Daktari wa Michael Jackson hatiani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Daktari wa Michael Jackson hatiani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shine, Nov 8, 2011.

 1. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Daktari binafsi wa Michael Jakson, Dk Conrad Murray amekutwa na hatia ya kosa la mauaji bila kukusudia na mahakama moja mjini Los Angeles, Marekani. Baraza la wazee wa mahakama - wanaume saba na wanawake watano - walichukua siku mbili kujadili kesi na kufikia hukumu hiyo.
  [h=2]Taarifa zinazohusiana[/h]

  Michael Jackson alifariki Juni 25 mwaka 2009 kutokana na kuzidisha kipimo cha dawa ya usingizi.

  [h=2]Adhabu[/h] Murray, 58, anaweza kukabiliwa na adhabu kamili ya kwenda gerezani kwa miaka minne na kupoteza leseni yake ya uganga.
  [​IMG]Michael Jackson alipanga kurejea jukwaani mwaka 2009


  Wanasheria wa Dk Murray walihoji kuwa Michael Jackson alijidunga mwenyewe dawa hiyo wakati daktari wake akiwa nje ya chumba.
  Dk Murray alipelekwa rumande baada ya kukutwa na hatia na atasalia huko hadi wakati atakaposomewa adhabu yake, inayotarajiwa kutolewa Novemba 29.

  Akielezea uamuzi wake, jaji alisema Dk Murray kwa sasa ni mhalifu aliyekutwa na hatia na kwa kuwa anafahamiana na watu nje ya jimbo la California, inamaanisha hakuna uhakika kuwa daktari huyo ataweza kubakia bila kutoka katika jimbo hilo.
  [h=2]Rumande[/h] Dk Murray alibaki kimya mahakamani hapo, akijisogeza kidogo katika kiti chake wakati hukumu ikisomwa.
  Maafisa wa mahakama walianza kumfunga pingu daktari huyo wakati jaji akikamilisha kusoma hukumu, na baadaye kupelekwa rumande.
  Baraza la wazee - lililoundwa na wazungu weupe sita, Mmarekani mweusi mmoja na Wamarekani watano wenye asili ya Hispania - walijadili shauri hilo kuanzia Ijumaa hadi Jumatatu asubuhi.
  [​IMG]Shabiki wa Michael Jackson nje ya mahakama


  Nje ya mahakama, mashabiki wa Michael Jackson walikuwa wakishangilia na kuimba "Hatia! Hatia!" muda mfupi kabla ya hukumu kusomwa.
  Wakati wa wiki sita za kusikilizwa kwa kesi hiyo, mashahidi 49 na zaidi ya vipande 300 vya ushahidi viliwasilishwa mahakamani hapo.
  Michael Jackson ambaye alikuwa kimya katika ulimwengu wa sanaa kwa miaka kadhaa, alikufa mwaka 2009 wakati akijiandaa kufanya mfululizo wa maonesho katika ukumbi wa 02 jijini London.
  [h=2]Kuwa na baba[/h] Katika hoja za mwisho mahakamani siku ya Alhamisi, upande wa mashtaka ulisema Dk Murray alisababisha kifo cha nyota huyo kutokana na uzembe, na hivyo kuwanyima watoto wa Jackson haki ya kuwa na baba.
  Upande wa utetezi ulihoji kuwa Jackson alikuwa amejizoesha kutumia dawa, kitu ambacho kilisababisha kifo chake kutokana na kujipa kiwango kikubwa cha dawa ya huku daktari wake akiwa nje ya chumba katika jumba alilokuwa amekodi nyota huyo mjini Los Angeles.

  BBC
   
 2. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 937
  Trophy Points: 280
  Ah, mtu wenyewe alikuwa wa kufa tu! wanamuonea dakitari wa watu.
   
 3. s

  sportslady New Member

  #3
  Nov 15, 2011
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haikuwa na sabab ya kumhukum dkt coz washasema hakukusudia,alipaswa kuachwa huru.
   
 4. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #4
  Nov 15, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 937
  Trophy Points: 280
  Hivi therapies ambazo huwa zinafeli madaktari waliozifanya huwa wanahesabika ni wauaji eh?
   
Loading...