Dada kama huolewi mlozi/mchawi wako huyu hapa..!

bigmind

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
12,457
12,668
Binafsi nitangaze interest kuwa sijaoa, lakini pia nitoe angalizo kuwa situmii bandiko hili kujitangaza ingawa pia azuiliwi mtu (mdada) kujaribu "never know, it might be you...!

Anyway tuache hizo taralila za hapo juu, twende kwenye moyo wa mada, tuidadafue kidogo madada yetu.

Nawaomba mniazime masiko yenu na twende wote sako kwa bako mpaka mwisho mada..!

Binafsi naongea haya, kutokana uzoefu wangu wa kimtaa, maana kuna msemo mmoja kuwa "" EXPERIENCE IS A GOOD TEACHER"" ukimanisha uzoefu ni mwalimu mzuri. Sasahivi ukipita mtaani, makanisani, makazini, misikitini wadada wengi wanahaha kutafuta watu(wanaume) wa kuwaoa,nasema haya kwa nia njema tu..! Sasa huwa najiuliza mbona hili tatizo linakuwa kubwa na hasa mjini vijijini lipo ila siyo kubwa sana kama ilivyo mjini.

Katika tafiti zangu (simple survey) nilizofanya nimegundua mambo yafuatayo yanayopelekea shida hii ya wadada wengi kukosa watu wa kuwaoa:-

Mosi wadada/wasichana wengi siyo watu wa timing, ninachomanisha hapa ni kwamba katika maisha huwa kuna timing ya kufanya mambo, mfano muda mzuri kwa mdada kuolewa ni kati ya umri wa miaka 20-25, sasa wapo wadada wasiyo lijua hili. Kuanzia miaka 16 mpk 25, ni muda ambao mdada huwa kileleni huvutia na kupendeza sana na nikatika kipindi hiki huwavutia wanaume wengi, hivyo ni fursa nzuri kwa mdada kuolewa ingawa wengi huwa hawatambui hili na hujikuta wamepitiliza kwenda miaka 30, hapa huwa shida sana.

Wanawake wengi, hawajui kupanga machaguo yao, hapa namanisha kama ni msichana uweke mapema chaguo/aina ya mwanaume unayemtaka vipo vigezo vingi sana na kila mtu anavyo vyake, kwa mdada usipofanya chaguo hutajikuta kila mwanaume hakufai huku umri unakwenda kuja kustuka unawahitaji walewale wanaume uliowakataa ndiyo sahihi ila sasa inakuwa too late muda huo.

Wadda wengi hawajui hadhi(status) zao, unakuta mdada asiyejitambua hujitesa miaka nenda miaka rudi kujishebedua kuwapenda wanaume wasio fiti katika status zao na mwisho wake huwa ni kuliwa na kuachwa huku wakibaki wakilia na kutafuta mchawi.

Wadada wengi siyo wao ni bali ni fake (they are not real). Lipo suala wadada wengi hasa maeneo ya mijini wamekuwa fake kuanzia miili yao, muonekano wao, na tabia zao na mitazamo yao ni fake tuu..! Sasa wanaume walio wengi wanakwazwa na hii tabia, wanapokuja kugundua kuwa siyo wewe jibu ni kutimua mbio hakuna lingine huku mkibaki na vilio.

Uelewa mdogo/mtazamo hasi juu ya mafanikio ya familia, wadada wengi wako mawindoni kutafuta wanaume waliofanikiwa tayari(successful man), wanasahau kuwa pia wao wanapaswa kuwa sehemu ya mafanikio hayo. Kuna msemo mmoja kuwa " kwa kila mwanaume aliyefanikiwa nyuma yake kuna mwanamke/mdada" hili somo kamwe haliwaingii wanawake wameamua kuziba masikio na mwisho wameambulia kunyanyaswa katika mahusiano na wanapobahatika kuolewa ndoa huwa ya moto na haikaliki.

Mitandao ya simu, kama kuna kitu kina mkera mwanaume ni kuwa na girl friend/mke mwenye alosto (uteja/uraibu) wa mitandao ya kijamii, sisemi kutumia mitandao ni kitu kibaya ila ukisha kuwa teja wa mitandao kwa mwanamke unaboa kuliko unafikiria, kwanza ni chanzo cha uvivu, umbea, umaskini na hukwamisha uwezo wa kufikiri pale mitandao inapotumika vibaya. Wazungu wanasema "time is money/time time is precious" wakimanisha kuwa muda ni utajidili mitandao ya kijamii ni chanzo kikubwa cha upotevu wa muda (tatizo hili liko mjini).

Yote kwa yote wadada wengi hawaamini kuwa mume bora hutoka kwa Mungu, sasa hivi wanaamini mwanaume anapatikana sehemu yeyote hasa mitandaoni. Ukweli ni kwamba BUZI BORA anatoka mtandaoni ila MUME BORA hutampata popote isipokuwa kwa MUNGU TU.

