Dada yangu anataka tufunge ndoa

Dada yangu anataka tufunge ndoa

DITOPILE WAPILI

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2015
Posts
386
Reaction score
265
Habari zenu wanajamvi,

Nimeleta issue yangu hapa mnisaidie kunishauri.

Dada yangu binamu, mtoto wa shangazi yangu, anataka nifunge nae ndoa, yaani tuwe Mr & Mrs.

Nimejaribu kumkwepa kwa kumuwekea mitego mbalimbali kumpima kama kweli anataka tuwe wapenzi, moja ya mtego huo nilimwambia kuna rafiki yake nampenda hivyo ajenae home ili nipate mteremko wa kuongea nae, basi binamu alinitukana, akalia sana mpaka akasusa kula na kuongea na mimi. Nilichoamua ili kumpooza nikamwambia nakutania tu. Ndio akarudi kwenye hali ya kawaida.

Ugumu unakuja kwenye kufikisha ujumbe kwa wazazi wake, namwambia aongee na baba yake kama anataka kuolewa na mimi, anaogopa sababu dingi yake mtata, halafu ndio mjanja wangu hapa mjini, amenisaidia kunisomesha hadi chuo kikuu na kunisaidia kupata kazi.

Yeye anachotaka tufanye nimpe ujauzito, halafu mambo mengine mbele kwa mbele.

Kwa jinsi anavyo nijali na kunipenda, mimi mwenyewe nimeingia line, yaani network inasoma full, madave dave.

Je! Nisawa kutebmea binamu yangu?


Vipi ikijulikana mimi ndio niliempa mimba?

Ipi njia sahihi kwangu kufikisha ujumbe kwa wazee?
 
Malipo ya kusaidiwa ni kumdunga binti yake miti na mimba juu. .aisee fikilia ungekuwa ni ww...
Kimbia lana hiyo na aibu ya maisha yako yote
 
Nyie mnataka kuendekeza tu uzinzi kama mtaoana. Sidhan kama kikwenu inaruhusiwa. Na kama mshua wake ni mtata jiandae kupigwa risasi ya kalio
 
Sijajua ila kuna utani ule wa dada binam, baba yake sometimes ananita Mkwe lakini katika hali ya utani tu.
Ujajua tena? Kama linaruhusu oaneni kama haliruhusu kaa pembeni na huyo baba kwann anakuita hivo usikute anajua kinachoendelea Sema uoga wenu tu.... Nawe mtanie umsikie atasemaje
 
Aisee!
Kwahiyo unawaza kuoa dada yako si ndiyo? Haya kila la kheri.
 
Ni hivi karibuni nlikuwa mkoa wa Kagera pale, nilishuhudia ndoa ya aina hiyo hiyo unayoitaka wewe, kwangu mie ilikuwa jambo la kushangaza ila wenyeji wa kule waliliona ni jambo jema tu
 
Wela welaaaaaaaa...?
me nataka pilau tu
ndoa lini...?
 
Back
Top Bottom