Dada muonee huruma shemeji

Samawia

JF-Expert Member
Dec 6, 2017
495
500
Nafahamu Shemeji yangu anakupenda sana,kwa uliyomfanyia angekuwa mwanaume mwingine sidhani kama angeendelea kuishi na wewe, mwanaume gani utakaye muacha ukiwa Mzima wa afya miaka kadhaa baadae urudi ukiwa umeathirika akupokee!kakupokea mnaishi vizuri,shemeji hajali hali uliyonayo ,anakutunza vizuri kiasi kwamba ni vigumu kukutambua kuwa ni HIV +,kajivalisha mabomu shemeji yetu kwa ajili yako ,wengi tulitarajia utatulia lakini imekuwa tofauti na matarajio yetu, tunakuona bado unaendelea na uchafu wako, miaka yote uliyokuwa umeajiachia umepata faida gani zaidi ya hilo gonjwa? Hata Kama unajua mumeo zuzu wewe sio wa kumfanyia hivyo unatakiwa utulie, ukija kumwagwa usitarajie kumpata mwanaume mwingine atakaye kujali kama huyu shemeji yetu,hata hao wanaokuona wa maana leo watakukimbia,na unaweza usimpate hata wa kutokukujali ukaishia kuzurura zurura na kudakadaka hao waume za watu,yana mwisho hayo hata kama mganga wako kakuhakikishia huwezi kuachwa.
 

mbere

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
6,906
2,000
Ni nani humu niambie kuna limoja nalizingia humu isije ikawa dadako aniachie upupu mimi
 

Shadeeya

JF-Expert Member
Mar 12, 2014
40,362
2,000
Aisee huyo shemeji yako sio wa anga hii. Na hayo yake ni yale mahaba niue.

Ila yote kwa yote kama ni kweli huyo dada yako anahitaji washauri aisee sababu sio kwamba anamkomoa shemeji yako pekee bali na yeye pia anaidhohofisha afya yake kwa ngono za mara kwa mara tena na huku anao mmh.
 

Sent Kb

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
4,653
2,000
Kamkanye huyo shemeji yako pia ongea na kaka yako kuhusu huyo shemeji.

Pia acha kuingilia ndoa ya ndugu yako.. Pambana na hali yako.
 

Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
8,335
2,000
Tabia yake hiyo, kama dada yenu hamkurekebisha akiwa msichana sasa hivi atawezekana?
 

Al-Watan

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
11,921
2,000
Kamkanye huyo shemeji yako pia ongea na kaka yako kuhusu huyo shemeji.

Pia acha kuingilia ndoa ya ndugu yako.. Pambana na hali yako.
Hawa dada wengine utafikiriwanatakakuolewa waona kaka zao.

Mtukaka yako ana matatizokwenye ndoa yake, badala ya kufanya vikao vya familia myamalize katikafamilia, unaleta JF.

Kama si umbea ni nini?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom