muuza ubuyu
JF-Expert Member
- Nov 23, 2010
- 3,543
- 3,604
Hi wana JF!
Ama kweli dunia ina mambo mengi na yaliyo mengi hatuyajui, ila sisi tu wajuvi kwa sababu ya vichache tu tuvijuavyo! Na mara nyingi dunia hii inahitaji watu werevu, makini, jasiri na wasiochoka kujifunza vitu vipya na kwa tahadhari! Na zaidi ya yote wamtambuaye/wamkirie na kumwabudu Mwenyezi Mungu bila kujali dini wala madhehebu yao!
Katika vitabu vyote vitakatifu vya dini (Biblia na Quran) kuna vitu vingi sana vimeongelewa vikiwemo uchawi na majini/mapepo, na kulingana na mada yangu ya leo ningependa kuongelea/kuulizia kuhusu majini! Mwanzo nilikuwa siamini kabisa katika uwepo wa viumbe hivi! Na katika maisha yangu ya kila siku nimekuwa mpenzi sana wa filamu na riwaya/hadithi (ref. story za Mzizi mkavu) za kutisha/za majini.
Sasa kitu kilichonifanya niandike mada/habari hii ni kisa kifuatacho. Mimi nimekuwa na urafiki na familia moja hivi for about 10 years now. Juzi nikapata taarifa kwamba binti mmoja wa pale (yupo chuo cha ualimu grade 3A anaingia mwaka wa pili) anasumbuliwa na majini yaliyotumwa na rafiki yake wanayesoma naye kuja kumuua. Jana nikawatembelea nikakuta hali ya binti yao ni nzuri lakini baada ya muda majini yale yakaingia tena, tukaendelea kuombea, awali yalikuwa mawili moja liitwalo zainabu likaanza kulalamika mwenzake makata ametoroka amerudi baharini kwani nguvu za Mungu maeneo hayo zilikuw zinayaumiza. Zainabu likatoka lakini baada ya muda makata likarudi tena linadai makata ameuawa hivyo jenyewe halitaki kumuua huyo binti kwa sababu linampenda na badala yake limekuja kumwambia aache kuwa urafiki na yule dada (wanayesoma pamoja na yule binti) na hata picha walizopiga naye azichome moto, baada ya maombezi kuzidi lile jini zainabu likatoka na binti kuwa katika hali yake kuwa ya kawaida. Wakati wote wa maombezi binti alikuwa anashindwa kutamka jina YESU, mpaka jini linapotoka ndipo anaweza! Na wakati tunaomba tunapotamka YESU majini yalikuwa yanalalamika sana tusimtaje huyo mtu kwani ananguvu sana.
Baada ya muda yule binti akawa na hali mbaya zaidi, mchungaji na mtumishi wa Mungu pamoja na sisi tukaanza maombezi na kukemea tena, bwana jini jipya likaanza kujitambulisha tena kwa hasira na ukali kwamba jenyewe ni jini mariamu limekuja kupambana na sisi kwani tumewaua watoto wake wawili yaani jini makata na zainabu! Ama kweli hali ilikuwa tete pale kwani binti alianza kutupiga kwa Ngumi na Mateke pale na tulipambana kwa hali ya juu kwani tulikuwa midume wanne pale na kijasho kilitutoka tulipokuwa tunamuweka under control kwani nguvu nyingi ilitumika!
Maombezi pale yaliendelea na hatimaye Jini mariam likatoweka na binti kurudi katika hali yake ya kawaida! Nilishangaa lakini hali ile iliyokuwa inaendelea pale nikama nacheki muvi!
Je, unajua ni mbinu gani iliyotumiwa kumwingizia majini hayo binti huyo? Katika kuyahoji majini yale yalidai binti (mgonjwa) huyo alipewa pafyumu na rafiki yake (dada aliyemtumia hayo majini) akajipulizia, mkoti na viatu! Baad ya kujipulizia, yule dada mmiliki majini aliyaagiza yamfuate binti anayenukia harufu ya pafyum yake na hapo ndipo yalivyomjua kwani yalikuwa hayamjui na hata hivyo yamehangaika sana yalipokuwa ndani ya binti huyo kwani yalikuwa yanaona binti huyo amezungukwa na watu waliovaa nguo nyeupe (which i think ni malaika) kwani yanakiri kwamba binti huyo kilichomponya ni yeye kuwa na tabia ya kusali. Na yalimuomba asije akaacha kusali katika maisha yake! kisa hiki kiliniacha katika hali tete, mawazo na nikalala kwa usingizi wa mang'amu ng'amu. Nilijaribu kuingia JF kusoma hadithi za CHAI CHUNGU na MziziMkavu na badala ya kuburudika hofu ikawa inanizidi na msisimko wa hali ya juu, kila nilipokuwa naendelea kusoma hadithi ya MziziMkavu kitu ambacho kilinifanye niache kusoma hadithi yake mpaka nimeimalizia asubuhi ya leo!
Kwa upande wa elimu ya duniani, kuna kitu wataalam wa afya wanakiita HALLUCINATION! Nahisi pia kisa hiki si cha kweli bali ni hallucinatinion! Kuna vitu viwili vinavyonifanya nihisi kuwa kweli ni hallucination ambavyo ni:
~kuna kipindi jini lilikuwa linaongea kiingereza, sasa kiingereza kilichokuwa kinaongewa ni broken ambacho kinaendana na level ya elimu ya huyo binti (form 4 Div 4 ya St. kayumba). Sasa nilitaraji kama kweli ni jini lazima lingeongea kiingereza kizuri sana!
~Pia kuna kipindi alikuwa anaongea lugha isiyojulikana na rafudhi ya kiarabu lakin katika kusikiliza kwa makini nikagundua ni maneno mawili tu ambayo alikuwa anayarudia rudia (japo kwa sasa nimeyasahau) kwa muda mrefu! Sasa kama alikuwa anaongea kitu flani kwa lugha ya kiarabu kwa nini atamke na kurudia rudia maneno mawili tuuu?
Sasa waungwana wenye uzoefu na hali hii naombeni tubadilishane mawazo kwani hali hii ikimpata mwanafamilia hali inakuwa tete, bora hivi vitu uvisome kwenye magazeti tu!
Nawasilishaaaaaaaaa!
NB: Kama hivi viumbe vipo navikemea kwa jina la YESU kristu vishindweeeeeeeeeeeeee kutusogelea tusiohusika!

Last edited by a moderator: