DADA YENU MAPENZI YAMENIKABA KOO

DADA YENU MAPENZI YAMENIKABA KOO

Dadahuyu

Member
Joined
Nov 23, 2018
Posts
9
Reaction score
29
Habari za weekend wanajamvi..

Mimi ni member mzoefu,nmeona nitumie ID mpya ili niwe huru zaidi kujielezea...nmefikwa kooni nahitaji ushauri

Mm ni mtu mwenye msimamo wa dini na nina misimamo yangu ya maisha,nashkuru Mungu nimesoma vzuri na nina kazi nzuri... (sio slay queen)..Anyways,,binafsi kwa mara ya kwanza kabisa nmeanza kujihusisha na mahusiano nilikua chuo mwaka 2 kuingia wa3...(field),,,Nilikutana na kijana na hapo ndio ilikua mwanzo wa mahusiano na mwanzo wa hata ku-kiss
Mahusiano yale yalidmu miezi kadhaa na nliyaacha baada ya kugundua yule mwanaume hakuwa wa dini yangu (alinidanganya dini)...na mm mtu wa hvo naona hatutafika mbali na mm sipendi kua na mahusiano yasio na future....uzuri ni kwamba sikusex nae

Sikujihusisha tena na mahusiano mpka nkamaliza chuo,nkawa kitaa nasaka ajira...nikakutana na mkaka wa makamo,,nikaona at least huyu age yake imeenda labda kweli anataka ku-settle down...
tulikaa kwenye mahusiano kwa muda wa miezi kama 7..huyu kaka nilimkuta na watoto wawili wa mama tofauti...mama wa mtoto wa kwanza alishaolewa,ana familia yake..mama wa mtoto wa pili walikua wameachana na huyu kaka alikataa mimba (kwamba hawakua na makubaliano ya yule dada kubeba mimba ila m.ke aliilengesha)...

Ukweli huu alinambia mwanzo kabisa akiwa ananitongoza,,basi me nkajua ntaweza yavumilia,,mahusiano yetu yalikua mazuri lakini likija swala la kuombwa mechi me nkawa nakaza..jamaa akawa ananiambia sasa tutakuaje kimahusiano kama kaka na dada?!,,,nkamwambia mm siwezi kulala na wewe... (siamini katika sex before ndoa)...akawa ananambia inabdi kwanza nizae au kama nikunioa basi niwe na mimba ila yeye hawezi uziwa mbuzi kwenye gunia...tuliendaaaaa ikafika point nkaona kabisa haya mahusiano nayalazimisha!,basi kila mtu akashika shughuli zake...

Akawa ananitafuta siku moja moja (hakutaka kuamini kweli naweza mkatalia kusex),basi tukionana hakuna jipya msimamo wangu ni ule ule..

Nkapata kazi nkapangiwa mkoa wa mbali na jamaa,,mawasiliano yetu yakaena yakawa yanafifia kabisaa..ila akawa kila akija mkoa niliopo ananitafuta (nature ya kazi yake anasafiri sana)..

Nkamwambia yaan wew siku zote huniuliziagi ila mpaka uje huku...anazuga na sababu zisizo za msingi..

Siku moja nkaona amepost picha ya mtoto (nikajua ni yule mtoto aliemkataaga),,kama vile wameelewana na yule mzazi mwenzie...basii siku aliokuja mkoa niliopo,,nkamuuliza akasema mm nmefata mtoto ila yule mwanamke sijarudiana nae...lakn yule mwanamke anacoment kabisa kwenye picha zake mara mume,mpenzi,kiboko yangu n.k....ikifika birthday ya m.ume mdada atajishughulisha cake na mazawadi kedekede...

anakuja huku nilipo anakataa hawajarudiana ila inta unaona yule mwanamke na the guy wameenda trip zanzbr na mtoto...hio siku nikanyanyua mikono juu nkasema hapa sina hata matumaini..nkawa mkali kwa jamaa nkamwambia tafadhali naomba ukija huku nilipo fanya yaliyokuleta usepe...nkawa mkali...nkafuta namba zake...akawa hata akinitext whatsapp simjibu!

sasa nkakaa kama miezi 8 au 9..nkajaribu mahusiano mengine...nafs yangu inakua ngumu kumuamini mwanaume tena!,naona uongo umezidi kiasi kwamba huyu mwanaume akanambia mm sionyeshi kumpenda na sina feelings nae (kilichoni dissapoint kwa huyu kaka ni na yeye ana watoto na hakuniambia before...)na mm nkapunguza mawasiliano na last week tukaachana kabisa..baada ya kujua ana watoto mzuka ule wa mahusiano ukafa..sitaki baby mama dramas

Nafsi yangu kusema ukweli ilimpenda sana sana sanaa huyu kaka mwengine ambae amaerudiana na baby mama wake (na hawaezi oana dini mbalimbali kabisaaaa),,...ila mwanamke sa hvi ni mjamzito anazaa mtoto mwingine baada ya miaka 8

Nafsi yangu ina maumivu makali sana jaman,nifanyaje nisahau na niweze move on?,!,yaan nmeshalia sana sana kwa Mungu wangu,kumuomba aniwezeshe nisahau jaman...

Nisaidieni wanajamvi..ni kweli kabisa siwezi pata mwanaume atakaekubali mvumilia mwanamke mpka amuoe?!,, Nahisi subira yangu ya kujitunza uanamke wangu inanishinda (Im 26 now)...,

Na pili huyu mwanaume namtoaje akilini jaman?!...

NB::: comments ntazisoma kupitia account yangu ya kawaida hapa nimemaliza...nmetumia hii ili nijimwae mwae...
 
Lazima uonje kwanza ndo ubebe mzigo. Ukioa mwanaume mwenzio je!?
 
Mmmmh mpenzi wako wa kwanza ulimpata ukiwa mwaka wa Pili....aseee dadangu utakua na Sura kama yangu.......Cha pili nakuja PM nikushauri vizuri, naomba unipokee tu.
Yaani kupitia maelezo yako naweza hata kuchora picha yako. Kiufupi wanaume wote wanaokufuata hawatumii nguvu Sana coz huwavutii kivile unless hii iwe chai.endelea kusubiri ikifika 30 akili itakuja
 
Ndiyo mapenz hayo vijana hawatak mbusi kwa gunia
Microphone test eeh
Microphone test
Unabahat hukutoa nyapu yako
Ushaur wangu usitoe nyapu kaza hivo hivo
Tulia omba Mungu atakupa
Tatizo nyie binadamu ni wabish sanaaa mnafanya mambo kwa akili zenu hautafika mbali
Yaan ww ni saiz yangu kukuoa kabsaaa kwa huo umri wako ila naogopa utaniumiza na mimi nlishasema sitak kuumiza mtu
Tulia Mungu nimwaminifu atakupa wako
Kuwa na imani dhabiti
Kwamwe usilipe kisas kwa huyo jamaa
Tulia tulia yupo wako
 
Dadahuyu Hongera sana sana kwa kujitunza na tafadhali kuwa na msimamo huo huo. Mungu anakuletea mitihani hii na ile na shetani nao anakuzengea utende dhambi kabla ya ndoa. Sasa cha kufanya ni hivi? Kwanza hao wote waliokutaka utoke nae kimapenzi kabla ya ndoa ni mafirauni tu achana nao. Kutoka kimapenzi ni kuuza utu wako Msemo huu wa kwamba kutokuuziwa mbuzi kwenye gunia ni msemo wa vijiweni tu..... na ukiona mwanaume anaunukuu huo msemo kwa ajili ya akule tu tunda mkimbie umbali mrefu maana hana mapenzi ya kweli, sisi wanaume tukigundua kuna udhaifu mdogo tu kwenye kugegeda basi demu tunamtosa na kumkibia tena kwa masimango siku ya pili tu. Dada yangu acha kuogopa maisha, usitafute mwanaume ambae amechoka (unavyowaita wame settle) tafuta hata kijana ambae ni mshika dini kama wewe walau anamiliki meza ya kuuza nyanya hata sokoni tu. Umri unakwenda na hao unaowaita walo settle wana mambo 100 kidogo, Kuna siri kidogo nyuma ya bazia ya kwanini wamama wakina mama diamond, wakina shilole na wengineo wanatafuta vijana wadogo wasio na mbele wala nyuma wengine hata kukoga tu hawajui? Katika Uislam bibi Khadija alitoa mahari kumpa Mtume Muhammad amuoe unajua ni kwanni? unajua Muhammad alikuwa na umri gani na Khadija alikuwa na umri gani wakati huo? ni funzo Mungu anatupa. Usijaribu kutafuta vilivyokwisha undwa, dada yangu pambana unda chako mwenyewee. Mungu amekuepusha na mitihani kwa hao wanaume sasa tafuta cha kwako, nenda sokoni, madukani kwa wauza mitumba na sehemu zengine, peleleza, uliza mpaka upate chako mwenyewe unakitengeneza from zero, from scratch hapo ndio utaona utamu wa ndoa.
 
Hii paragraph ya tatu kutoka chini imenitoa jasho siwezi ku-bold maandishi humu but nadhani nitakuwa nimeeleweka,kama siyo kuwa nimeshaowa basi hii ingekuwa bahati yangu nyengine.

Hakuna maisha ya ndoa ya kujiamini kama pale unapokuwa wewe ndiye umemuanza mkeo,ni muda sasa mnaotaka kuowa kuitafuta hii bahati hapa ila mwenyewe ameshasisitiza hakuna kufanya kitu hadi mmehalalisha kwa imani yenu.
 
Kwa hiyo mpaka sasa hivi hujawahi kugegedwa tangu uzaliwe?
 
Kubali hali mmeachana, kukubali hali inasaidia uambie moyo wako you and him ts over hakuna kingine pingana na akili yako na moyo wako kila linapokuja swala kuhusu yeye

Jichanganye na watu, jipende focus na maisha yako mtu sahihi atakupenda vile ulivyo usifos kitu ambacho kitakuja kukucost baadae sababu moyo na akili havitaki

Usipende kua alone muda mrefu jaribu kua na watu,jikeep busy jipe trips uifrahishe nafs najua kama mwanadam swala la mapenzi haliepukiki lakini utafika muda wake na mtu sahihi

Hold on Allah hasnt finished with you yet!
 
Inaonesha ww Mdada Ni mtu wa Zanzibar ,hii story inakuwa kama Yako wakati nipo mosomoni mwaka wa pili nikakutana na mtoto wa kiarabu Yeye alikuwa Muisalum Mm Mkristo ,Sasa Yule Mtoto wakiarabu tulianza urafiki baadaye nikantongoza mtoto kakubali ila kusex sasa mpaka sasa huyu Mtoto mkali wa kiarabu huwa anakataa kata kata wanasema ananipenda ila kusex mpaka nimuoe kwanza ,nimetongozaa ww mwaka Mzima mtoto hataki kabisa kusex ila zawadi hela alikuwa ananipa ,Sasa mm mwenyewe huwa naogopa hapo tu Kuuziwa mbuzi kwenye gunia ,Nikwambia issue ya kusex ananiambia nibadili dini alafu niandike barua kwa yuko tayari kuolewa na mm ,ila sasa issue inakuja kubadili dini na kufunga ndoa kabla ya kusex yaani hata sijampa Mimba
 
Back
Top Bottom