjini, makonda, madereva na wapiga debe wa stend ndogo wamejikusanya 'Soko Mjinga' wanahakikisha hakuna daladala linalopakia abiria.... njia ya Mjini, Sanawari, Ngulelo mpaka USA magari yanafanya kazi kama kawaida"
 
Kwenye mida ya saa tatu hivi nilipishana na magari mawili ya polisi maeneo ya ngulelo yakiwa kwenye mwendo wa kasi huku wamewasha taa za mbele na ving'ora
 
shidaa...nn tena jaman jiji letu la amaniii...hii serikali mbona inazingua wajameniii!!
 
Shida Arusha ni wakuu wa mikoa kila anaekuja anataka onyesha kuwa kuna mtu mpya Arusha, malongo alibadilisha eneo la wazi kuwa soko eti ili chadema wakose eneo la kufanyia mikutano, alifeli kwa kuwa mikutano inaendelea, huyu alokuja kaja na route zake na sumatra wako kimya tu, inakuwaje abiria wa kijenge, moshono wapitie filips wazunguke sanawari kuja mjijni wakati njia ya mwanzo ilikuwa ndio sahihi na abiria wote wanaunga mkono hii, wengi wanashuka Naaz hotel na NBC wengine wanaishia sokoni na friends kona gari linabaki tupu, sasa unataka wazunguke sanawari wakashuke stand ndogo wachukue gari gani tena kurudi vituo vyao vya mwanzo? ushuke stand halafu utembee mpaka Naaz hotel, au unaenda AICC? Hata abiria wameunga mkono hizi route sio, hawa viongozi wa CCM ndio tatizo, sio watu wanapayuka tu LEMA, LEMA, hawa ccm ni janga Arusha, walivunja vibanda vya wauza matunda pale uzunguni, Lema akauliza jiji sababu ni nini wakakosa jibu zaidi ya kuwaambia wa mama wa watu wajenge vibanda vyao na kuendelea na biashara bila kujali hasara waliyo wasababishia. Huyu RC ajiangalie upya au kwa kuwa yeye ana gari lake ndio maana hajali walalahoi? Huko usa, tengeru, ngaramtoni na njia yote ya Moshi, na njia ya ngaramtoni hawawezi goma kwa kuwa hawana route mpya, eti mkuu hataki daladala katikati ya mji, ajabu sana usafiri wa wengi kuwa kero kwa viongozi wa nchi hii.
 
Arusha bana kutoka town-kwamromboo au town -majengo ya juu au town-njiro kwangu mimi hata wagome mwaka poa tu, kwa mtu ambaye hajafika Arusha ni kama kutoka kariakoo - magomeni usalama ila kwa mboga 15 parefu
 
Bora aondoe ujinga ktk ya Jiji.
Mbagala Mwenge.
Gongo la Mboto Msasani.
RC chapa kazi Arusha irudishe Hadhi yake.
Ukifika unakuta Jiji chafu na kituo kila mita kumi kumi.
Wamezowea upumbavu KOMESHA KABISAAA usitishiwe Nyau
 
Daladala zagoma mji mzima, wananchi wanatembea kwa miguu, vikundi vya makonda vinappiga wenzao waliobeba abiria, wanavunja vioo, ni tatizo kubwa...

Bora SUMATRA waruhusu Costa zifanye kazi ya kusafirisha abiria Jijini.
 
Watazoea tu hizo ruti mpya/ndefu.
Sumatra na wadau wengine simamieni hapohapo. Barabara zimefunguka vizuri sana.

Mkuu ilikuwa kero sana yani...Imagine ruti ya Unga-ltd town mita 800...Mjini kunajaza mafoleni yasiyo na maana...

SUMATRA kazeni hapo hapo..Mwanzo mgumu...WAtazoea tuu
 
Njaa ikiwakamata wenyewe wataendelea na kazi.wao waendelee kugoma hivyohivyo.mfano hapo majengo mpk mjn cyo mbali kbsa hivyo tutaenda kwa mguu.tena bora walivyohamishwa kule juu mana walikuwa wanazingua.
 
Back
Top Bottom