Dada zangu naombeni mnishauri cha kufanya

Nduka Original

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Posts
1,012
Reaction score
817
Mimi nimeoa, yapata mwaka sasa nimekuwa na mahusiano na mdada ambae alikuwa mke wa shemeji yangu ambae familia zetu zilikuwa karibu sana. Wote tunaishi hapa hapa dar. Kwa bahati mbaya rafiki/ndugu yangu yule alifariki. Nilihusika sana katika kumuuguza mpaka mauti ilipomkuta.

Mahusiano na familia ya marehemu yaliendelea vizuri na nilijitahidi sana kutoa msaada pale ambapo niliweza. Kibaya ni kwamba tumekuja kuwa na mahusiano na kimapenzi na huyu shemeji yangu.hakika wote tunapendana sana. Mapenzi yamenoga ambapo mpaka naona ni hatari mke wangu akija kujuwa. Naomba muelewe shemeji huyu hana matatizo kwani mume kamuachia nyumba, magari kama matano ya biashara, maduka mawili hapa mjini na yeye mwenyewe pia ni msomi ana mba.

Swali: Mimi nina wazo niongee na huyu shemeji yangu tusimamishe uhusiano wetu kabla mke wangu hajafahamu. Kuna baadhi ya marafiki zangu tayari wanafahamu. Je madada zangu mnadhani huyu mama atalichukulia vipi? Au kuna approach nyingine ninaweza kuitumia?

Naomba ushauri.
 
Ushindwe kuwaza mkeo akijua atajisikiaje....how deep will you hurt her feelings...

unamuwazia huyo mwanamke....

hivi huwa mnakosa nini kwa wake zenu jamani.........
 
Hivi maswali mengine ni ya kuuliza kweli?Wewe ungefanyiwa hivo ungejisikiaje?
Ama kweli kila mtu amepewa akili lakini uwezo wa kuzitumia hizo akili ndo unatofautisha watu....Wewe ndio kati ya wale wenye akili kama za kunguni...
Kama unampenda sana kuliko mkeo kwanini usimuoe yeye?Unajiumauma!!Na nina wasiwasi vilevile njaa inakusumbua...
 
"njaa inakusumbua" ha ha ha ha ha haaaaaa dah! Ukiboreka we log in humu ha ha ha
 
Hivi maswali mengine ni ya kuuliza kweli?Wewe ungefanyiwa hivo ungejisikiaje?
Ama kweli kila mtu amepewa akili lakini uwezo wa kuzitumia hizo akili ndo unatofautisha watu....Wewe ndio kati ya wale wenye akili kama za kunguni...
Kama unampenda sana kuliko mkeo kwanini usimuoe yeye?Unajiumauma!!Na nina wasiwasi vilevile njaa inakusumbua...

yaani mi hapa ndio huwa nachoka akili na mwili aisee....

nikiwazaga kuingia kwenye ndoa halafu nisikie habari hizi roho hupatwa na baridi

nampatia picha mke wake ndo ukute ni yule Innocent/humble halafu husby ndo hivi
 
Nilijua wajutia dhambi yako na kuacha kabisa.....lakin wewe unaogopa wanadamu watasema nini????Kazi ipo sana aiseeee
 
Ushindwe kuwaza mkeo akijua atajisikiaje....how deep will you hurt her feelings...

unamuwazia huyo mwanamke....

hivi huwa mnakosa nini kwa wake zenu jamani.........
he is not serious bhana
 
Hivi maswali mengine ni ya kuuliza kweli?Wewe ungefanyiwa hivo ungejisikiaje?
Ama kweli kila mtu amepewa akili lakini uwezo wa kuzitumia hizo akili ndo unatofautisha watu....Wewe ndio kati ya wale wenye akili kama za kunguni...
Kama unampenda sana kuliko mkeo kwanini usimuoe yeye?Unajiumauma!!Na nina wasiwasi vilevile njaa inakusumbua...

Kweli mimi pia sina njaa niko vizuri kiasi, nina ka uwezo kangu kazuri tu.
 
Nilijua wajutia dhambi yako na kuacha kabisa.....lakin wewe unaogopa wanadamu watasema nini????Kazi ipo sana aiseeee

Wasi wasi wangu ni reaction yake kwahiyo natafuta soft approach for a beautiful exit
 
yaani mi hapa ndio huwa nachoka akili na mwili aisee....

nikiwazaga kuingia kwenye ndoa halafu nisikie habari hizi roho hupatwa na baridi

nampatia picha mke wake ndo ukute ni yule Innocent/humble halafu husby ndo hivi
Halafu shost we chill tu life is about taking risks...Huwezi kumdetermine huyo mwandani wake kwa matendo ya wengine...naelewa unajihadhari lakini is better being with someone than dieing lonely
 
Jamani mimi nimeshafanya makosa tayari na nina yajutia sana sana, shida yangu nahitaji approach ambayo it will not hurt this lady. ofcourse naelewa impact kama mke wangu akijuwa itakuwa mbaya sana sana
 
wewe mpaka hapo ni msaliti... acha huo mchezo mara moja.. mrudie mkeo acha mapepe.
 
Embu subiri wanaoiba waume za watu waje wakuambie.

Naomba Mungu mkeo ajue na akuache haufai kabisa hizo pesa si zingeendeleza familia yako kuwa zaidi ya mlivyo sasa.

Shame on you
 
Halafu shost we chill tu life is about taking risks...Huwezi kumdetermine huyo mwandani wake kwa matendo ya wengine...naelewa unajihadhari lakini is better being with someone than dieing lonely

sawa besti....endelea tu kunipa moyo....lem be a risk taker

ngoja niwaache uendelee kumshauri Nduka Original kuhusu soft exit/approach
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom