DOKEZO Daktari aliyefumua nyuzi za mgonjwa kisa hakuwa na hela ya kulipa kaletwa Hale, adhabu ya uhalifu ni kuhamishiwa kituo kipya?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Dodau

Member
Feb 26, 2024
6
7
Wakazi wa Hale tunashukuru kwa kuletewa kituo ambacho kitasaidia kwa kiasi kikubwa kusaidia wakazi wa maeneo yaliyo karibu yake.

Ila kweli Mzava, ndio tuletewe mganga (dokta) ambaye alikuwa na kesi ya ajabu ya kumfumua nyuzi mgonjwa aliyemshona kisa alikosa hela ya kumlipa kwa muda ule, maana mama wa watu alikuwa amepata ajali kule Kerenge.

Baada ya kuharibu Kerenge walimpa likizo huku akiendelea kula mshahara wake kama kawaida. Baadaye wakampa cheo kufanya kazi kule hospitali mpya na wakati wa uzinduzi kuna waliolalamika kuwa ukatili wake wa kukataa kutoa huduma kama huna hela uliendelea bila woga.

Sasa amekuja Hale wananchi watapona au wameletewa ugonjwa wa ziada?

Adhabu ya uhalifu ni kukabidhiwa kituo kipya?

Hatujasahau tunawaangalia tu.

Pia soma: Mapya yaibuka: Tukio la daktari aliyefumua mshono wa mgonjwa lilitokea mwezi Julai
 
Mpeni onyo uenda amebadilika Kawa mtu mwema,asipobadilika mchukulieni hatua
onyo alilopewa ndio kuhamishwa na kupewa kituo kipya akiongoze, angekuwa mtu wa kubadilika asingeendelea na ujinga alipopelekwa makuyuni kabla ya hale
 
Hiv sisi tunashida gani?waliosomea udaktar wapo wengi sana mtaani kwanini lazma huyo tu ahamishwe,alitakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria ili iwe fundisho Kwa wengine.Kuna viduku wamevamia sana kada ya afya sikuhizi mda wote mlegezo au visuruali modo na earphones masikioni ndiyo wanaotaka kutibu watu.
 
Wakazi wa Hale tunashukuru kwa kuletewa kituo ambacho kitasaidia kwa kiasi kikubwa kusaidia wakazi wa maeneo yaliyo karibu yake.

Ila kweli Mzava, ndio tuletewe mganga (dokta) ambaye alikuwa na kesi ya ajabu ya kumfumua nyuzi mgonjwa aliyemshona kisa alikosa hela ya kumlipa kwa muda ule, maana mama wa watu alikuwa amepata ajali kule Kerenge.

Baada ya kuharibu Kerenge walimpa likizo huku akiendelea kula mshahara wake kama kawaida. Baadaye wakampa cheo kufanya kazi kule hospitali mpya na wakati wa uzinduzi kuna waliolalamika kuwa ukatili wake wa kukataa kutoa huduma kama huna hela uliendelea bila woga.

Sasa amekuja Hale wananchi watapona au wameletewa ugonjwa wa ziada?

Adhabu ya uhalifu ni kukabidhiwa kituo kipya?

Hatujasahau tunawaangalia tu.

Pia soma: Mapya yaibuka: Tukio la daktari aliyefumua mshono wa mgonjwa lilitokea mwezi Julai
Hivi kwa nini mnachukulia poa kada ya afya?Hamjui huyo daktari naye yupo kazini?
 
Msiishie kusikitika tu. Picha yake iwekwe kwenye fremu yenye maandishi: HATARI: Dr hatari, anayefumua nyuzi za wagonjwa kama wamechelewesha malipo yuko Hale. Jina lake ni ........... Kaa naye mbali. Hiyo picha ipostiwe kila mahali kwenye wilaya alipo, na kwenye social media.
kweli mkuu
japo familia yake itaingia kwenye sonona kwa ajili ya dingi yao
 
Back
Top Bottom