Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,166
- 10,897
Ugomvi wa seneta wa Minnesota Ilham Omar mwenye asili ya kisomali na raisi Trump hauishi. Juu ya kwamba huyu dada ni mwanamke lakini tabia ya kidomodomo cha Trump ndiyo inayoendeleza ugomvi huo wa kisiasa nchini Marekani.
Juzi moja katika kampeni za uchaguzi raisi Donald Trump alifika kwenye jimbo linalowakilishwa na ilhamu Omar na ambalo lina wakazi wengi wenye asili ya Somalia.Katika kampeni zake raisi Trump alimponda Ilham Omar kwamba asiwafundishe wamarekani namna ya kuendesha nchi yao na kwamba yeye alifanya nini kule alikotokea.
Katika kujibu Ilham alisema yeye ni Mmarekani na aliingia Marekani akiwa na miaka 8 kwa hivyo popote alipokuwa asingeweza kufanya jambo, lakini yeye Trump kinyume chake sasa anaonekana kuiongoza nchi hiyo kama mtoto mwenye umri huo.