Dada tuliekutana Mwenge please nitafute

Dada tuliekutana Mwenge please nitafute

Wiki iliyopita nilikuwa kwenye daladala za makumbusho nawasiliano tukawa tumekaa na dada mmoja hivi jina aliniambia anaitwa Cathy

Huyu dada cathy sio siri alikuwa mzuri sana na nilijiapiza japo si kawaida yangu kuomba namba kwenye usafiri wa uma lakini kwa huyu nilisema lazima nijitoe ufahamu nichukue

Tukiwa tunatoka mawasiliano nikamuuliza anashukia wapi akasema mpakani nikaona ni kipande kidogo sana hivyo nikajitahidi kujipigisha stori chache ili anipatie namba na kweli mpaka kufika mpakani alikuwa kashanichorea namba na nikaipiga ikaita kwake nikawa na uhakika then yeye akashuka

Ile nimetoka mpakani kuelekea mwenge mataa nikiwa nafurahaa kusave namba ya mtoto cathy alipita jamaa mmoja na boda boda akaikwapua simu yangu na kupotea nayo mazima kiukweli maumivu yalikuwa makubwa sana si kwaajili ya simu yangu ila ile namba muhimu niliyopewa na Cathy

Tumaini pekee lilikowa limebaki ni kurenew namba labda mtoto Cathy atanitafuta leo ni siku ya tatu toka nirenew napigiwa na wengi ila sijaona simu ya huyu mtoto kuingia sasa sijui anasubiri nianze mimi kumtafuta au alijaribu akaona sipatikani

Naomba nikuombe Cathy kama upo humu na unausoma uzi huu kama namba yangu bado unayo nitafute leo kabla ya pasaka utafurahi sana au kama uliifuta namba kwa bahati mbaya njoo pm fasta leo ule pasaka utakayoikumbuka maisha yako yote

Halafu ni kama bahati mimi si mtu wa daladala nimeacha kutumia daladala toka mwaka 2014 gari yangu ilipata matatizo kuna dogo huwa namtuma sana kunichukulia baadhi ya vitu aliligongesha hivyo ile siku tunakutana Cathy nilikuwa naenda shughulikia suala hilo

Ila wakuu nimejifunza kitu nilikuwa nadharau sana hizi daladala kumbe kuna wadada wazuri wengi wanatumia huu usafiri tujitahidi kuwapunguza huko kama una kiuwezo hata IST sio mbaya kwa mtoto

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo lako inaonyesha hujiamini Mkuu ndio maana hata kwenye posti yako hapa umetafuta huruma za huyo mrembo kwa kujimwambafai Sana.
Siku hizi hizo gear warembo hawazipendi kabisa kwa sababu wengi tunawadanganya uhalisia wetu then wanakuja kushtuka when is too late.
 
Labda kama ulikuwa unatumia kitochi, ilà kama ilikuwa android/iOS, unapotezaje contacts wakati namba zinaseviwa huko Google account. Ukinunua dimu mpya na ku-register Google account kila kitu kinarudi na majina yote, drive indkuletea picha zote nk.

Upo dunia ipi mkuu!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom