Dada wa kazi anavyosaidiwa kuwa mke bora kuliko mabinti wa bosi

Kuna mdada wa kazi nilikaa nae mpaka nikamwozesha, tulikua na undugu kwa mbalii, tangia ameolewa kila siku ni kesi kwangu maana hapa mjini mimi ndio nilikua kama mzazi wake, alibahatika akapata mume mtulivu ambae amejijenga kimaisha..ila bi dada akawa pasua kichwa hata sikutegemea maana kwangu alikua anafanta kazi vizuri na alikua mtulivu...hapa ndio nilielewa maana ya msemo maskini akipata tako hulia mbwata

Kwa kweli ndoa ilimshinda, mume alichoka, binti hafanyi chochote ndani kwake zaidi ya kukaa vibarazani maana wanapoishi wamepanga nyumba ya kushare. Mume akaona isiwe tabu akamtafutia housegirl, tobaa anapiga mahousegirl mpaka wanakimbia nyumba, nimeletewa kesi nyingi hapa, majibu ya shombo kwa mume, hafanyi chochote anadai eti sasa yeye ni bosi maisha ya kuwa housegirl yamemtoka

Nilimwita nikazungumza nae zaidi ya mara tatu, tena nikamuuliza mbele ya mumewe kama niliwahi hata kumpiga au kumuachia kazi zote mwenyewe, maana sielewi tabia ya kupiga waschana wa kazi aliipata wapi au alijisahau kwamba nae alikua mmoja wao, nilijaribu kumkumbusha vile tumekua tukiishi kwa kusaidiana kazi pale ninapokua na nafasi

Nikamuuliza ni kipi kinamfanya awekewe housegirl wakati yeye ni mama wa nyumbani na wana mtoto mmoja tu, akaomba msamaha akasema atabadilika...kumbe ndio alikuwa worse zaidi

Mwaka jana alikuja kwangu na mtoto na begi lake, namuuliza kulikoni, kumbe mume alikimbia zambia muda mrefu kimya kimya, na hajarudi tangu aondoke, kodi walipopanga iliisha kumpigia mume akamwambia jiongeze, mimi sina mpango wa kurudi, mwenye nyumba akamtimua

Alipofika kwangu mi nlichofanya ni kumpa nauli nikamwambia aende kijijini akaanze maisha maana hata ndugu wa upande wa mume walimchoka tabia zake , amechezea ndoa yake amesahau ulipotoka, sikua na msaada wowote kwake na wala sikutaka anichoshe maana nilimuonya sana, mpaka na leo amedoda kule kijinini na mtoto wake
 
" Wapumbavu wasiruhusiwe kupenda, kupendwa au kuingia ktk daraja la ndoa"
- J. Comey

Huyo dada ni mpumbavu wa dunia.
 
Ndio maana siafiki 100% kwamba housegirls anaweza kuwa mke bora...wengi ni malimbukeni wa maisha na wana upeo mdogo pia, anachofanya anapokua kazini ni kwa sababu analinda maslahi yake na si vinginevyo

Ukioa uweke ndani, utajionea maajabu
 
Nimeona house girls wasio wapumbavu wakiolewa na kutulia. Inshu ya huyo ni upumbavu tu.
 
Back
Top Bottom