Daladala wajipatia pesa kupeperusha bendera za CCM Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Daladala wajipatia pesa kupeperusha bendera za CCM Arusha

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ibrah, Oct 6, 2010.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Nimehakikishiwa kuwa bendera za CCM sasa ni dili kwani baadhi ya madereva wa Daladala Arusha wanakunja shilingi elfu 10 kwa kukubali kupeperusha bendera za CCM kwenye Magari yao!

  Mgombea wa CCM Arusha amepaniki maana daladala nyingi za hapa mjini zinapeperusha bendera za CHADEMA ambazo hutolewa bure na kwa hiyari. Hali hiyo imepelekea Wapambe wa mgombea huyo kuwashawishi madereva wa daladala kupokea bendera za CCM na kuzipeperusha kwenye magari yao.

  Inaonekana Mgombea Ubunge wa CCM Arusha ana pesa nyingi sana maana kama Wapambe wanaweza kutoa shilingi elfu 10 ili kupeperusha bendera kwenye gari wao wanabaki na ngapi?

  Wajinga ndio waliwao!
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,507
  Trophy Points: 280
  Usijali sana wenye sauti ni sisi wapigakura na wala siyo wao.

  Hata hao wanaopepeprusha bendera ya CCM kwa ugali kura zao haziendi CCM. Hapo ndipo mtu atabana na masikio yake.
   
 3. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chakachua pesa yao kwenye kibox ni W.Slaa (PhD)
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Oct 6, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Du kweli hawa jamaa hawafai yaani wanataka uongozi kwa nguvu zote, lakini mwaka huu wataisoma!
   
 5. MwanaCBE

  MwanaCBE JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2010
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,773
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Hii tabia ya kujipendekeza na vibendera vya CCM huwa inanikera sana hasa kwa watu wanaofanya shughuri zao maeneo ambayo ni illegal Dodoma mjini.
   
Loading...