Daktari ataka ukeketaji uhalalishwe

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,146
13,216
images

Daktari mmoja nchini Kenya amewasilisha kesi mahakamani akitaka upashaji tohara wa wanawake ambao hufahamika pia kama ukeketaji uhalalishwe.

Dkt Tatu Kamau anasema sheria inayoharamisha ukeketaji wa wanawake na wasichana inakiuka utamaduni katika jamii nyingi za Kiafrika.

kadhalika, amesema ni ubaguzi dhidi ya wanawake ikizingatiwa kwamba upashaji tohara wa wanaume unakubalika kisheria.

Daktari huyo anataka pia bodi ambayo iliundwa nchini humo kukabiliana na upashaji tohara wa wanawake ivunjiliwe mbali.

Aliwasilisha kesi hiyo katika Mahakama Kuu mjini Machakos, mbele ya jaji David Kemei.

Kesi hiyo itaanza kusikilizwa mwezi ujao.

Dkt Kamau, akizungumza na wanahabari baada ya kuwasilisha kesi yake, alisema wanawake wote, sawa na watu wazima popote pale, wanafaa kuruhusiwa kufanya uamuzi kuhusu miili yao wenyewe bila kuwekewa vikwazo na sheria.

Amesema ukeketaji ni neno ambalo lilitetwa na watu kutoka nchi za Magharibi

Daktari ataka ukeketaji uhalalishwe Kenya
 
Pumbavu huwezi kufanya maamuzi na mwili wako ambayo yatawagharimu wengine na taifa
 
Back
Top Bottom