Dada zetu muwe makini mara tu muendapo mahospitalini


kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Messages
3,073
Likes
23
Points
135
Age
42
kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2009
3,073 23 135
Habari ya kusikitisha toka Uganda inasema kuwa daktari mmoja ambaye kwa sasa ni marehemu aaliyefariki dunia kwa UKIMWI aliacha orodha ya majina ya watu wapatao 782 ambao aliwaambukiza Virusi Vya UKIMWI (VVU).

Daktari huyo kwa jina Byarugaba alikuwa na kliniki yake katika eneo la Nakulabye mjini Kampala. Alifariki wiki iliyopita na kuzikwa katika Wilaya ya Kanungu huko Magharibi ya Uganda. Ameacha orodha hiyo aliyoiandika katika daftari ambamo aliandika majina ya watu hao pamoja na namba zao za simu.

Inasemekana kuwa aliugua UKIMWI kwa miaka mitano na kabla ya kifo chake alimfahamisha rafiki yake kuwa amewaambukiza wagonjwa wote wanawake ambao walihudhuria katika kliniki yake kwa huduma za utoaji mimba au kwa matatizo mengine yoyote ya kiafya. Pia alisema aliwaambukiza wanawake wengine katika kumbi za starehe na muziki, kwenye baa, mahotelini na katika migahawa.

Inasemekana wengine walibakwa baada ya kulazwa kwa dawa ya usingizi (Chloroform) na kwamba baadhi yao hawafahamu kama wameambukizwa VVU.

Taarifa hii inakuja wakati ambapo Serikali ya Uganda inandaa mswada utakaowaadhibu wale wote watakaogundulika ama kuthubutu kujaribu tu au kufanikiwa kitendo cha kuambukiza kwa makusudi VVU watu wengine.
 

Forum statistics

Threads 1,236,236
Members 475,029
Posts 29,250,891