Dada Juliana Shonza fikisha ushauri huu wizarani kwako

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,488
13,608
Pole na kazi mheshimiwa naibu waziri mwenye dhamana ya michezo na masuala ya utamaduni.

Dada Juliana Shonza nimefanikiwa kuiona video ndogo yenye kuwaongelea mawaziri na manaibu ambao ni vijana, waliopo kwenye baraza kwa sasa. Wewe ni mmojawapo.

Video hiyo (clip) inaonyesha kuwa umezaliwa mwaka 1987, yaani mwaka huu umetimiza umri wa miaka 30, bado kijana mbichi kabisa.

Ni bahati iliyoje kwako kupewa dhamana ya unaibu waziri ukiwa na umri mdogo, natumaini Mungu atakuongoza na utatumia vyema maarifa uliyonayo kwa faida ya Tanzania.

Naomba nikushauri suala moja muhimu sana kwenye uendelezaji wa michezo kwa ujumla

UMUHIMU WA USIMAMIAJI WA TAALUMA ZA WAFUNDISHAJI WA MICHEZO NCHINI.

Mheshimiwa Shonza kwa taarifa yako ni kwamba majirani zetu Uganda wamekuwa katika kiwango kizuri cha soka, timu yao ya taifa imepambana vilivyo katika kutafuta nafasi ya kwenda Russia mwakani kushiriki kombe la dunia lakini kwa bahati mbaya wameshindwa, na Misri ndio wamefanikiwa. Uganda ni nchi ambayo ipo imara kimichezo kuliko sisi, na sababu haswa ni kusimamia katika weledi wa wafundishaji wa michezo katika ngazi za mashule na vyuo.
Pamoja na kufanikiwa kwao katika malezi bora ya wanamichezo, waganda wamefikia hatua ya kumwomba kocha wa zamani wa Zambia Kalusha Bwalya aende akawape ushauri wa namna ya kumpata kocha bora wa timu ya Taifa.

Waganda wanao walimu wazuri wa michezo, lakini bado kwao wameona ni muhimu kutafuta ushauri wa Kalusha Bwalya. Ifike mahali na sisi watanzania tusiridhike tu kuwa na bora waalimu wa michezo bali tuwe na waalimu bora.

Ifike mahali tuwe wepesi wa kutafuta kilicho bora zaidi kwa maana ya mafanikio kitaaluma na sio kwa kubwetekea tukiamini katika kile tunachokifahamu pasipo kuongeza ubora wa taaluma za waalimu wa michezo. Dada Shonza nakushauri tu, usikubaliane na hizi siasa za wizara yako kuwa wafunguaji na wafungaji wa semina za ukufunzi wa michezo, nenda hatua moja zaidi katika kuweka mkakati wa kupima matokeo ya kazi za hao wakufunzi kila mwaka.

Inaweza ikawa ni business as usual kwa makocha kupewa semina mbalimbali halafu ubunifu wao ukashindwa kuonekana. Timu zetu za taifa zinakuwa kwenye viwango duni kwa sababu changamoto ya ufundishaji wa waalimu wetu ni ndogo sana.

Dada Shonza ukiwa kama naibu waziri mwenye umri mdogo, ambaye naamini una hamu ya kutaka kuwa kama kina Mama Anna Makinda ndani ya miaka kadhaa ijayo, anza kwa kumshauri waziri wako juu ya kuja na mkakati mpya wa usimamiaji wa taaluma za waalimu wa michezo.

Nakutakia kazi njema, nakutakia maisha mema. Dada Juliana Shonza.
 
Hawezi kukuelewa, taaluma yake ni kujibishana na wapinzani.
Huko unampeleka kukubwa sana. Pengine ataisimamia vizuri tasnia ya mziki wa Taarabu.
 
Back
Top Bottom