Dakika 45 ITV: Kafulila azungumzia ufisadi wa ESCROW

Dakika 45 ITV: Kafulila azungumzia ufisadi wa ESCROW

Usikose leo dakika 45 itv, Kafulila kuzungumzia ufisadi wa vigogo wa serikali kwa kushirikiana kampuni ya IPTL kupora 321 billion kwenye ESCROW akaunti.
 
Usikose leo dk 45 itv kafulila kuzungumzia ufisadi wa vigogo wa serikali kwa kushirikiana kampuni ya iptl kupora 321billion kwenye escrow akaunti

ahsante sana kwa kutujuza, nadhani tutapata mwanga kuhusu hiyo riport na hasa kama imechakachuliwa ama la
 
Kafulila apewe tuzo ya ushujaa wa kupigania maslahi ya umma bila woga wala kupepesa macho..
 
Kafulila anaelezea chanzo cha Mgogoro wa Tegeta - ESCROW.

Kafulila anaulizwa kuwa ana maslahi binafsi kwa kulizungumzi suala la Tegeta - Escrow Account??
 
Huyu Kafulila asubiri kupelekwa
lupango na kalasinga wa PAP. Siku
zake za kukaa uraiani zinahesabika
 
Usikose leo dakika 45 itv, Kafulila kuzungumzia ufisadi wa vigogo wa serikali kwa kushirikiana kampuni ya IPTL kupora 321 billion kwenye ESCROW akaunti.

Tayari yuko hewani anamwa vitu. Anasema tangu mwanzo mkataba huu ulikuwa unanuka rushwa na serikali ilijulishwa mapema ila ikaikalia.
 
Usikose leo dakika 45 itv, Kafulila kuzungumzia ufisadi wa vigogo wa serikali kwa kushirikiana kampuni ya IPTL kupora 321 billion kwenye ESCROW akaunti.

Kafulila anasema anamshukuru mungu kwamba baada ya kejeli na vitisho vingi alivyopata, hatimaye ukweli umeanza kuonekana.Na kwamba alipokuwa Israel kikazi miezi kadhaa iliyopita aliamua kwenda kufanya maombi/ ibada. Tayari ana imani na ripoti ya CAG kwani imeonyesha kwamba fedha ni za serikali.
 
Nimejifunza jambo moja la msingi sana baada ya maelezo ya kafulila. Nimeshabaini mwizi wa mikataba hii mibovu.

1994-IPTL; uchaguzi mkuu "mpya" 1995
2004-Richmond; uchaguzi mkuu "mpya" 2005
2014-Escrow Acnt; uchaguzi mkuu "mpya" 2015

Kumbe kila tukiwa na uchaguzi mkuu wa kumuingiza "mmagogoni" mpya hii kitu inatokea
Na mara zote watu wa "system" ndio wanaodili na kuficha ukweli. Kwa akili rahisi, mwizi wetu tushamjua. Ni wale wazee wa....
 
Kafulila anasema anamshukuru mungu kwamba baada ya kejeli na vitisho vingi alivyopata, hatimaye ukweli umeanza kuonekana.Na kwamba alipokuwa Israel kikazi miezi kadhaa iliyopita aliamua kwenda kufanya maombi/ ibada. Tayari ana imani na ripoti ya CAG kwani imeonyesha kwamba fedha ni za serikali.


Swali la kijinga sana .Changanya na zako . Pesa ya Umma na ni 321bn. You stuid wake up .
 
Namsikiliza hapa anaendelea kutufafanulia zaidi hili Sakata.
 
kafulila yupo hewani itv,kafulila watanzania wanakupongeza sana kaka,hakika ulionekana mzushi,ukaitwa tumbili lkn bado ulipigana na hatimae leo ni shujaa wa watanzani hongera kaka mungu wa watanzania masikini anakupigania.
 
Usikose leo dakika 45 itv, Kafulila kuzungumzia ufisadi wa vigogo wa serikali kwa kushirikiana kampuni ya IPTL kupora 321 billion kwenye ESCROW akaunti.

Kafulila ameulizwa angependa nini kifanyike? Majibu: 1. Fedha zote zirudishwe 2. Wahusika wachukuliwe hatua, ikiwemo kushtakiwa.
 
Back
Top Bottom