Dada, umri ndo mtaji wa ndoa yako acha kuwa 'selective'

Dada, umri ndo mtaji wa ndoa yako acha kuwa 'selective'

Pure_sapiens

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2016
Posts
2,251
Reaction score
2,131
Habari zenu ndugu jamaa na marafiki natumaini nyote ni wazima wa afya,

Kumekuwa na kauli mbalimbali zikijaribu kueleza kuhusu sekta hii ya ndoa na mimi leo nitaeleza japo kwa uchache nitatumia kisa cha kweli.

Siku moja mwanafunzi XY alimfuata mwalimu wa mahusiano na ndoa kwa ajili ya kumuliza swali lililosumbuwa kichwa chake. Alivyomkuta mwalimu ofisini alisalimia na kuuliza swali lake.

XY aliuliza"Mwalimu kuna tofauti gani kati ya mahusiano na ndoa"?
Mwalimu" akamwambia kabla sijakupa majibu nikupe kazi ya kufanya alafu nitakupa tofauti zake. Mwalimu akamwambia mwanafunzi nenda katika shamba la shule la mahindi kaniletee mche wa mhindi mkubwa kuliko wote lakini usirudi nyuma unapotafuta mche huo.

Mwanafunzi akaenda shambani kutafuta mche huo.Alipofika tuta la kwanza alikuta miche mikubwa alipotaka kuchukuwa akasema ngoja labda mikubwa zaidi ipo matuta ya mbele. Alifika tuta la pili, tatu, nne, tano lakini kila alipotaka kuchumu mche huo alisita na kujisemea labda mbele zaidi nitakuta mkubwa zaidi. Kutahamaki amefika mwisho wa shamba bila kupata mche alioagizwa na mwalimu wake.

XY akarudi kwa mwalimu wake bila kuwa na muhindi, mwalimu akamuliza mbona umekuja bila nilichokuagiza, mwanafunzi akamwambia nimezunguka shamba zima nimekosa.

Basi mwalimu akampa mtihani mwingine akamwambia" nenda katika shamba la miwa kanichagulie mti mkubwa kuliko wote shambani alafu uniletee.

Mwanafunzi XY akaondoka huku akisema sitafanya makosa kama ya awali. Alipofika shambani katika tuta la kwanza aliona mche mkubwa alikata na kupeleka kwa mwalimu haraka. Alipomkabidhi, Mwalimu akahoji mbona safari hii hukuchelewa na umekuja na mche.

Mwanafunzi XY akasema nilijifunza kupitia makosa ya Mara kwanza. Mwalimu akamwambia hiyo ndo tofauti kati ya mahusiano na ndoa. Kuwa kipindi cha mahusiano mwanamke anachaguwa sana bila kuzingatia umri akitahamaki umri umeenda anatamani kuwarudia aliowakata lakini wakati si rafiki tena kwake.

Ndoa, mwanamke analiyetayari kwa ajili ya ndoa basi atajiandalia mazingira ya kuwa tayari kama akitokea mwenye nia ya dhati basi hatokuwa na machaguo lukuki. Dada zangu kama unatarajia ndoa basi umri ndo nauli ya kukufikisha unapokwenda.

Naomba kuwasilisha

great thinker
 
Watakuja kusema kuolewa sio lazima washazoea usingle maza.

Sent From Guest House
 
madada msioolewa msijali mimi mwenyewe sijaoa bado
 
NAONA MADA ZA WADADA KUOLEWA VS UMRI ZIMEJAA SKU HZ, NI WAZI KUNA TATIZO.
 
Kabisa
Mwanamke hana uchaguzi wa umri katika kuolewa, tatizo ni jamii masikini zinazoamini Mwanamke akifika umri wa kuolewa lakini hajaolewa basi ana matatizo, kumbe wengine ndio maisha waliyoyachagua.

Kuolewa siku hizi sio ishu sana na sio lazima.
Kama una Dada halafu hajaolewa muulize atakupa mrejesho
Kitu chema kwa muda muafaka...


great thinker
 
Wadada punguzeni kukataa kuolewa mnawafanya watu waumize vichwa jinsi ya kufikisha ujumbe...na nyie wanaume tafuteni ela utaoa umtakaye..jiwekini kama wanaume sio wavulana,maana mada za kushauri wadada zimezidi.
 
Wadada punguzeni kukataa kuolewa mnawafanya watu waumize vichwa jinsi ya kufikisha ujumbe...na nyie wanaume tafuteni ela utaoa umtakaye..jiwekini kama wanaume sio wavulana,maana mada za kushauri wadada zimezidi.
Gwangala nini??
 
AISEE...KAMA HUMU NDANI KUNA MDADA FULANI AMEANZISHA NYUZI NYINGI KWELI KWA AJILI YA KUTAFUTA MCHUMBA HADI LEO HAJAPATA...SASA SIJUI NI NUKSI AU NI KUWA SELECTIVE SANA

Sent from my iPhone 5s using Tapatalk
 
AISEE...KAMA HUMU NDANI KUNA MDADA FULANI AMEANZISHA NYUZI NYINGI KWELI KWA AJILI YA KUTAFUTA MCHUMBA HADI LEO HAJAPATA...SASA SIJUI NI NUKSI AU NI KUWA SELECTIVE SANA

Sent from my iPhone 5s using Tapatalk
Yupi Huyo
 
Back
Top Bottom