USHAURI WANGU

Nimeongea kwa uzoefu/experience yangu ya mtaani, ila habari nzuri ni kuwa siyo kweli kuwa wanawake ni wengi kuliko wanaume, takwimu zinasoma na kuonesha hivyo kwa wanawake wanaozaliwa mahospitalini ila pia mortality rate, mila na desturi km (polygamy kwa waislamu na traditionalist) na factor nyinginezo bado zinafanya kazi kubalance hii tofauti ndogo hii ya takwimu hii. Kwa uzoefu wa hapa JF kwenye jukwaa la MMU (love connect) bandiko za wanaume kutafuta wenza ni nyingi kuliko za wadada (not justify the truth).

Naomba niwaseme kidogo kuhusu sisi wanaume ili kubalance, ni lazima na sisi pia tujue kuwa mke mzuri licha kuwa hutoka kwa Mungu ila tunalojukumu la kumtengeneza kwa kumushape mke unayemtaka.

Asanteni sana..!

Imeandaliwa na;
Rise Africa co.Ltd.
Business services and social consultant.
 
Na mchawi wa akina kaka wasiooa ni nani

Sent from my TECNO-J7 using JamiiForums mobile app
 
kwa kweli mwanamke yupo busy na simu muda wote halafu hela ya vocha anaomba wanakera sana

mwanamke kuwa karibu mitandao yote ya kijamii huku ukiniambia nipo peke yangu tambua kwamba najua unanidanganya
 
kwa kweli mwanamke yupo busy na simu muda wote halafu hela ya vocha anaomba wanakera sana

mwanamke kuwa karibu mitandao yote ya kijamii huku ukiniambia nipo peke yangu tambua kwamba najua unanidanganya
Ndiyo hapo sasa..! Hawapendi ukweli huu..!
 
Mwanamke yupo, Inst,Fb Tango ,Viber na kadhalika na hana biashara yyt anayoifanya humo halafu kutwa nzima yumo humo kwakweli mwanamke wa aina hii ni Bomu zaidi ya Bomu la nyukilia

Send from Buja
Hapo sasa!
 
Ni mhimu sana! Shida huyo mwanamke anashapika...??

Wengine ukimwambia anapensa uwe hivi wanaleta feminism..

Hili la feminism ndio poison inayowatafuna dada zetu taratibu bila wao kujua! BTW ni somo zuri sana kwa dada zetu! hasa hii ishu ya timing
 
Aaah we waache tu.
Kuna manzi mmoja mzuri kweli juzi kaniambia

" yani Senior Boss ki ukweli im not happy wit my love life....kila siku nakua mtu wa kuachwa bila sabab.....Its really pain me " ( U can imagine her accent )

Katika kukaa nae huyu manzi nimekuja note ni mtu flan hajui kujiongeza kabisa....fursa anazo nyingi wako vizuri sana kwao ila hata siku moja hajawahi niuliza hata michakato ya kutafta hela ni ile kijuu juu tu...ingawa ana manage issue zao...she z all about spending and having fun...sio mtu wa kuumiza kichwa (think tank/business explorer).....sumtyms she isnt efficient with resources ila cz ni rafiki yangu huwa namuelezaga ukweli tu at tyms.

Some women really need to change...There is something more than just beauty and good character that draws a man to a woman. (Excuse my long post)
 
Aaah we waache tu.
Kuna manzi mmoja mzuri kweli juzi kaniambia

" yani Senior Boss ki ukweli im not happy wit my love life....kila siku nakua mtu wa kuachwa bila sabab.....Its really pain me " ( U can imagine her accent )

Katika kukaa nae huyu manzi nimekuja note ni mtu flan hajui kujiongeza kabisa....fursa anazo nyingi wako vizuri sana kwao ila hata siku moja hajawahi niuliza hata michakato ya kutafta hela ni ile kijuu juu tu...ingawa ana manage issue zao...she z all about spending and having fun...sio mtu wa kuumiza kichwa (think tank/business explorer).....sumtyms she isnt efficient with resources ila cz ni rafiki yangu huwa namuelezaga ukweli tu at tyms.

Some women really need to change...There is something more than just beauty and good character that draws a man to a woman. (Excuse my long post)
Sure 100%...!

Girls' beautifulness must be in and out..! Being with good looking/standing doesn't grantee her a good and character man but brain smartness can..!

Ataolewa atakayejitambua, wapuuzi wataishia kupiga domo humu tuuh..!
 
Ukumbafu huu badala nishape shilingi nikae kushape mdada alieshindikana kwao mpaka JF anaijuwa ? wacha nisioe
 
Back
Top Bottom