Dada poa alivyotaka nigeukia fisi guest

Dada poa alivyotaka nigeukia fisi guest

Ndenji five

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2021
Posts
1,985
Reaction score
3,125
Sijui nianzie wapi kuelezea kwa kisa kilichonipata .

Ila nimeona leo ni share kisa kimoja kilichowahi nikuta 2019 nipo kwenye harakati za uchimbaji na usafirishaji wa madini

Ilikuwa Mida flani hivi ya jioni mara baada ya kupata madini kwenye migodi tukiwa tumemaliza kazi na kuelekea kuyauza

Siku hiyo jamaa yangu akaniambia kwa kuwa leo pesa IPo ya kutosha na isitoshe ni wikiendi unaonaje tukàenda kutafuta sehem tukale Bata Nikamwambia sawa tufanye hivyo tukakodi ndinga letu baada ya masaa kama mawili tukawa tumefika sehem husika,

Kabla ya yote tukaenda kutafuta chumba maana ilikuwa Mida ya saa mbili hivi usiku, basi tukafanikisha kupata ila kila mmoja alichukua guest yake, sio chumba ni guest yake

Tulivyokamilisha zoezi hilo tukaoga zetu maji na kwenda kuanza kula bata, ndio siku ya kwanza naanza kunywa bia ila
Jamaa yangu akaagiza kama kret 20 na kumwambia mmiliki wa bar naomba nitolee wateja wote wa kiume niachie wa kike kweli jamaa akafanya hivyo, Si unajua mbele ya pesa hakishindikani kitu, kuja kupiga hesabu wamebaki kama warembo 17,

Jamaa akawaambia leo tutakunywa na mimi na kulala na mimi kila kitu nitalipia akaenda tena alikochuku akalipa guest mzima, na kurudi pale kuniambia My friend leo ndio siku yangu ya kuuaga umaskini,

Kwa hiyo nakuomba kwanza uniache kidogo,kiufupi alikuwa anamaanisha niondoke nimuache na wale wanawake

Kwakuwa pesa tuligawana sawa na kila mmoja anazo haikuwa kesi nikaamua kumuacha na kwenda kutafuta bar nyingine kuangalia saa ni saa tano ndio kwanza kunapambazuka

Kwa kuwa ilikuwa mara yangu ya kwanza kunywa vileo nikajikuta baada ya dakika kadhaa pombe imeanza kufanya kazi,nikainuka nilipo kaa, Ee bwana ee nikakuta kama miguu yangu imefungiwa shokapu ile natembea inanesa nesa, Nikasema Mungu wangu kumbe pombe ndivyo ilivyo gafla nikajikuta ninajiamini hakuna mfano

Yaani mimi ni mimi kwa muda ule, kucheki tuviela twangu nina kama milion 25 hiyo ni ya kulia Bata tu tena kwa siku mbili hata ikiisha sio kesi mana hom nilituma ndugu niliwasaidia kilichobaki kikawa ndio hicho na isitoshe mgodi wetu ndio kwanza unatema mawe/madini

Swali likawa kichwani namalizaje haka kahela ikiwa starehe zenyewe sizioni na sio mwenyeji kivile yaani sio mtu wa madem wala pombe kivile kama jamaa yangu nikasema hapana hapa nikujifunza tu hata wenzangu walianza hivihivi nikaenda guest niliko kikodi chumba nikamuuliza muhudumu humu ndani kuna wateja wa ngapi?

Akanipa hesabu nikasema warudishie hela zao wahame humu ndani mana nina stress nataka nipumzike mwenye, nitalipa mara mbili

kweli akafanya vile,nikamlipa pesa yake,nikamwambia nitafutie vijana Akawatafuta nikawaambia kusanyeni godoro zote wekeni chumbani kwangu nikawakesh laki kila mmoja alafu nikamwambia muhudumu nitafutie watu kama sita wanilinde huko nje wakatafutwa "magwanda"nazan naeleweka usie elewa kuna kambi ndani ya huo huo mji ya hao jamaa, chezea hela,

Basi nikamuomba jamaa anitafutie mwanamke mrembo kushinda wote pale kwenye mtaa sio siri ule mtaa ulijaa watu wenyewe fedha tena pesa mtu kukàa na m200 ndani kawaida msije mkasema ni Tanzania nooo ni huko kwa jirani Si mnajua tulilijua hilo tokea mwanzo ila tukasema siku tukizipata tutakuja hapa kufurahia mji.

Basi nikatafutiwa binti nikaletewa nikamtia kama laki unusu maana kulala na binti hadi asubuhi ilikuwa elfu 50000 mi nikampa hiyo pesa ila akili yangu ikawa na ukomo wa matumizi nikasema ikifika milion kumi ndio mwisho wa matumizi yaani nilijiwekea ukomo na ile pesa sikuiweka mle guest niliiweka kwa jamaa ambae ni mtu wa kununua madini.

Basi nilivyo mlipa yule binti nikaenda kuoga maji ndani humo humo, ile kuoga maji pombe zikapungua ila binti alijuaga nimelewa nikaja moja kwa moja kulala nimepiga usingizi nisikumbuke kama nimemlipa binti pesa inabidi nimshughulikie, Nipo usingizini tena ule mzito nikaanza kuota mambo ya ajabu pembeni akiwa yule binti nikajikuta nimebanwa ile hata kuamka siwezi, jalibu kila namna wapi
emoji20.png
emoji20.png


Nikajikuta naanza kutaja marehemu wote , babu uliko huko unisaidie nakufa, mimi tena hapa ni ugenini angalau uniokoe nikawaonyeshe pesa zangu familia yangu, nakuta wapi kitu kimenikaba ile ile nikaomba Mungu katika jina la yesu

Lakini wapi mazingira ya ndani nayaona macho yangu yanaona na binti yuko pembeni yuko na usingizi, Ila mimi hata kusogeza kidole kumshika siwezi wakuu nilitaabika sana mara kwa ghafla taa ndani zikazimwa baada ya dakika sita kuna kitu kimeingia kwa ukuta alafu ndani mwanga ukawa mkubwa

Ila sio wa taa za umeme kumbuka macho yanaona ila nguvu ya kutoka nilipo sina, yule mtu sikuweza kuiona sura yake, akawa ameingia kimiujiza ndani ya mwili wa binti,,(utajiuliza nilijuaje kama kaingia kwenye mwili wa bint usijali utajua nilijuaje)

Nikasema Dah sasa kifo hikoo kinanijia maana sina cha kufanya nikatulia tuli kiasi kwamba hata kuliwa ilikuwa naliwa kilaini bila bughuza.

wakuu sikuwai kuamini haya mambo, ilaa nakuta mara Shaaa nimezungukwa na team ya viumbe nisio waelewa kama wa nne ivi, Nikajioji wametokea wapi maana mlango niliufungua kwa ndani funguo nilificha kwenye mto nilio ulalia si unajua mabinti hawaeleweki unakuta.

unampelekea moto ameshindwa kuhimili unakuta kakimbia au kakupaka madawa ya kukulaza.
 
Nimekumbuka kumbe ni wewe na jamaa yako ndio mlisababisha tutimuliwe bar 🤔🤔
Sijui nianzie wapi kuelezea kwa kisa kilichonipata .

Ila nimeona leo ni share kisa kimoja kilichowahi nikuta 2019 nipo kwenye harakati za uchimbaji na usafirishaji wa madini

Ilikuwa Mida flani hivi ya jioni mara baada ya kupata madini kwenye migodi tukiwa tumemaliza kazi na kuelekea kuyauza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom