Dada wa kazi anavyosaidiwa kuwa mke bora kuliko mabinti wa bosi

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,211
5,937
KAULI YA RAIS UHURU KENYATTA KWENDA KWA WAZAZI

Amesema hata kama watakasirika wakasirike lakini huu ndio ukweli wanaopaswa kuupokea.

Kumuamsha mdada wa kazi saa 11 alfajiri na kuwaacha binti zako wamelala ni kumuandaa binti wa kazi kuwa mke bora kuliko wanao.

Eti kumtumikisha dada wa kazi apige deki, apike, afue nguo, aoshe vyombo wakati wanao wanaangalia TV. Ni kumuandaa mdada wa kazi kuwa mwanamke anayewajibika kuliko wanao.

Kumuacha binti wa kazi aandae watoto kwenda shule, awaandalie uji mapema, awalishe, awasafishe wakati wanao wanacheza gemu kwenye simu au computer ni kumuandaa binti wa kazi kuwa mama na mlezi bora kwa watoto kuliko wanao.

Na kwakuwa yote hayo unayafanya kwa masimango na manyanyaso unamfanya mdada wa kazi kuwa jasiri mwenye kuzikabiri changamoto za ndoa yake kuliko wanao.

Ukimaliza kwa kusema mwanao akiwa hajui hayo yote, ndoa ikiharibika mnazungukuka kutafuta maombi kwa wachungaji kumbe ninyi mmeharibu ndoa za watoto wenu.

Msiwasumbue wachungaji.

Nimefikisha ujumbe wako mzee nami nakaza hapo hapo, msiwasumbue wachungaji.

Mwalimu Bemasha Bemastasha
 
Na bahati mbaya sasa binadamu huwa tunamfumo wa kulipisha tunapopata nafasi. Aliyeteswa nae huja kutesa wengine akipewa nafasi ya juu. Mwanafunzi wa form one huteswa anapoanza shule na watangulizi wake. Na huyachukia sana mateso hayo pia huombea itokee mamlaka flani izuie matendo hayo lakini huwa hajifunzii kwake juu ya wale watakaomkuta mwaka kesho. Wakij nae anawatesa tena. Usishangae dada wa kazi akiolewa na mwenye uwezo kama wa bos wake basi dada wa kazi nyumbani kwake anapata mateso mara mbili kiliko yeye.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndoa sio hayo ambayo mnazungumzia kuhusu hayo mambo mtoa mada anasema inasemekana hiyo ni robo tu ya ndoa kamili.

Ndoa inamambo mengi ikiwemo Upendo, Uaminifu, Msiri, Kujali

Kumsaidia mme wako kwa ushauri na kumliwaza akiwa katika stress hizi za maisha mwanamume anatakiwa afanyiwe mambo mengi ikiwemo kudekezwa pia.

Ili hali wewe unaona ni mwanaume tu anatakiwa afanyiwe hata mwanamke anatakiwa hayo afanyiwe na yote hayo kichwa ni upendo uolewe au uoe chaguo lako wote kuridhiana mtaeza kufanyiwa kila kitu ila kama hamna upendo si kitu.

So kupika kufua kwanza kuna mashine na mengine mtaeza kujifunza ila kama ila tabia njema huwezi kujifunza wala ni kitu ambacho unacho ambacho kinakutambulisha.

So wadada wakazi sio watakuzibia watoto wako riziki wala kila mtu anafungu lake duniani tabia njema ndio key ufunguo wa maisha jinsi unavyoishi na watu ndio asilimia ya mazuri yako unapata.
 
Na bahati mbaya sasa binadamu huwa tunamfumo wa kulipisha tunapopata nafasi. Aliyeteswa nae huja kutesa wengine akipewa nafasi ya juu. Mwanafunzi wa form one huteswa anapoanza shule na watangulizi wake. Na huyachukia sana mateso hayo pia huombea itokee mamlaka flani izuie matendo hayo lakini huwa hajifunzii kwake juu ya wale watakaomkuta mwaka kesho. Wakij nae anawatesa tena. Usishangae dada wa kazi akiolewa na mwenye uwezo kama wa bos wake basi dada wa kazi nyumbani kwake anapata mateso mara mbili kiliko yeye.

Sent using Jamii Forums mobile app
kweli kabisa
 
Mama Greener wa Mabibo -, alikuwa house girl mbona ametunza ndoa yake vizuri? ila ana mdomo? heee! chiriku akasome! utadhani karogwa!!
 
Back
Top Bottom