Samawia
JF-Expert Member
- Dec 6, 2017
- 594
- 458
Nafahamu Shemeji yangu anakupenda sana,kwa uliyomfanyia angekuwa mwanaume mwingine sidhani kama angeendelea kuishi na wewe, mwanaume gani utakaye muacha ukiwa Mzima wa afya miaka kadhaa baadae urudi ukiwa umeathirika akupokee!kakupokea mnaishi vizuri,shemeji hajali hali uliyonayo ,anakutunza vizuri kiasi kwamba ni vigumu kukutambua kuwa ni HIV +,kajivalisha mabomu shemeji yetu kwa ajili yako ,wengi tulitarajia utatulia lakini imekuwa tofauti na matarajio yetu, tunakuona bado unaendelea na uchafu wako, miaka yote uliyokuwa umeajiachia umepata faida gani zaidi ya hilo gonjwa? Hata Kama unajua mumeo zuzu wewe sio wa kumfanyia hivyo unatakiwa utulie, ukija kumwagwa usitarajie kumpata mwanaume mwingine atakaye kujali kama huyu shemeji yetu,hata hao wanaokuona wa maana leo watakukimbia,na unaweza usimpate hata wa kutokukujali ukaishia kuzurura zurura na kudakadaka hao waume za watu,yana mwisho hayo hata kama mganga wako kakuhakikishia huwezi kuachwa.