Dakika moja ya ukimya kutoa heshima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dakika moja ya ukimya kutoa heshima

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by babykailama, Apr 15, 2012.

 1. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  DAKIKA MOJA YA UKIMYA KUTOA HESHIMA:A S-key:

  Chukua dakika moja, kaa kimya, weka pembeni kazi uliyotumwa /kujituma hapa JF, sahau msukumo wa itikadi yako ya sasa ya Chadema , CCM , CUF, NCCR au za vyama vinginevyo, na pia hata upendeleo wa imani ya Dini yako, kuheshimu haya maamuzi magumu yanayotakiwa kufanywa ili kuleta ushindi wa kulikomboa Taifa letu muda si mrefu ujao.


  1. Kama ushindi huu utaongozwa na Vyama Visivyotawala (siviiti vya Upinzani):
  Lazima Wanachama na Viongozi mahili wa ukweli wasio WANAFIKI wa vyama vikubwa visivyotawala ( CHADEMA, CUF na NCCR- Mageuzi) WAKUBALI KUUNGANA NA KUUNDA MTANDAO MMOJA ( hata kama inabidi kuwa chama kimoja cha siasa) na kuwa tayari kumsimamisha mtu mmoja 2015. Huyu awe ni yule atakayekuwa amekubalika machoni pa Wananchi bila kulazimisha mawazo ya mtu binafsi (iwepo Opinion Poll huru ya Kisayansi kwa muda wa mwaka mzima) tumpate huyo Mtarajiwa na Mwenza wake - atakayemfuatia mshindi kwa kura nyingi ).


  1. Kama ushindi huu utaongozwa na Chama Tawala (CCM):
  Lazima CCM igawanyike (ipasuke) sasa waziwazi (physically not ideologically) kwa Viongozi mahili na wakweli wasio WANAFIKI kutanganza kujitoa na kuunda Chama chao mf. kiitwe CCM- MAENDELEO au CCM – ASILI au CCM – HALISI na kisha wawe tayari kumsimamisha mtu mmoja 2015. Huyu awe ni yule atakayekuwa amekubalika machoni pa Wananchi bila kulazimisha mawazo ya mtu binafsi (iwepo Opinion Poll huru ya Kisayansi kwa muda wa mwaka mzima) tumpate huyo Mtarajiwa na Mwenza wake - atakayemfuatia mshindi kwa kura nyingi).


  1. Mazingira ya kufikia ushindi huu ni kuhakikisha kuwa kuna Tume ya Uchaguzi Huru (not on its ID but on its existence and operations).

  Yeyote ktk makundi mawili (A au B), atakaye anza kutekeleza kwa vitendo yanayopendekezwa hapa ndiye atatuongoza kufikia ushindi . Vinginevyo hakuna cha threads za kupasua vichwa toka JF, wala cha Migongano ya Fikra toka kwa Mwanakijiji wala Operation Sangara wala Kauli Mbiu ya Kujivua Gamba wala maandamano ya hapa na pale yaliyopenya kati mwa chujio la Taarifa za ki-Intelijensia yatakayotutoa tulipo!


  Mambo yataendelea kuwa yalivyo sasa kwa muda mrefu sana na tukiwa na bahati kizazi hiki kitashihudia Viongozi wa Chama Tawala ‘kuwahurumia ‘ Chama kitakachokuwa kinawafuatia kwa karibu katika kura kujilazimisha kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa au ya Mseto ambayo si lazima iwe na Viongozi makini bali tu ya kimpito aka ‘Funika Kombe’ ya kufurahisha wachache na kuendeleza matakwa ya wachache kama huamini rejea mahusiano ya kikazi na uhalisia wa utendaji kati ya Mugabe & Tsvangirai na kati ya Kibaki & Odinga.


  Pazeni sauti za ujumbe huu katika Mikutano Mikuu ya vyama vyenu vya siasa na Asasi zenu, sambazeni mbegu hii katika vilima, mabonde na kwenye uwanda katika kona zote za nchi.:humble:

  Shukrani kwa heshima hii, mwaweza endelea na kazi zenu.:wave:
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  A moment of silence!  Mapigo is on the menu choose one!
   
 3. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,800
  Likes Received: 17,884
  Trophy Points: 280
  For sure, i dedicate Just a Moment by Nas Escobar
   
 4. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  "For sure, i dedicate Just a Moment by Nas Escobar" :wave:
   
 5. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #5
  Apr 15, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni mtazamo tuu
   
 6. l

  liverpool2012 Senior Member

  #6
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunatakiwa kuangarilia matatizo yanayo tukabili kwanza kisha tutafute/tuangalie ni yupi ataweza kuyatatua matatizo hayo.
   
 7. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #7
  Apr 15, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  matatatizo hayatatuliwa na mtu mmoja. anatakiwa anayeweza kumobilize umma tuyatatue kwa pamoja.
   
 8. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #8
  Apr 15, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Liverpool 2012

  "Tunatakiwa kuangarilia matatizo yanayo tukabili kwanza kisha tutafute/tuangalie ni yupi ataweza kuyatatua matatizo hayo".


  Je hujajua kuwa kukosa Mkakati imara na uthubutu nalo ni tatizo linalotukabili? Undani wa Mada si nani bali njia gani, soma tena uone!
   
 9. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #9
  Apr 17, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35

  Na utashangaa kuona watu wengi wamefanya maamuzi kufuatana na mitizamo mbalimbali waliyonayo. Shukrani kwa dakika ya ukimya katika huu mtizamo !
   
Loading...