RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Uongozi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure umemnasa mkazi wa Nyakato Mecco jijini Mwanza David Igwesa kwa tuhuma za kujifanya daktari na kupokea pesa toka kwa baadhi ya wagonjwa wanaohitaji kufanyiwa upasuaji.
Daktari huyo ‘feki’ amekamatwa na uongozi wa hospitali ya Sekou Toure, baada ya kuomba shilingi laki tano kutoka kwa Bw. Tungu Sibula kwa ajili ya kumfanyia upasuaji baba yake mzazi, aitwaye Dotto Sibula mkazi wa Tinde Shinyanga, hata hivyo mgonjwa huyo alifanikiwa kulipa shilingi laki moja na elfu sabini tu, kati ya kiasi cha pesa alichoombwa na daktari huyo.