Daktari ashauri watu kupima DNA kabla ya kuoana

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
DAKTARI bingwa wa magonjwa ya damu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Dk Elineema Meda, amewashauri vijana kupima vinasaba (DNA) kabla ya kuona ili kuepuka kupata watoto wenye ugonjwa wa selimundu.

Akizungumza na MTANZANIA katika mahojiano maalum jana jijini Dar es salaam, Dk Meda alisema ni vema vijana kupima ili kujua kama wanachembechembe za selimundu kwani itasaidia kupunguza kasi ya ugonjwa huo.

“Ugonjwa huu wa selimundu unatokea pale ambapo wazazi wote wawili watakuwa DNA yenye chembechembe za selimundu, hapa ndio kunauwezekano wa wazazi kuzaa watoto wenye ugonjwa huo au hata kama hawana watakuwa na chembechembe za selimundu.

“Kasi ya ugonjwa wa selimundu imeongezeka katika bara la Afrika lakini ninachosema ni kuwa ugonjwa huu unaepukika kama vijana au wazazi watakapoamua kupima DNA kabla ya kuoana kwani wakishajua wanaweza kufanaya maamuzi ya kuchagua,”alieleza Dk Meda.

Kwa mujibu wa Dk Meda alisema utafiti uliofanywa na Muhimbili unaonesha kati ya watu 100 waliofanyiwa vipimo, 13 wanachembechembe za selimundu.

Alisema ikiwa vijana wanaendelea kuoana bila kupima DNA kujua kama wanachembechembe za selimundu, kuna uwezekano ugonjwa huo ukaendelea kuongezeka.

Dk Meda alipendekeza vipimo vya selimundu kufanywa kwa watoto wanaozaliwa kwani itasaidia kupata tiba mapema na kuokoa maisha yao.

“Wapo watoto wengi tu wanaopoteza maisha kutokana na kuchelewa kupata chanjo na matibabu ya ugonjwa huu, mimi natoa mapendekezo ya kuanzishwa kwa vipimo vya selimudu pindi watoto wanapozaliwa ili wakigundulika mapema wapewe chanjo na tiba haraka kama ilivyo kwa magonjwa ya surua, pepopunda, polio na mengineyo,”alisema Dk Meda.

Pia alitoa wito kwa wazazi kuwawahisha hospitali watoto wao pindi watakapoona dalili wasizozielewa na si tu kuwanunulia dawa na kuwapa.
 
Huu ugonjwa hauna tiba??na je ikitokea baada ya kupima mtu na mwenza wake wakakutwa wote wanahizo chembechembe ila wakaamua tu kuzaa hakuna njia ya kuzuia maambukizi kwa mtoto??

Cc Kingsmann
Huu ni ugonjwa wa kurithi, hauambukizwi. Kuzuia kwake ndio inatakiwa ujue vinasaba(DNA) vyenu na mwenza wako unayemtarajia kama Dokta alivyoshauri.

Wewe unaweza ukawa na chembe chembe halafu mwenza wako akawa hana, miongoni mwa watoto wako watakuwa na chembe chembe, watoto wengine hawatakuwa navyo.

Mtoto mwenye chembe chembe akija kuoa/kuolewa na mwenye chembe chembe kama yeye ndio watazaa(wajukuu wako hapa) wenye huu ugonjwa na wengine watakuwa na chembe chembe.

Kwa hiyo mzazi mmoja akiwa na chembe chembe za Selimundu ataurithisha kuanzia kwa wajukuu zenu au atarithisha hizo chembe chembe endapo mtoto wenu atapata mwenzi asiye na chembe chembe.

Kwenye Biology kidato cha 4 tulijifunza Genetics(Masuala ya kurithi), ndio ninacho kizungumza hapa
 
Na inakuwaje endapo majibu ya mmoja wetu hana hizo chembechembe za selimundu mtoto atakaepatikana anachances za kuupata au la

Cc Kingsmann

Mtoto hatakuwa na disease bali atakuwa na traits za sickle cell. Kwa hiyo huko mbeleni ana chances kubwa ya kuzaa watoto wenye sickle cell disease endapo ataoana na mume/mke mwenye traits hizo pia.

Cc Unforgetable
 
Huu ni ugonjwa wa kurithi, hauambukizwi. Kuzuia kwake ndio inatakiwa ujue vinasaba(DNA) vyenu na mwenza wako unayemtarajia kama Dokta alivyoshauri.

Wewe unaweza ukawa na chembe chembe halafu mwenza wako akawa hana, miongoni mwa watoto wako watakuwa na chembe chembe, watoto wengine hawatakuwa navyo.

Mtoto mwenye chembe chembe akija kuoa/kuolewa na mwenye chembe chembe kama yeye ndio watazaa(wajukuu wako hapa) wenye huu ugonjwa na wengine watakuwa na chembe chembe.

Kwa hiyo mzazi mmoja akiwa na chembe chembe za Selimundu ataurithisha kuanzia kwa wajukuu zenu au atarithisha hizo chembe chembe endapo mtoto wenu atapata mwenzi asiye na chembe chembe.

Kwenye Biology kidato cha 4 tulijifunza Genetics(Masuala ya kurithi), ndio ninacho kizungumza hapa

Naomba kuongeza sauti hapa📢🔔🔊🔊

Asante kwa ufafanuzi,nimekwelewa

Cc Kingsmann
 
Najaribu kuwaza mmependana na mmefikia hatua ya kutaka kuoana ili mzae watoto wenu. Mnaenda kupima mnaambiwa mna chembechembe za selimundu kwa hiyo hampaswi kuzaa.

Sijui mtaendelea na harakati za kuoana ila hamtazaa au mtapuuza ushauri wa wataalamu.
 
Back
Top Bottom